Papa asema makasisi wa Kanisa Katoliki wanaweza kuwabariki wapenzi wa jinsi moja

g

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Papa Francis anasema watu kubarikiwa hakuhitaji "ukamilifu wa kimaadili"

Papa Francis amewaruhusu mapadre kuwabariki wapenzi wa jinsi moja, yakiwa ni maendeleo makubwa kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsi moja na mahusiano mengine ya kijinsia wanaofahamika kama LGBT katika Kanisa Katoliki la Roma.

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki la Roma amesema makasisi wanapaswa kuruhusiwa kuwabariki wapenzi wa jinsi moja na wanandoa "isiyo ya kawaida", kwa misingi ya hali fulani.

Lakini Vatican ilisema baraka hazipaswi kuwa sehemu ya taratibu za kawaida za Kanisa au zinazohusiana na miungano ya kiraia au harusi.

Iliongeza kuwa inaendelea kuiona ndoa kuwa kati ya mwanamume na mwanamke.

Papa Francis aliidhinisha waraka uliotolewa na Vatican kutangaza mabadiliko hayo siku ya Jumatatu.

Vatican ilisema inapaswa kuwa ishara kwamba "Mungu anawakaribisha wote", lakini hati hiyoinasema Makasisi lazima waamue kwa kuzingatia uhalisia wa kila tukio.

Akitambulisha andiko hilo, Kardinali Víctor Manuel Fernández, ambaye ni msimamizi wa Kanisa, alisema kwamba tamko jipya limebakia kuwa "imara kwenye fundisho la kimapokeo la Kanisa kuhusu ndoa".

Lakini aliongeza kuwa kwa kuzingatia "maono ya kichungaji" ya Papa" ya "kupanua" ombi la Kanisa Katoliki, miongozo mipya inawaruhusu mapadre kubariki uhusiano ambao bado unachukuliwa kuwa wa dhambi.

Watu wanaopokea baraka "haifai kuhitajika kuwa na ukamilifu wa kimaadili wa awali", kulingana na tamko hilo.

Katika Kanisa Katoliki, baraka ni maombi au ombi, ambalo kwa kawaida hutolewa na mhudumu, akimwomba Mungu ambariki mtu au watu wanaobarikiwa.

Kardinali Fernández alisisitiza kwamba msimamo huo mpya hauhalalishi hadhi ya wapenzi wa jinsia moja mbele ya Kanisa Katoliki.

Unaweza pia kusoma:

Tamko hilo linawakilisha urejeshaji wa sauti kutoka kwa Kanisa Katoliki, ingawa sio mabadiliko ya msimamo.

Mnamo 2021, Papa alisema makasisi hawawezi kubariki ndoa za watu wa jinsia moja kwa sababu Mungu hawezi "kubariki dhambi".

Mnamo mwezi Oktoba Papa Francis alikuwa amependekeza kwamba alikuwa wazi kuhusu Kanisa kuwabariki wapenzi wa jinsi moja.

Maaskofu katika nchi fulani hapo awali wameruhusu mapadre kuwabariki wapenzi wa jinsi moja, ingawa msimamo wa mamlaka ya Kanisa haikufahamika wazi.

Unaweza pia kusoma:

Imetafsiriwa na Dinah Ghamanyi