AI: Je, ni mianya gani ya uhalifu wa kifedha ya benki inayosababishwa na teknolojia hii?

fedha

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Akili Mnemba (AI) kwa sasa imesababisha wasiwasi wa makampuni, nyota wa filamu na viongozi wa kisiasa.

AI ni moja ya mabadiliko mengi yanayoletwa na maendeleo ya kiteknolojia. Kila mahali kuna wasiwasi kuhusu teknolojia ya kina ya kughushi ambayo akili mnemba imeleta.

Hivi karibuni, video za waigizaji wengine maarufu zinaenea kwa kasi kutokana na Deep Fake (aina ya akili mnemba inayotumiwa kutengeneza picha zenye kusadikisha, ulaghai wa sauti na video.)

Wataalamu wa teknolojia wana wasiwasi kuhusu matatizo ambayo teknolojia hii italeta.

Je, ni mianya gani ya uhalifu wa kifedha sasa italetwa teknolojia hii? Ni tahadhari gani zinazopaswa kuchukuliwa ili kuepuka kunasa kwenye mtego huu?

Makala haya yanaainisha;

Aina mbili za uhalifu wa kifedha

Hadi sasa, watu wanatapeliwa na kuibiwa pesa kutoka kwenye akiba zao za benki kwa njia mbili.

1. Uhalifu kama vile kuchukua pesa kutoka kwenye akaunti ya benki ya watu kwa kupata OTP na nywila zao kwa idhini yao kwa kisingizio cha kupata mapato zaidi.

Mnamo mwaka wa 2019 pekee, pesa zilizopotea na watu kutoa maelezo yao ya binafsi nchini India kwa mfano kwa watu wasiojulikana inakadiriwa kuwa karibu Rupia elfu 50.

Aina hizi za ulaghai hufanywa kupitia mikopo ya binafsi na UPI inayotolewa na taasisi na programu mbalimbali za fedha. Tunaweza kuepuka ulaghai huo kwa kutotoa taarifa zetu binafsi kwa wengine.

2. Aina ya pili ni pale watu wanapotapeli pesa zao kwa kudukua akaunti ya benki au kuiba nenosiri bila kushiriki maelezo ya akaunti zao za benki na taarifa nyinginezo na mtu yeyote. Serikali na benki zinachukua hatua mbalimbali kuzuia ulaghai huo.

Lakini matatizo yanayosababishwa na akili mnemba na matatizo yanayosababishwa na deep fake yanatofautiana. Kwa sababu deepfake inaweza kutengeneza mtu bandia kidigitali ili aonekane mtu halisi.

v

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Wakati wa uchaguzi tumeona baadhi ya wagombea wakitengeneza wasifu ghushi na kuharibu nafasi za wagombea wengine kushinda. Inawezekana pia kufanya shughuli za kifedha kupitia wasifu bandia.

Kwa mfano, ikiwa watu wa familia yetu wanatupigia simu na kutuomba tutume pesa kwenye nambari ya akaunti ya benki, tunatuma bila kusita. Kwa sababu tunaamini kwamba aliyepiga simu ni mwanafamilia wetu.

Lakini, kwa akili mnemba, kuna uwezekano kwamba mtu mwingine atazungumza kama mshiriki wa familia yetu. Hata benki hazitatambua shughuli hii kama ya ulaghai.

Mnamo mwaka wa 2019, Jarida la Wall Street liliandika kwamba mtendaji mkuu wa kampuni ya nishati ya Uingereza alikuwa mwathirika wa kashfa kama hiyo. Hatari ya ulaghai kama huo huenda ikasumbua kila mtu kutoka kwa watu mashuhuri hadi watu wa kawaida.

Sasa hebu tuone ni aina gani ya uhalifu wa kifedha inaweza kufanywa kwa mbinu hii ya Deep Fake, (aina ya akili mnemba inayotumiwa kutengeneza picha zenye kusadikisha, ulaghai wa sauti na video.)

n

Chanzo cha picha, Getty Images

Athari za Akili Mnemba

Kama ilivyotajwa hapo juu, kutengeneza nakala ya kidijitali kama mtu na kupata faida kutokana na hilo itakuwa suala kubwa katika siku zijazo. Maendeleo ya kiteknolojia yatarahisisha hili.

Kuna uwezekano wa kueneza uvumi kuhusu utendaji kazi wa taasisi za fedha au utendaji kazi wa taasisi fulani ikiwa kana kwamba ni ripoti rasmi ya taasisi hiyo.

Hapo awali, kulikuwa na uvumi kwamba mashine za ATM za Benki ya ICICI, benki ya kimataifa ya India na kampuni ya huduma za kifedha yenye makao yake makuu mjini Mumbai, hazikupokea pesa taslimu, hivyo wateja wa benki hiyo walisubiri kwenye foleni ili kuchukua fedha kutoka kwenye akaunti zao za benki.

Hivyo kama kampuni inapotosha wawekezaji kwamba utendaji wa kampuni si mzuri, inaweza kusababisha hasara kubwa kwa kampuni hiyo.

Baada ya sheria kuhusu BlueTick kubadilishwa kwenye njia ya X (Twitter), baadhi ya watu walianzisha akaunti kwa jina la makampuni maarufu na kueneza habari za uongo.

Matukio hayo yalipotokea, Kampuni X iliyatambua na kuchukua hatua stahiki. Lakini ni vigumu sana kuepuka habari au matukio kutoka kwa teknolojia ya 'deepfake'.

Je, ni hatua gani za tahadhari za kuchukua?

Teknolojia ya kijasusi bandia inaweza pia kuwashawishi watu kwamba serikali au taasisi za fedha zimebadilisha sheria zao.

Kwa mfano, ikiwa habari itaenea kwamba serikali inaondoa msaada wa kifedha kwa sekta fulani, wawekezaji wataondoa uwekezaji wao kutoka kwenye sekta hiyo. Kwa kufanya hivi, thamani ya soko ya makampuni katika sekta itashuka hadi kiwango cha chini sana na kusababisha hasara kubwa kwa wawekezaji.

Na habari kwamba serikali imeainisha sekta fulani ya kuweka kipaumbele itaelekeza uwekezaji kwenye sekta hiyo. Teknolojia ya kina hurahisisha sana kueneza habari hizo za uwongo.

Hebu tuone ni tahadhari gani ambazo mwekezaji wa kawaida anaweza kuchukua ili kuhakikisha usalama wetu wa kifedha hauathiriwi:

1. Usitegemee faida kubwa

Mradi wowote wa mapato ya juu unapaswa kufanyiwa utafiti wa kina.

Usiamini maneno au maoni ya mtu yeyote. Chukua muda wako na usome mwenyewe. Angalia ikiwa mipango kama hiyo ilikuwapo hapo awali.

Ikiwa una shaka, usiwekeze kwao.

Kwa sababu ni muhimu zaidi kulinda pesa tulizonazo kuliko maslahi yanayopatikana kwetu. Hii ni moja ya kanuni binafsi za fedha.

Usiamini maneno au maoni ya mtu yeyote. Chukua muda wako na usome mwenyewe.

Chanzo cha picha, Getty Images

2. Usishirikishe mtu taarifa za siri kama vile OTP, PIN n.k.

Kwa hali yoyote usitoe taarifa kama ya OTP na PIN kwa wengine. Hakuna shirika lililo na haki au sharti la kupata taarifa kama vile OTP yako.

3. Usisumbuke

Ukipata habari hasi kuhusu sera au makampuni ambayo umewekeza, subiri kwa siku chache bila kuchukua hatua yoyote ya haraka. Amini tu ripoti rasmi za vyombo vya habari.

Kumbuka kwamba akili mnemba ina uwezo wa kupenyeza hata vyombo vya habari vya kawaida.

4. Mipango ya muda mrefu

Kupanga na kuwekeza kwa muda mrefu ni msingi wa usimamizi wa binafsi wa kifedha.

Kwa kuwekeza kama hivi, makampuni yanaweza kupona kutokana na mashambulizi.

Kampuni zinazofanya vizuri hurejea haraka. Warren Buffett amekuwa na hisa alizowekeza katika Kampuni ya Coca-Cola kwa miongo kadhaa. Huu ni mfano mzuri wa mipango ya muda mrefu.

(Kumbuka: Makala haya ni ya uelewa wa jumla wa mada mahususi pekee. Maamuzi yanapaswa kuchukuliwa kwa kushauriana na washauri wako wa kifedha wa binafsi.)