Je, unaweza kunywa pombe iliyotengenezwa kwenye maabara?

Charles Denby na wenzake wakionja bia zilizotengenezwa na kampuni yake

Chanzo cha picha, BERKELEY YEAST

Maelezo ya picha, Charles Denby na wenzake wakionja bia zilizotengenezwa na kampuni yake.

Charles Denby anasema kazi yake ni kujaribu tu kuboresha ladha ya pombe.

"Tuna nia ya kugeuza ladha zinazohitajika, na kupunguza ladha zisizo bora, na kutengeneza ladha mpya."

Kwa mamilioni na mamilioni ya wapenzi wa pombe, mawazo haya yote yanaonekana kuwa mazuri. Lakini inapojua kile ambacho kampuni ya Bw Denby ya Marekani inafanya, kuna mchanganyiko wa hisia ambayo inazidi kuongezeka.

Yeye ndiye mwanzilishi mwenza na mtendaji mkuu wa Berkeley Yeast, mmoja wa waundaji wakuu wa chachu iliyobadilishwa vinasaba (GM) katika tasnia ya utengenezaji wa pombe.

Chachu hii ni muhimu katika utengenezaji wa pombe, kwani hugeuza sukari inayotolewa na kimea cha shayiri na nafaka nyingine kuwa pombe, huku pia ikiongeza ladha yake.

Berkely Yeast huhariri DNA ya aina za chachu ili kuondoa au kuongeza jeni fulani. Moja ya bidhaa zake ni Tropiki, imebadilishwa ili kutoa ladha ya tunda la passion na mapera.

Bw Denby anasema chachu hii ni ya kutegemewa zaidi kwa watengenezaji wa bia kuliko kuhitaji ugavi wa perechi, na ni bora zaidi kuliko kutumia ladha bandia.

Hamira ni kungo muhimu cha kutengeneza pombe, kugeuza sukari inayotolewa na kimea cha shayiri na nafaka nyingine kuwa pombe.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Hamira ni kungo muhimu cha kutengeneza pombe, kugeuza sukari inayotolewa na kimea cha shayiri na nafaka nyingine kuwa pombe.

"Ni vyema zaidi kuwa na hamira iliyotengenezwa katika maabara, kwani inapunguza utegemezi wa viungo vya ziada kufanya bustani ya mmea wa peach kustawi mwezi baada ya mwezi, mwaka baada ya mwaka. Tafakari maji na mbolea zote ambazo zingeingia kwenye zao hilo."

Berkeley Yeast, iliyoko Oakland, California, hailengi tu kuongeza ladha kwenye kinywaji, inaweza pia kuziondoa. Mojawapo ya aina zake za chachu husaidia kuondoa diacetyl, ladha ambayo huathiri badhi ya pombe.

Wakati huo huo, chachu yake nyingine inasemekana kuwa na uwezo wa kutengeneza bia ya sour ya mtindo wa Ubelgiji katika muda mfupi wa kawaida.

Ikiwa unaishi Marekani, ambayo ina kanuni zilizolegezwa zaidi kuhusu vyakula vilivyobadilishwa vinasaba kuliko nchi nyingi, huenda tayari umeonja pombe zilizotengenezwa kwa bidhaa za Berkeley Yeast, kwa kuwa tayari zinatumiwa na kampuni za ufundi za kutengeneza pombe kote nchini.

Watengenezaji wengine wa pombe ya aina hiyo ni pamoja na Temescal, Alvarado Street na Cellarmaker, kutoka California.

Kiwanda cha pombe cha California cha Lagunitas kinafanya majaribio ya kutumia chachu ya GM

Chanzo cha picha, LAGUNITAS

Maelezo ya picha, Kiwanda cha pombe cha California cha Lagunitas kinafanya majaribio ya kutumia chachu ya GM
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kuhusu uuzaji wa bidhaa zake nje ya nchi, Bw Denby anasema amebanwa na sheria katika nchi nyingi zinazozuia matumizi ya teknolojia ya GM katika sekta ya chakula na vinywaji.

Nchini Uingereza, vyakula vya GMO vinaweza kuidhinishwa na Mamlaka ya kutathmini Ubora wa Viwango vya Chakula, ikiwa vitathibitishwa "kutokuwa na hatari kwa afya, kutowapotosha watumiaji, [na] kutokuwa na thamani ya lishe kuliko zile ambazo ni halisi". Na lazima ziandikwe kwamba zinatoka kwa chanzo cha maabara.

Mtoa huduma mwingine wa chachu za Maabara ni Omega Yeast Labs ya Chicago. Mapema Julai ilitangaza kwamba imegundua jeni maalum ambayo husaidia kusababisha bia ya hazy.

Kwa kutumia teknolojia ya uhariri wa jeni inayoitwa Crispr/Cas9, watafiti waliweza kufuta jeni hili kutoka kwa aina za chachu zenye ukungu. Kwa sababu hiyo, bia zilizochachushwa nazo hazikuwa na weusi tena.

Ian Godwin, profesa wa sayansi ya mazao na mkurugenzi wa Muungano wa Queensland wa Kilimo na Ubunifu wa Chakula, anasema kwamba watengenezaji pombe wa Marekani wanaotumia chachu iliyohaririwa na jeni katika bidhaa zao ni "siri ambayo kila mtu [katika tasnia] anajua".

Hata hivyo anaongeza kuwa ni nadra sana kwa watengenezaji pombe kutukuza ukweli huo kwa kuhofia kugongwa vichwa vya habari hasa ikizingatiwa ukosoaji ambao teknolojia ya GM imepokea hadi sasa.

Wakati huo huo, mtaalam wa kutengeneza chachu Richard Preiss anasema kwamba "nchini Marekani, unaweza kufanya kile unachotaka". Yeye ni mkurugenzi wa maabara katika Escarpment Labs huko Ontario, Canada. Inatoa zaidi ya 300 pombe na chachu, lakini haitumii teknolojia ya kubadilisha jeni.

"Unaweza kuchukua [nchi kama Marekani], kwa mfano, jenomu kutoka kwa basil, na kuichomeka kwenye chachu, na kupata soko haraka na bia yenye ladha."

Huko Lagunitas Brewing, kampuni yenye makao yake makuu California inayomilikiwa na kampuni kubwa ya Uholanzi Heineken, bwana wake Jeremy Marshall anasema kwamba ingawa bado hawana mpango wowote wa kutumia chachu ya GM, wamekuwa wakifanya majaribio.

Birgitte Skadhauge na wenzake hawatumii teknolojia yoyote ya GM

Chanzo cha picha, CARLSBERG

Maelezo ya picha, Birgitte Skadhauge na wenzake hawatumii teknolojia yoyote ya GM

"Kunaweza kuwa na hali ya kusitasita au hofu kutoka kwa wale wanaohusika kuhusu uhusiano wa vyakula vya GMO na makampuni kama Monsanto amabyo imekumbwa na utata wa kukuza vyakula vya GMO, na inaweza kuwa ya kutisha kwa watu wengi," anasema.

"Lakini wanapaswa kutambua kwamba chachu huchujwa, na hakuna kilichobadilishwa vinasaba kinachoingia kwenye bidhaa ya mwisho."

Bado watengenezaji pombe wengine hawajajiingiza kabisha katika utengenezaji wa chachu iliyohaririwa na jeni. Na kwa kutambua kwamba wanywaji wengi wangepinga teknolojia hiyo.

Huko Carlsberg, mojawapo ya makampuni makubwa zaidi ya pombe duniani, kwa muda mrefu imeanzisha sera ya no-GM katika uundaji wa viambato vyake vya kutengeneza pombe - shayiri, chachu zingine - na jinsi inavyotengeneza pombe zake.

Badala yake kampuni hiyo kubwa ya Denmark inafanya kazi ya kuzalisha aina mpya za shayiri ambazo hustahimili joto au ukame vyema. Inafanya hivyo kupitia mchakato wa zamani na imesaidai sana.

Anabainisha kuwa pombe ya kampuni inayopatikana kwa wingi sasa inatumia aina mpya ya shayiri ambayo ni rahisi kukuza, na hudumisha ubichi wake kwa muda mrefu.

Kuhusu kile kitakachojiri kwa bia za kutengezwa kwenye maabara, Bw Marshall anasema ana matumaini kuhusu mustakabali wa bidhaa hiyo.

"Mbinu ambayo watengeneza chachu kama Berkeley wanatakiwa kuzingatia ni kuunda bidhaa ambayo itasalia kuwa safi milele, ladha yake ni sawa kila mahali unapoenda, na na haizeeki," anasema.

"Nadhani watengenezaji wa pombe ya aina hiyo wako mbioni kufikia lengo hilo."