Maandamano Tanzania: 'Mwanangu alipigwa risasi akafariki akielekea dukani'

Maelezo ya sauti, Maandamano Tanzania: 'Mwanangu alipigwa risasi akafariki akielekea dukani'
Muda wa kusoma: Dakika 1

Familia za watu waliowapoteza wapendwa wao kwenye maandamano yaliyotokea baada ya uchaguzi mkuu nchini Tanzania, wanaendelea shughuli za kuandaa mazishi ya wapendwa wao huku wengine nao wakiendelea kuomboleza baada ya shughuli hiyo kukamilika. ripoti zinasema kuwa watu wengi walipoteza maisha kwenye maandamano hayo.

Mjini Mbea Famili ya Daktari mmoja ambaye mtoto wake aliuawa baada ya kupigwa risasi kifuani na maafisa wa Ulinzi amesema kuwa familia yake daima itasalia na makovu ya uchaguzi wa mwaka huu.

Daktari huyu anasema kuwa mwanawe aliuawa wakati alipokuwa akienda dukani na kwa bahat nzuri tayari wamekamilisha shughuli za mazishi.