Afisa wa zamani afichua maelezo mapya ya mauaji ya JF Kennedy

fgdv

Chanzo cha picha, Getty Image

Maelezo ya picha, Gavana wa Texas, John Connally akitengeneza tai yake wakati John F Kennedy na mke wake Jackie Kennedy wameketi siti ya nyuma

Miongo sita baadaye, maelezo mapya yanakuja juu ya mojawapo ya matukio yaliyochunguzwa sana katika historia ya Marekani; mauaji ya Rais John F Kennedy.

Paul Landis, 88, afisa wa zamani wa Secret Service ambaye alishuhudia kifo cha rais kwa karibu, anasema katika kitabu kitakacho chapishwa karibuni, alichukua risasi kutoka katika gari baada ya Kennedy kupigwa, na kisha kuiacha kwenye machela ya hospitalini.

Inaweza kuonekana ni kama maelezo kidogo katika kesi ambayo imekuwa ikichambuliwa tangu miaka ya 1960, lakini kwa mtu ambaye ametumia miongo kadhaa kuangalia kila sehemu ya ushahidi, maneno ya Landis ni muendelezo mkubwa.

Kitabu chake The Final Witness, itategemea ni jinsi gani mtu anavyoitazama kadhia hiyo – kwani kauli za Landis zinaweza kubadilisha mambo ama zisibadilishe chochote.

"Hii ni habari muhimu katika mauaji ya 1963," anasema James Robenalt, mwanahistoria na mtaalamu aliyefanya kazi na Landis kutayarisha ufichuzi wake wa umma.

Maelezo mapya katika kesi ya zamani

Tarehe 22 Novemba 1963, gari iliyokuwa imembeba Rais Kennedy, mke wake Jackie Kennedy, na Gavana wa Texas John Connally Jr huko Dallas ndipo iliposhambuliwa.

Bwana Kennedy alipigwa kichwani na shingoni, na Connally akapigwa mgongoni. Wote wawili walikimbizwa hospitali ya karibu ya Parkland Memorial, ambapo Kennedy alitangazwa kuwa amefariki. Gavana alinusurika.

Ripoti ya Tume ya Warren, iliyotokana na uchunguzi wa serikali kuhusu mauaji hayo, ilimtambua Lee Harvey Oswald kama mshambuliaji pekee aliyekuwa na bunduki. Alipigwa risasi na kuuawa muda mfupi baada ya mauaji hayo akiwa chini ya ulinzi wa polisi.

Tume hiyo ilieleza kwamba risasi moja ilipatikana baadaye kwenye machera ya hospitali. Hakuna mtu aliyejua ilitoka wapi. Lakini kamati ilihitimisha kwamba risasi ilikuwa imetolewa na madaktari wakati wa kumtibu Connally.

Anachokumbuka Paul Landis

refd

Chanzo cha picha, Getty Image

Maelezo ya picha, Polisi wa Dallas amebeba bunduki iliyotumika kumuuwa Rais John F Kennedy
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Siku ya mauaji, Landis, wakati huo alikuwa na umri wa miaka 28, alikuwa mlinzi wa Jackie Kennedy. Shambulizi lilipotokea alikuwa karibu na Rais Kennedy na kushuhudia risasi ikipiga kichwani mwa Kennedy.

Katika mahojiano na gazeti la New York Times, Landis alisema baada ya msafara wa magari kufika hospitalini, aliona risasi ikiwa kwenye gari la Kennedy nyuma ya kiti cha rais alichokuwa ameketi.

Akaichukua na kuiweka mfukoni. Muda mfupi baadaye, katika kumbukumbu zake, akiwa kwenye chumba cha dharura na Rais Kennedy. Anasema aliiweka kwenye machera ili ushahidi usafiri na mwili.

"Hakukuwa na mtu wa kulinda eneo la tukio, na jambo hilo lilinisumbu sana," Landis aliambia Times. "Ulikuwa ni ushahidi muhimu ambao sikutaka kuona ukipotea au kutoweka."

Inaonekana Landis hakuwahi kueleza ushahidi huu, na Tume ya Warren haikumhoji kamwe. Hakuwahi kuiandika katika ripoti yoyote rasmi.

"Alisahau kuhusu risasi," anasema Robenalt, ambaye alitumia muda mwingi kumhoji Landis kuhusu kumbukumbu zake. "Alikuwa bize na mambo mengi yaliyokuwa yakiendelea."

Kwa miaka mingi, aliepuka kusoma kuhusu mauaji au nadharia za njama ya mauaji - hadi alipoamua kuwa yuko tayari kueleza ulimwengu hadithi yake.

Risasi

Wale ambao wamesikia Landis wanaamini simulizi yake inazusha maswali mengi kuliko inavyoweza kujibu. Landis anaamini kwamba risasi aliyoipata kwenye gari ndiyo iliyompata Connally.

Ikiwa yuko sahihi, Robenalt anasema, Connelly na Kennedy huenda hawakupigwa na risasi moja. Anaamini kuwa inaweza kufungua tena maswali kuhusu iwapo Oswald alitenda peke yake.

Kama isingekuwa risasi moja iliyosababisha majeraha ya wanaume wote wawili, Robenalt anauliza; Je, Oswald angeweza kufyatua risasi zote mbili mfululizo kwa kasi hiyo na bunduki aliyotumia?

Clint Hill, afisa ambaye aliruka nyuma ya gari la Kennedy kumlinda rais, haamini maelezo ya Landis. "Ikiwa alikagua ushahidi wote, taarifa, mambo yaliyotokea, vyote haviendani na anachosema yeye," Hill aliambia NBC News.

Gerald Posner, mwandishi wa habari za uchunguzi na mwandishi wa kitabu cha: Lee Harvey Oswald na Mauaji ya JFK, anasema "maneno yake yanapaswa kuchukuliwa kwa uzito", lakini pia ana shaka kuhusu uhakika wa kumbukumbu za Landis baada ya takriban miongo sita kupita.

Kwa mfano, Posner alieleza kwenye mahojiano juu ya watu waliokuwa katika chumba cha dharura na Kennedy katika hospitali ya Parkland. Hakuna anayetaja uwepo wa Landis. Na ukweli kwamba Landis hakuwahi kujitokeza unazua maswali.

Haya ni mauaji ya Kennedy, ufunuo wake utaendelea kwa miaka mingi na mijadala yenye mgawanyiko yataendelea. "Je, utasuluhisha kwa watu wote kuridhika kwa 100%? Hapana," Bw Posner anasema. "Ni kesi ambayo haitafungwa kamwe, kwa watu wengi."