Kipimo cha saratani tofauti chaonyesha matumaini halisi katika utafiti Uingereza

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Uchunguzi wa damu kwa zaidi ya aina 50 waliokuwa na saratani umeonyesha matumaini halisi katika jaribio la taarisi ya huduma za afya nchini Uingerza NHS, watafiti wanasema.

Vipimo hivyo vilifichua saratani mbili kati ya tatu miongoni mwa watu 5,000 ambao walikuwa wamemtembelea daktari wao na dalili zinazoshukiwa, huko Uingereza au Wales.

Katika 85% ya visa hivyo chanya, pia ilibainisha tovuti ya asili ya saratani.

Kipimo cha Galleri huangalia mabadiliko tofauti katika vipande vya kanuni za kijeni zinazojitokeza kutoka kwa saratani tofauti.

Kugundua saratani inayoweza kutibika mapema kunaweza kuokoa maisha.

Kipimo hicho kinasalia kuwa "kazi inayoendelea", watafiti, kutoka Chuo Kikuu cha Oxford, wanasema, lakini kinaweza kuongeza idadi ya saratani zilizotambuliwa.

Mara nyingi, wagonjwa wana dalili, kama vile kupoteza uzito, na sababu mbalimbali zinazowezekana na huhitaji vipimo vingi na kumuona daktari hospitalini mara kwa mara.

Zaidi ya 350 ya wale walioshiriki utafiti – na la muhimu zaidi kwa wagonjwa walio na dalili zinazoshukiwa kuwa za saratani – waligunduliwa kuwa na saratani, kwa kutumia njia za kitamaduni kama vile vipimo na biopsy. Takriban:

  • Asilimia 75 ya watu waliopimwa damu waligundulika kuwa na saratani
  • Asilimia 2.5 ya waliopimwa hawakupatikana na saratani

Ingawa si sahihi vya kutosha "kubaini au kutobaini saratani", jaribio hilo lilikuwa muhimu sana, mtafiti mkuu wa wagonjwa Prof Mark Middleton aliambia BBC News.

"Kipimo kilikuwa sahihi kwa asilimia 85 katika kugundua chanzo cha saratani - na hiyo inaweza kusaidia sana kwasababu mara nyingi huwa haionekani mara moja unapokua na mgonjwa mbele yako kubaini ni kipimo gani kinahitajika ili kuona kama dalili zake ni za saratani au la," alisema.

"Kwa ubashiri huo kutoka uliotokana na kipimo, tunaweza kuamua ikiwa tutaagiza vipimo vya jumla au skani na kuhakikisha kuwa tunafanya kipimo sahihi mara ya kwanza."

Matokeo yatawasilishwa katika mkutano wa Jumuiya ya Marekani ya Kliniki za maradhi ya saratani mjini Chicago.

‘Utafiti zaidi'

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

NHS pia imekuwa ikitumia kipimo cha Galleri, kilichotengenezwa na kampuni ya California ya Grail, kwa maelfu ya watu bila dalili, ili kuona ikiwa kinaweza kugundua saratani zilizofichwa.

Matokeo ya awali yanatarajiwa mwaka ujao - na, ikiwa kitafaulu, NHS nchini Uingereza inapanga kupanua matumizi ya kipimo hicho kwa watu milioni moja zaidi katika mwaka 2024 na 2025.

Jaribio hilo ni zuri sana katika kupata saratani ambazo hazionekani wazi kama vile saratani ya kichwa na shingo, utumbo, mapafu, kongosho na koo.

Dk David Crosby, kutoka Utafiti wa Saratani UK, alisema: "Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa kipimo hiki kinaweza kutumika kuwasaidia madaktari kufanya tathmini ya kimatibabu - lakini utafiti zaidi unahitajika, katika jaribio kubwa, ili kuona kama inaweza kuboresha tathmini ya daktari na hatimaye matokeo ya mgonjwa."

Mkurugenzi wa kitaifa wa saratani katika taasisi ya NHS Prof Peter Johnson alisema: "Utafiti huu ni hatua ya kwanza ya kupima njia mpya ya kutambua saratani haraka iwezekanavyo, ikifanywa na NHS - kugundua saratani mapema ni muhimu na kipimo hiki kinaweza kutusaidia kupata saratani zaidi katika hatua ya awali na kusaidia kuokoa maelfu ya maisha."