Ngono kwa njia ya mdomo chanzo kikuu cha Saratani ya koo- Utafiti

The Conversation

Cancer

Chanzo cha picha, The Conversation via Alamy

Katika kipindi cha miongo miwili iliyopita, kumekuwa na ongezeko kubwa na la kasi la saratani ya koo katika nchi za magharibi, kiasi kwamba wengine wameliita janga.

Hii imetokana na ongezeko kubwa la aina maalum ya saratani ya koo inayoitwa saratani ya oropharyngeal (eneo la tonsils au mafindofindo na nyuma ya koo). Chanzo kikuu cha saratani hii ni human papillomavirus (HPV) ambayo pia ndiyo chanzo kikuu cha saratani ya shingo ya kizazi. Saratani ya Oropharyngeal sasa imekuwa ya kawaida zaidi kuliko saratani ya shingo ya kizazi nchini Marekani na Uingereza.

HPV inaambukizwa ngono. Kwa saratani ya oropharyngeal, sababu kuu ya hatari ni kuwa na idadi kubwa ya wenzi wa kingono maishani, haswa ngono ya mdomo.

Wale walio na wenzi sita au zaidi katika maisha yao wana uwezekano mkubwa wa takribani mara 8 na nusu wa kupata saratani aina ya oropharyngeal kuliko wale ambao hawafanyi ngono kwa njia ya mdomo.

Uchunguzi wa mienendo ya tabia unaonyesha kuwa ngono ya mdomo imeenea sana katika baadhi ya nchi. Katika utafiti ambao mimi na wenzangu tulifanya kwa kutumia karibu watu 1,000 waliokuwa na tonsillectomy kwa sababu zisizo za kansa nchini Uingereza, 80% ya watu wazima waliripoti kushiriki ngono kwa njia ya mdomo katika kipindi fulani cha maisha yao. Walakini, ni idadi ndogo tu ya watu hao wanaougua saratani ya oropharyngeal. Kwa nini ni iko hivyo, ukweli haijulikani mpaka sasa.

Nadharia iliyopo ni kwamba wengi wetu hupata maambukizi ya HPV na tunaweza kuyaondoa kabisa. Hata hivyo, idadi ndogo ya watu hawawezi kuondokana na maambukizi, labda kutokana na kasoro katika mfumo wao wa kinga. Kwa wagonjwa hao, virusi vinaweza kujirudia mfululizo, na baada ya muda huweza hata kuingia kwenye vinasaba na kusababisha seli za aliyevibeba kuwa na saratani.

Cancer

Chanzo cha picha, The conversation

Chanjo ya HPV kwa wasichana wadogo imekuwa ikifanyika katika nchi nyingi ili kuzuia saratani ya mlango wa kizazi. Sasa kuna ongezeko, ingawa ushahidi usio wa moja kwa moja, unaonyesha kwamba inaweza pia kuwa na ufanisi katika kuzuia maambukizi ya HPV mdomoni. Pia kuna ushahidi unaopendekeza kwamba wavulana pia wanalindwa na "kinga inayopigwa na wasichana wengi" katika nchi ambazo kuna viwango vya juu vya chanjo kwa wasichana (zaidi ya 85%). Kwa pamoja, hii inaweza kusababisha katika miongo michache ijayo kupunguza saratani ya oropharyngeal.

Wavulana wanapaswa kuchomwa chanjo ya HPV pia

Throat Cancer

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Muonekano wa saratani ya koo

Umuhimu wa hili umesababisha nchi kadhaa, kwa mfano Uingereza, Australia na Marekani, kupanua wigo wa mapendekezo yao ya kitaifa ya chanjo ya HPV kujumuisha wavulana wadogo - inayoitwa sera ya chanjo kwa wote (isiyopendelea kijinsia).

Lakini kuwa na sera ya chanjo kwa wote sio uhakikika wa chanjo. Kuna idadi kubwa ya baadhi ya watu ambao wanapinga chanjo ya HPV kwa sababu ya wasiwasi kuhusu usalama, umuhimu, au, mara chache sana, wenye wasiwasi kwamba inahimiza uasherati.