Liz Truss: Mrithi wa Boris Johnson kama kiongozi wa Tory na Waziri mkuu wa Uingereza

ggg

Chanzo cha picha, Reuters

Katika umri wa miaka saba, Liz Truss alicheza nafasi ya Margaret Thatcher kwenye maigizo yaliyohusu uchaguzi mkuu katika shule yake.

Lakini tofauti na waziri mkuu, ambaye alishinda kura nyingi mnamo 1983, hakuweza kufanikiwa.

Miaka mingi baadaye, Truss anakumbuka: "Nilijitosa katika nafasi hiyo na nikatoa hotuba ya iliyogusa moyoni kwenye mikutano ya uchaguzi, lakini nikaishia kupata kura sifuri. Hata sikujipigia kura."

Miaka thelathini na tisa mbele, anajitosa kwenye nafasi hiyo kufuata nyayo za uongozi wa Iron Lady katika maisha ya kweli kuwa kiongozi wa Conservative na waziri mkuu.

Waziri huyo wa mambo ya nje alimfuata aliyekuwa Kansela Rishi Sunak katika awamu zote tano za upigaji kura wa wabunge wa Tory.

TH

Lakini washika dau ndio walipendelea ashinde, akiwa ametumia miaka mingi kujenga uhusiano na vyama vya maeneo bunge na kubaki mwaminifu kwa Boris Johnson wakati wa siku mbaya zaidi za uwaziri mkuu wake.

Kwa njia nyingi, yeye sio mwanachama wa Tory wa kawaida.

Mary Elizabeth Truss alizaliwa Oxford mwaka 1975. Analeza kuwa baba yake ni profesa wa hisabati na mama yake ni nesi.

Akiwa msichana mdogo, mama yake alishiriki maandamano kwa ajili ya Kampeni ya Kupunguza Silaha za Nyuklia, shirika lililopinga vikali uamuzi wa serikali ya Thatcher kuruhusu vichwa vya nyuklia vya Marekani kuwekwa katika kituo cha anga cha RAF Greenham Common, magharibi mwa London.

Unaweza pia kusoma

Liz Truss: Maelezo ya msingi

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Umri: 47

Mahali pa kuzaliwa: Oxford

Nyumbani: London na Norfolk

Elimu: Shule ya Roundhay huko Leeds, Chuo Kikuu cha Oxford

Familia: Ameolewa na mhasibu Hugh O'Leary na ana mabinti wawili vijana

Eneo bunge: Kusini Magharibi mwa Norfolk Familia ilihamia Paisley, magharibi mwa Glasgow, wakati Truss akiwa na umri wa miaka minne.

Akiongea na BBC kaka yake alisema familia ilifurahia kucheza michezo ya ubao, lakini Truss akiwa mdogo alichukia kupoteza na mara nyingi alitoweka alipoona kuna hatari ya kutoshinda.

Familia hiyo baadaye ilihamia Leeds, ambapo alisoma Roundhay, shule ya sekondari ya serikali. Ameelezea kuona "watoto waliofeli na kukatishwa tamaa na matarajio madogo" wakati alipokuwa huko.

Baadhi ya wanafunzi wa rika la Truss huko Roundhay wamepinga maelezo yake kuhusu shule hiyo, akiwemo mwandishi wa habari wa Guardian Martin Pengelly, ambaye aliandika: "Labda anachagua kupeleka malezi yake, na kutafsiri kwa urahisi shule na walimu waliomlea, kwa manufaa rahisi ya kisiasa."

Bila kujali masomo yake, Truss alifika Chuo Kikuu cha Oxford, ambako alisoma falsafa, siasa na uchumi na alikuwa akijishughulisha na siasa za wanafunzi, awali akiwa na chama cha Liberal Democrats.

Katika mkutano wa chama wa 1994, alizungumza kuunga mkono kukomeshwa kwa utawala wa kifalme, akiwaambia wajumbe huko Brighton: "Sisi Wanademokrasia wa Kiliberali tunaamini fursa kwa wote. Hatuamini watu wamezaliwa kutawala."

Matarajio ya westminster

Huko Oxford, Truss alihamia Conservatives.

Baada ya kuhitimu alifanya kazi kama mhasibu wa Shell, na Cable & Wireless, na alifunga ndoa na mhasibu mwenzake Hugh O'Leary mwaka wa 2000. Wanandoa hao wana watoto wawili.

Truss alisimama kama mgombea wa Tory wa Hemsworth, West Yorkshire, katika uchaguzi mkuu wa 2001, lakini alishindwa.

Truss alishindwa tena huko Calder Valley, pia huko West Yorkshire, mnamo 2005.

Lakini, matarajio yake ya kisiasa hayajafifishwa, alichaguliwa kama diwani huko Greenwich, kusini-mashariki mwa London, mwaka wa 2006 na kuanzia 2008 pia alifanya kazi katika taasisi ya wataalamu wa Mageuzi ya right-of-centre Reform think tank.

ggg

Chanzo cha picha, PA Media

Maelezo ya picha, Liz Truss alikua mbunge mnamo 2010

Kiongozi wa chama cha Conservative David Cameron alimweka Truss kwenye "orodha A" ya wagombea waliopewa kipaumbele katika uchaguzi wa 2010 na alichaguliwa kuwania kiti salama cha Norfolk Kusini Magharibi.

Lakini alikabiliwa vita wakitaka kuondolewa katika uteuzi na chama cha Tory , baada ya kufichuliwa kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mbunge wa Tory Mark Field miaka kadhaa iliyopita

Juhudi za kumfukuza hazikufaulu na Truss aliendelea na kushinda kiti hicho kwa zaidi ya kura 13,000.

Aliandika kitabu cha Britannia Unchained kwa kushirikiana na wabunge wengine wanne wa Conservative waliochaguliwa mwaka 2010, ambacho kilipendekeza kuondolewa kwa udhibiti wa serikali ili kuongeza nafasi ya Uingereza duniani, na kumtambulisha kama mtetezi maarufu wa sera za soko huria wa Tory.

Wakati wa mjadala wa BBC kuhusu uongozi, alipingwa kuhusu maoni katika Britannia Unchained, yanayoelezea wafanyakazi wa Uingereza kama "miongoni mwa watu wavivu zaidi duniani". Alisisitiza kuwa hakuwa ameiandika.

Mwaka 2012, miaka miwili tu baada ya kuwa mbunge, aliingia serikalini kama waziri wa elimu na mwaka 2014 alipandishwa cheo na kuwa katibu wa mazingira.

Katika mkutano wa Wahafidhina wa 2015, Truss alikejeliwa kwa hotuba ambayo alisema, kwa sauti ya chuki: "Tunaagiza theluthi mbili ya jibini yetu. Hiyo ni aibu."

Mageuzi ya Brexit

Chini ya mwaka mmoja baadaye lilikuja bila shaka kuwa tukio kubwa zaidi la kisiasa katika kizazi - kura ya maoni ya EU.

Truss alifanya kampeni ya kubaki, akiandika katika gazeti la Sun kwamba Brexit itakuwa "janga mara tatu - sheria zaidi, aina zaidi na ucheleweshaji zaidi wakati wa kuuza EU".

Hata hivyo, baada ya upande wake kushindwa, alibadili mawazo yake, akisema kwamba Brexit ilitoa fursa ya "kuyumbisha jinsi mambo yanavyofanya kazi".

Chini ya uwaziri mkuu wa Theresa May, aliwahi kuwa waziri wa sheria kabla ya kuwa waziri wa fedha.

Wakati Boris Johnson alipokuwa waziri mkuu mwaka 2019, Truss alihamishwa hadi waziri wa biashara ya kimataifa - kazi ambayo ilimaanisha kukutana na viongozi wa kisiasa na biashara ulimwenguni kukuza UK PLC.

ggg

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Liz Truss alifanya mkutano na waandishi wa habari na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov katika wiki chache kabla ya uvamizi wa Ukraine.

Mnamo 2021, akiwa na umri wa miaka 46, alihamia katika moja ya nafasi kubwa zaidi serikalini, akichukua nafasi ya Dominic Raab kama katibu wa mambo ya nje.

Katika jukumu hilo alijaribu kutatua tatizo kubwa la Itifaki ya Ireland Kaskazini, kwa kufuta sehemu za makubaliano ya baada ya Brexit EU na Uingereza, hatua ambayo EU ilikosolewa vikali.

Alifanikisha kuachiliwa kwa raia wawili wenye asili ya Uingereza na Irani ambao wote walikuwa wamekamatwa na kuwekwa kizuizini.

Na wakati Urusi ilipoivamia Ukraine mnamo Februari aliweka msimamo mkali, akisisitiza kwamba vikosi vyote vya Vladimir Putin vinapaswa kuondolewa nchini humo.

Lakini alikabiliwa na ukosoaji kwa kuunga mkono watu kutoka Uingereza ambao walitaka kupigana nchini Ukraine.

'Kupingana takrima'

Kampeni za Bi Truss kwa uongozi wa chama hazijawa na utata.

Akibanwa kuhusu atakavyokabiliana na gharama ya mzozo wa maisha, amesema ataelekeza juhudi zake katika "kupunguza mzigo wa ushuru, sio kutoa takrima".

Amelazimika kutupilia mbali mpango wa kuunganisha malipo ya sekta ya umma na gharama za maisha za kikanda baada ya kupingwa na waandamizi wa Tory ambao walisema itamaanisha malipo ya chini kwa mamilioni ya wafanyikazi nje ya London.

Na alimwita Waziri wa Kwanza wa Scotland Nicola Sturgeon "anatafuta umaarufu", akiongeza kuwa ni bora "kumpuuza".

Walakini, kura za maoni zinaonyesha kuwa yeye ni maarufu zaidi kati ya wanachama wa chama kuliko mpinzani wake Rishi Sunak.

Baadhi wanasema kuwa Truss, kupitia mavazi yake anajaribu kumuiga mwanasiasa kipenzi wa Tory Bi Thatcher.

Truss amepuuzilia mbali hili, akiambia GB News: "Inasikitisha sana kwamba wanasiasa wa kike huwa wanalinganishwa na Margaret Thatcher wakati wanasiasa wanaume hawafanani na Ted Heath."

Lakini ulinganisho kama huo sio, hasara linapokuja suala la kupata uungwaji mkono kutoka kwa wanachama wa Chama cha Conservative.