Urusi na Ukraine:Je vifo vya kushangaza vya majenerali hawa wa Urusi vinaashiria nini kuhusu vita hivi?

Chanzo cha picha, КANAMAT BOTASHEV
Kutunguliwa kwa ndege ya kisasa ya Urusi aina ya Su-25 katika eneo la Donbas nchini Ukraine mwezi Mei kulizua maswali mengi kuhusu kifo cha rubani huyo.
Kwa nini mzee wa miaka 63 alikuwa kwenye chumba cha marubani cha ndege ya hali ya juu hivyo? Afisa mstaafu ambaye alikuwa ameacha jeshi la Urusi miaka kumi iliyopita alikuwa akifanya nini kwenye ndege?
Kwa nini jenerali mwingine wa Kirusi amepoteza maisha katika mstari wa mbele? Na ni majenerali wangapi wa Urusi wamekufa?
Kufumbua fumbo hili hutuambia mengi kuhusu hali ya mashine ya vita ya Kremlin na gharama ya kibinadamu ya vita, hata kwa maafisa wa ngazi ya juu zaidi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Meja Jenerali Kanamat Botashev alikuwa rubani wa Kirusi mwenye ujuzi na kuheshimiwa, na licha ya cheo chake, umri mkubwa, na hali ya kustaafu, alirudi hewani siku hiyo ya maafa.
BBC ilizungumza na watu watatu waliokuwa chini yake, ambao walisema "hangeweza kukaa mbali" na "operesheni maalum ya kijeshi", neno ambalo Urusi hutumia kurejelea uvamizi mkubwa ilioanzisha dhidi ya Ukraine mnamo Februari 24.
"Alikuwa rubani wa P," mmoja wa wafanyakazi wenzake wa zamani wa Botashev alisema. "Kuna watu wachache duniani wanaozingatia anga kama yeye."
"Siku zote nitajivunia kutumikia chini yako," aliongeza mwingine. Lakini ukweli kwamba Botashev alishiriki katika mapigano huko Ukraine haukuongeza, na sio tu kwa sababu ya umri wake. Afisa mkuu hakuwa hata mshiriki wa Jeshi la Urusi: alikuwa amefukuzwa kazi miaka kumi nyuma.
Majenerali waliouawa

Bootshev ni mmoja wa majenerali kadhaa wa Urusi waliokufa katika mzozo huo, na ingawa idadi kamili inabishaniwa vikali, kupoteza hata jenerali mmoja sio kawaida sana katika vita vya kisasa.
Kwa kulinganisha, wakati Meja Jenerali wa Marekani Harold Greene aliuawa na mwanajeshi wa Afghanistan katika shambulio la 2014, kifo chake kilikuwa mara ya kwanza katika zaidi ya miaka 40 kwamba jenerali wa Marekani aliuawa katika mapigano.
Ukraine imedai kuwa majenerali 11 wa Urusi wameuawa katika mzozo huo kufikia sasa. Licha ya hayo, baadhi ya ripoti zimeonekana kuwa mbaya: watatu kati ya wale ambao wametangazwa kuwa wamekufa baadaye walionekana kwenye video iliyowekwa mtandaoni, na kukanusha habari za vifo vyao.
Kati ya maafisa wanane waandamizi waliosalia ambao Kyiv inadai kuwaua, hadi sasa ni wanne tu kati yao wamethibitishwa kufariki, huku taarifa za wengine wanne bado hazijathibitishwa, lakini wala hazijakanushwa.
2.Andrey Sukhovetsky
Kifo cha Meja Jenerali Andrey Sukhovetsky kilitangazwa mnamo Machi 1.
Afisa wa kijeshi aliyestaafu alitweet kwamba Sukhovetsky alipigwa risasi na mshambuliaji wa Kiukreni katika eneo la Hostomel, si mbali na mji mkuu wa Kyiv.
3.Vladimir Frolov
Jeshi la Ukraine lilitangaza kuwa Meja Jenerali Vladimir Frolov amekufa mnamo Aprili 16, ambayo ilithibitishwa na ripoti zilizotangaza mazishi yake katika jiji la Urusi la Saint Petersburg. Mazingira ya kifo chake hayajawekwa wazi.
4.Roman Kutuzov

Hivi majuzi, mnamo Juni 5, mwandishi wa habari wa vyombo vya habari vya serikali ya Urusi alichapisha kwenye huduma ya ujumbe wa Telegraph kwamba Meja Jenerali Roman Kutuzov aliuawa wakati akiongoza shambulio dhidi ya vikosi vya Ukraine katika mkoa wa Donbas mashariki mwa Ukraine.
Kwa nini hatujui ni majenerali wangapi wa Urusi wamekufa?
Jibu rahisi ni kwamba Waukraine hawajui kwa hakika na Warusi hawasemi.
Kwa Urusi, vifo vya kijeshi vinachukuliwa kuwa siri ya serikali hata wakati wa amani.
Kwa kuongezea, Moscow haijaweka wazi idadi yake rasmi ya waathiriwa wa Ukraine tangu Machi 25, iliposema kuwa wanajeshi 1,351 waliuawa katika mwezi wa kwanza wa vita.
Katika mradi unaoendelea wa utafiti, kwa kutumia vyanzo vya wazi na kuzungumza na familia za wanajeshi wa Urusi, BBC imeandaa orodha ya zaidi ya majeruhi 3,500, pamoja na majina na vyeo vyao, ikionesha kwamba huenda idadi halisi ni kubwa zaidi.
Utafiti wetu pia unaonesha kuwa askari mmoja kati ya watano wa Urusi waliouawa alikuwa afisa wa cheo cha kati au mwandamizi.
Haya yote yanasema nini?

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Uwiano wa maafisa wa ngazi za juu waliouawa ni ya kushangaza, lakini Jeshi la Kirusi lina idadi kubwa ya maafisa wa juu: karibu 1,300 kwa jumla.
Ingawa wengi wao hawangetarajiwa kuishia mstari wa mbele, idadi kubwa ya majenerali wamejikuta hapo.
Hii inaweza kuwa kwa sababu majenerali wanatarajiwa kufanya kazi na kufanya maamuzi ambayo yanalingana na wasaidizi katika taasisi za kijeshi za nchi zingine, ambayo huwaleta karibu na mbele kuliko inavyotarajiwa.
Maafisa wa nchi za Magharibi pia wamependekeza kwamba ari ya chini miongoni mwa wanajeshi wa Urusi imewalazimu jeshi kuzindua vifaa vyake vizito.
Pia, uhaba wa vifaa vya mawasiliano unaweza kuongeza hatari kwa maafisa hao, ikidaiwa kuwalazimisha kutumia simu za kizamani wanapokuwa karibu na mapigano, na hivyo kuhatarisha usalama wao.
Hatimaye, vyombo vya habari vya Marekani vinadai kwamba maafisa wa kijasusi wa kijeshi wa Ukraine wanalenga kwa makusudi uongozi wa Urusi kwa wadunguaji na mizinga, na kwamba Marekani imetoa taarifa kwa Ukraine kuhusu waliko.












