Mabomu ya nyuklia yaliyopotea ambayo hakuna mtu anayeweza kuyapata

Mabaki ya momu

Chanzo cha picha, Getty Images

Marekani imepoteza bomu tatu za nyuklia ambazo hazijawahi kupatikana- hadi wa leo. Bomu hizo zilipotea katika mazingara gani? Zinaweza kuwa wapi? Na je zitawahi kupatikana?

Ilikuwa asubuhi ya majira ya baridi kali katika kilele cha Vita Baridi.

Mnamo Januari 17,1966, karibu saa 04:30 asubuhi, mvuvi wa Kihispania aliona kitu cheupe kikianguka kutoka angani…na kuteleza kimya kimya kuelekea Bahari ya Alboran.

Ilikuwa ni kitu kinachonig’inia chini ya maji, ingawahakuweza kujua ni nini. Kisha ikapotea chini ya mawimbi.

Wakati hayo yakifanyika,katika kijiji cha karibu cha Palomares,wenyeji walipowaliona tukio tofauti angani.

Mipira miwili mikubwa ya moto, ikielekea upande wao. Ndani ya sekunde chache, Kijiji cha idyll kilikuwa kimesambaratika. Majengo yalitikisika. Vipande vya chuma iliyokatika ilikuwa ikianguka ardhini.

Wiki chache baadaye, Philip Meyers alipokea ujumbe kupitia teleprinter – kifaa kinachofanya kazi kama fax na ambacho kilikuwa na uwezo wa kutuma na kupokea barua pepe.

Wakati huo alikuwa akifanya kazi kama afisa wa kutegua bomu kayika kambi ya jeshi la majini la Sigonella, mashariki mwa mji wa Sicily. Aliambiwa kuwa kuna siri ya dharura nchini, na kwamba alitakiwa kufika mahali hapo ndani ya siku chache. 

Msako unaendelea

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Hata hivyo oparesheni hiyo haikuwa ya siri kama vile jeshi lilivyotarajia. "Haikushangaza kuitwa kazini," alisema Meyers.

Hata watu walijua nini kilikuwa kikiendelea. Alipohudhuria karamu cha chakula cha jioni siku hiyo na kutangaza safari yake ya ajabu, usiri wake uliokusudiwa ukawa kitu cha mzaha.

"Ilikuwa aibu kusema kweli," asasema Meyers. "Ilipaswa kuwa sirisiri lakini marafiki zangu walikuwa wakiniambia wanajua kwa nini nilikuwa naenda."

Kwa wiki kadhaa, magazeti duniani yamekuwa yakiripoti uvumi kuhusu ajali mbaya– ndege mbili za jeshi la Marekani zilikuwa zimegongana, kutawanya mabomu manne ya nyuklia ya B28 kote mjini Palomares.

Matatu yalipatikana haraka ardhini lakini moja lilikuwa limetoweka kwenye anga ya bluu inayometa kusini mashariki, likapotea chini ya bahari ya Mediterania iliyo karibu.

Sasa msako ulikuwa ukiendela ili kuitafuta pamoja na kichwa chake cha uzani megatani 1.1, chenche uwezo wa kulipua tani 1,100,000 za TNT

Idadi isiyojulikana

Tukio la Palomares sio wakati pekee silaha ya nyuklia imetoweka. Kumekuwa na angalau ajali 32 zinazojulikana kama "mshale uliovunjika" - zile zinazohusisha vifaa hivi vyamaangamizi- tangu 1950.

Mara nyingi, silaha ziliangushwa kwa kimakosa, kisha kupatikana tena. Lakini mabomu matatu ya Marekani yametoweka kabisa - bado yako nje hadi leo, yakinyemelea kwenye vinamasi, mashamba na bahari katika sayari nzima.

"Kwa kiasi kikubwa tunajua kuhusu kesi za Marekani," anasema Jeffrey Lewis, mkurugenzi wa Mpango wa Kuzuia Uenezi wa silaha za nyuklia wa Asia Mashariki katika Kituo cha James Martin cha Mafunzo ya Kuzuia Uenezi wa silaha hizo, California.

Anaeleza kuwa orodha kamili iliibuka tu wakati muhtasari uliotayarishwa na Idara ya Ulinzi ya Marekani ulipotolewa katika miaka ya 1980.

Mengi yalitokea wakati wa Vita Baridi, wakati taifa lilipozama kwenye genge la Maangamizi ya Pamoja (MAD) na Umoja wa Kisovieti - na hivyo kuweka ndege zenye silaha za nyuklia angani wakati wote kutoka 1960 hadi 1968, katika operesheni iliyojulikana kama Chrome Dome.

"Hatujui mengi kuhusu nchi nyingine. Hatujui chochote kuhusu Uingereza au Ufaransa, au Urusi au China," anasema Lewis. "Kwa hivyo sidhani kama tuna hesabu kamili."

Historia ya nyuklia ya Umoja wa Kisovieti ni mbaya sana - ilikuwa imekusanya akiba ya silaha za nyuklia 45,000 kufikia 1986.

Kuna visa vinavyojulikana ambapo nchi ilipoteza mabomu ya nyuklia ambayo hayajawahi kupatikana, lakini tofauti na matukio ya Marekani, yote yalitokea kwenye manowari. na maeneo yao yanajulikana.

Leo, ulinzi wa nyuklia wa Marekani unajumuisha makombora ya balestiki ya ardhini (ICBMs), ndege za bomu, na nyambizi za makombora ya balestiki (SSBNs)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Leo, ulinzi wa nyuklia wa Marekani unajumuisha makombora ya balestiki ya ardhini (ICBMs), ndege za bomu, na nyambizi za makombora ya balestiki (SSBNs)

Moja ilianza tarehe 8 Aprili 1970, wakati moto ulipoanza kuenea kupitia mfumo wa kiyoyozi wa manowari ya Soviet K-8 yenye nguvu ya nyuklia ilipokuwa ikipiga mbizi kwenye Ghuba ya Biscay - sehemu ya maji yenye hila kaskazini mashariki mwa Bahari ya Atlantiki karibu na pwani ya Uhispania na Ufaransa, ambayo ni maarufu kwa dhoruba zake kali.

Ilikuwa na torpedo nne za nyuklia, na ilipozama mara moja, ilichukua shehena yake ya mionzi.Hata hivyo , Marekani iligundua na kuamua kufanya jaribio la siri la kupata silaha hizo za nyuklia, "hatua ambayo ilikuwa ya kushangazacrazy", anasema Lewis.

Timu ya watafutaji iliomba usaidizi wa uvumbuzi wa aina mbili. Mojawapo ilikuwa nadharia isiyoeleweka ya Karne ya 18 iliyobuniwa na waziri wa Presbyterian aliyegeuka kuwa mwanahisabati ambaye huwasaidia watu kutumia taarifa kuhusu matukio ya zamani ili kuhesabu uwezekano wa kutokea tena.

Walitumia mbinu hii ya " Bayesian inference" kuamua wapi pa kutafuta bomu ili kuwasaidia kutafuta kwa njia bora zaidi iwezekanavyo na kuongeza nafasi zao za kuipata.

Ya pili ilikuwa "Alvin", manowari ya kisasa ya kina kirefu inayoweza kupiga mbizi kwenye kina kisicho cha kawaida. Kama papa mweupe, kila siku anashuka kwenye maji ya bluu ya Mediterania akiwa na timu yake tumboni na kuanza kuwinda kwa macho.

Mabomu matatu yaliyopotea

Bomu moja la nyuklia Mark 15.

Wapi? Kisiwa cha Tybee, Georgia.

Lini? Februari 5 1958.

Ikuaje? lilirushwa kwa ndege ili kupunguza uzito wa ndege ili kutua kwa usalama zaidi.

Bomu moja la nyuklia la B43.

Wapi? Bahari ya Ufilipino.

Lini? Desemba 5 1965.

Namna ilivyokuwa?Ndege yenye bomu, rubani na silaha ya nyuklia iliteleza kutoka kwenye kando ya mashua ya kubebea mizigo, haikuonekana tena. Bomu moja la nyuklia la B28FI

likiwa hatua ya pili.

Wapi? Kituo cha Hewa cha Thule, Greenland.

Lini? 22 Mei 1968.

Namna gani? Moto ndani ya ndege uliwalazimu wafanyakazi kuondoka na kuiacha ndege hiyo kuanguka ikiwa na mzigo wake wa nyuklia.

Alvin iliyokuwa chini ya maji ilikaribia kuvutwa hadi kilindini ilipodondosha bomu la Palomares

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Alvin iliyokuwa chini ya maji ilikaribia kuvutwa hadi kilindini ilipodondosha bomu la Palomares

Mnamo tarehe 1 Machi 1966, kikundi kidogo hatimaye kiliona kitu: mlio wa bomu wakati lilipogonga chini ya bahari kwa mara ya kwanza.

Picha za baadaye zilifichua tukio la kuogofya ncha ya mviringo ya silaha ya nyuklia iliyopotea, iliyofunikwa na parachuti nyeupe, ambayo ilikuwa imerushwa nayo ilipoanguka, ikajichanganya yenyewe na shehena yake ya thamani.

Bomba hili la chuma hatari limefanana kwa kiasi Fulani na mtu aliyevaa kwa ajili ya Halloween katika shuka.

Lakini mapambano hayajaisha. Sasa ilikuwa kazi ya Meyers kutafakari jinsi ya kulitoa bomu hili kwenye sakafu ya bahari ambapo lilikuwa na kina cha futi 2,850 (869m).

Waliboresha aina ya njia ya uvuvi kutoka kwa futi elfu chache kwa kamba nzito ya nailoni na ndoano ya chuma, wazo lilikuwa kushikilia kifaa na kukivuta hadi kiwe karibu zaidi na uso wa bahari kiasi kwamba mzamiaji angeweza kwenda chini na kulitoa. "Huo ndio ulikuwa mpango. Haukufaulu," anasema Meyers. "Yote yalifanyika kwa makusudi sana na kwa tahadhari na polepole," anasema Meyers. "Kwa hivyo tulingoja tu ... tulikuwa na wasiwasi, tukitaka kuona tutafanya nini wakati linakuja juu."

Walifanikiwa kulinasa bomu la nyuklia na kuanza kuliinua kutoka kwenye maji.

Walikuwa wameliinua kutoka chini wakati maafa yalipotokea. Parashuti, iliyofufuliwa kutoka kwenye sakafu ya bahari, ghafla ilianza kupunguza kasi ya mzigo na kuifanya kuwa vigumu kusogea