Manupuli: Je, ni kweli miti hii huuma na kung'ata watu na mifugo?

a
Muda wa kusoma: Dakika 3

Jamii za kiasili katika kijiji cha Valagajji, wilaya ya Parvathipuram-Manyam, wamelalamika kwa maafisa wa misitu kwamba kuna miti, vigogo na vijiti vya aina fulani ya mti katika eneo la Seetampet agency ambayo huwaauma na kuwang'ata

Kutokana na hili, maafisa wa misitu wamekuwa wakifuatilia kwa karibu kinachotokea katika kijiji cha Valagajji kwa siku chache zilizopita.

Hata hivyo, wataalamu wanasema kuwa yote haya hayapaswi kuaminiwa kwanza, kwani wasiwasi wa wanakijiji, unatokana na imani zisizo za kisayansi. Lakini wananchi wenyewe wana ushuhuda.

Miti hiyo katika kijiji cha Valagajji Ikoje?

Timu ya BBC, pamoja na maafisa wa misitu, walitembelea kijiji cha Valagajji.

Tulipoingia kijijini, tuliona mti mkubwa wa mkwaju na mti wa mnazi. Pamoja na ana hii, tuliona miti mingi ya misaji, ndizi, mlozi, na saffron... na miti mingine mingi. Ikilinganishwa na miti katika maeneo mengine, hii haikuwa na kitu cha pekee. Ilikuwa ya kawaida.

Kijiji hiki, ambacho kina takriban familia 60, kina idadi ya watu 210. Wote wanategemea ufugaji na kilimo kwa maisha yao. Kuna vibanda na uzio iliyotengenezwa kwa miti ama fito kwenyebaadhi ya nyumba. Watu wawili au watatu walionekana wakienda kwenye bustani wakiwa na mapanga mabegani mwao.

Jamii hiyo inasema kuwa fito na miti katika kijiji hicho huwauma watu na mifugo, pamoja na kuwazingira wapita njia. Wameiita miti hiyo Manupuli.

Wanakijiji wanasema kuwa mti huu una makucha kama ya tiger, ndiyo maana unaitwa Manu-Puli.

ఆంధ్రప్రదేశ్, విశాఖపట్నం, ఏజెన్సీ ఏరియా, గిరిజనులు

"Miaka kumi iliyopita, nilipokwenda kwenye kukata miti, fito moja ilininasa mguuni mwangu, na ilibidi mpaka nishonwe nyuzi kutokana na jeraha," Gatikamma, mwenye umri wa miaka 62, aliiambia BBC.

"Nilipokuwa nikipiga kelele, mke wangu aliona na kukata na kisu, na kimti hicho kiliniacha. Hivyo ndivyo nilivyookoka," alisema Gatikamma.

"Nilienda kumwagilia ng'ombe karibu na mti. Kisha mti wa misaji ulikama mkia wa ng'ombe wetu. Kisha tukaukata kwa kisu na kuondoka," alisema Mounika kutoka kijiji cha Valagajji kwa BBC.

ఆంధ్రప్రదేశ్, విశాఖపట్నం, ఏజెన్సీ ఏరియా, గిరిజనులు

Dk. J. Prakasarao, mtaalamu wa mimea katika Idara ya Botania ya AU, aliiambia BBC kuumwa na kung'atwa na miti hakutokei.

"Kawaida, wakati mifugo inafungwa karibu na nyumba au kupelekwa msituni... utaona kuwa mikia ya mifugo ni mikavu. Mikia inaweza kujifunga kwenye vijiti, Mifugo, isiyoweza kujinasua vizuri, hujaribu kujifunga zaidi. Wanajifunga kwa nguvu. Katika matukio kama haya, watu hufikiri kuwa kijiti au mti umewakamata," alieleza Dk. Prakash Rao.

Dk. Prakash Rao alisema kuwa binadamu pia wakati mwingine wanaweza kupata hali kama hiyo wakati nguo zao zinapogusa miti.

'Miti inaweza kuwa hatari" - Wataalamu

ఆంధ్రప్రదేశ్, విశాఖపట్నం, ఏజెన్సీ ఏరియా, గిరిజనులు

Maafisa wa misitu wanasema kuwa hata kama hakuna Wanyama ama... miti wakati mwingine inaweza kuwa hatari.

"Kuna uwezekano wa ajali wakati kuna nyaya za umeme zinaning'inia karibu na miti. Ikiwa tunategemea mti wowote wakati wa kupanda au kushuka milima... ikiwa ni dhaifu, tutateleza. Kuna uwezekano wa miti iliyokufa kudondoka na kutuangukia sisi. Pia kuna uwezekano wa miti kuanguka wakati wa radi na umeme. Lakini, miti haiwakamati au kuwaumiza watu au wanyama," alisema Neelaveni.

Haina mvuto kwa binadamu au wanyama"

ఆంధ్రప్రదేశ్, విశాఖపట్నం, ఏజెన్సీ ఏరియా, గిరిజనులు
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Dk. Prakash Rao alisema kuwa miti hata matawi, fimbo, fimbo na vigogo vyake havina sifa ya kuwavuta, kuwang'ata watu na mifugo.

"Kuna uwezekano kwamba vidole vyetu au ngozi inaweza kuingia kwenye upenyo au uwazi wakati wa kukata miti na kukwama kwa nguvu, na kusababisha majeraha. Hii kawaida huitwa kuumwa. Ikiwa hiyo itatokea, inaweza kutokea... Rao namaanisha binadamu anaifuata miti ambayo inamshika wakati wa shughuli zake za kawaida, lakini miti yenyewe haina sita ya kukufuata na kung'ata na kuumiza watu. Hiyo linaonekana tu kwenye filamu," alisema Dk. Prakash Rao.

Ingawa jamii za kiasili katika kijiji cha Valagajji wanaamini kuwa miti, na magogo yake yanaweza kuumiza, kuwakamata watu na mifugo, wataalamu na maafisa wa misitu wanasisitiza kuwa haya ni matokeo ya imani za asili na si matukio halisi. Uelewa wa kisayansi unahitajika ili kuelewa na kuelezea matukio haya, na elimu zaidi inapaswa kutolewa kwa jamii hizi ili kuondoa hofu zisizo na msingi.