"Tulikua tunashiriki mapenzi hotelini bila kujua tulirekodiwa na kuonwa na maelfu"

A designed image showing a generic hotel room, black wheelie suitcase, a standard lamp, a double bed with a white bedspread and blue, gold and black and white checked pillow, and the words REC with a red recording dot emblazoned over the top.
    • Author, Wanqing Zhang
    • Nafasi, BBC Global China Unit and Eye Investigations
  • Muda wa kusoma: Dakika 9

Usiku mmoja mwaka wa 2023, Eric alikuwa akiangalia mitandao ya kijami kwenye simu yake. Siku hiyo alikuw aanafuatilia ukurasa wa mtandao unaoonyesha picha/video za ngono (Pornography) kama alivyokuwa akifanya mara kwa mara, lakini alikutwa na mshangao mkubwa mara tu alivyokutana na video moja iliyokuwa kama anaifahamu.

Aligundua kwamba watu aliyokuwa akiwatazama – wakiingia chumbani, wakijipumzisha na kisha kushiriki ngono kumbe ilikuwa yeye na mpenzi wake. Wiki tatu kabla ya tukio hilo, wawili hao walikuwa kwenye mapumziko katika hoteli moja mjini Shenzhen kusini mwa China, bila kujua kwamba walikuwa wanachunguzwa na kurekodiwa.

Vitendo vyao vya kushiriki ngono vilirekodiwa na kamera za siri ambazo zilifichwa kwenye chumba walicholala. Na baadaye picha hizo za video zilichapishwa kwenye mitandao na kutazamwa na maelfu ya watu kwenye ukurasa wa mtandao wa kuchapisha video za ngono ambao yeye mwenyewe Eric alikuwa anapenda kuutazama.

Erica (ambalo si jina lake halisia) hakuwa tena mteja wa mtandao huo wa picha za ngono zilizorekodiwa kisiri nchini China, bali alikuwa muathiriwa.

TAHADHARI: Taarifa hii inalugha ambayo huenda ikakukera.

Biashara haramu ya picha za ngono zilizorekodiwa kwa siri almaarufu SPY CAM imekuwepo nchini China kwa zaidi ya muongo mmoja sasa, japo kurekodi na kutayarisha picha hizo za video kumeharamishwa na ni kinyume na sheria nchini humo.

Lakini katika miaka ya hapo nyuma, suala hili limekuwa kama jambo la kawaida kujadiliwa miongoni mwa wengi katika jamii hasa kwenye mitandao ya kijami – hasa miongoni mwa wanawake - wanaojipa mawaidha ya jinsi ya kutambua kamera za siri zilizofichwa chumbani kwa kutumia kifutio cha kalamu ya mate au penseli. Baadhi wamejitolea kuandamana na wenzao na kukesha kwenye vyumba vya mahoteli ili kuzuia kurekodiwa.

Mwezi Aprili mwaka jana, kanuni mpya za serikali zilizotolewa zilijaribu kuangamiza tatizo hilo na kulidhibiti – sheria hizo ziliwataka wamiliki wa hoteli kukagua vyumba vya kulała kwa ajili ya kupata na kuondoa kamera za siri.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Lakini tishio hilo la kurekodiwa bila ya kujuwa katika chumba cha kulała kwenye hoteli halijamalizwa kabisa. Idhaa ya dunia ya BBC (BBC World Service) imepata maelfu ya picha za video zilizorekodiwa na kameza za siri kwenye vyumba vya kulała hotelini ambazo zimeuzwa kwa mitandao ya kuonyesha video za ngono.

Video hizi zinatangazwa kwa mtandao wa kijami wa Telegram. Kwa muda wa zaidi ya miezi 8, niligundua tovut sita tofauti ambazo zimefanyiwa matangazo kwa mtandao wa telegram. Miongoni mwa mitandao hii, haya yamedai kuwa na kamera katika vyumba zaidi ya 180 vya Hoteli tofauti a,bazo hazirekodi tu, bali kuchapisha mubashara picha hizo za video kwenye mitandao. Aidha imagunduliwa kwamba nusu ya idadi ya kamera hizo zinafanya kazi kwa saa 24 kwa siku.

Nilifuatilia mmoja ya tofuti nilizozitaja , mara kwa mara kwa muda wa miezi saba na kupata picha zilzizorekodiwa na kamrea 54 tofauti.

Hii ina maanisha kwamba maelfu ya wateja na wageni wanaofika hotelini huenda walirekodiwa katika muda huo, ambapo BBC inakadiria kwamba kutokana na idadi ya wateja hapo ni wengi wlaioathirika. Wengi huenda hawafahamu wala hawajui kuwa wlairekodiwa na kamera hiz za siri.

Eric ambaye ni makzi wa Hong Kong, alianza kutazama picha za ngono zilizorekodiwa kisiri akiwa kijana mdogo. Anasema alivutiwa na jinsi mahusiano yaliyorekodiwa yalivyokuwa kati ya watu ambao hakuwa wanaigiza walichokuwa wakifanya.

'Kilichonivutia kilukuwa kwamba waliokuwa katika video hizo, hakuwa na ufahamu kwamba wanarekodiwa,' alisema Eric ambaye kwa sasa ana muri wa miaka 30. 'Nadhani picha ngono za kawiada zinaonekana sana kuwa watu wenye kushriki huwa wanaigiza, na hazina uhalisia wowote.'

Lakini alishuhudia moja kwa moja wanachohisi wengi ambao wako uoande wa pili wa video hizo – wenye kurekodiwa bila kutoa idhini au kufahamu- alijipata karekodiwa pamoja na mpezi wake 'Emily' – na tangu hapo, hahisi tena kwamba video kama hizo za ngono hazifurahisi nafsi yake tena.

Alipomueleza mpenzi wake kuhusu taarifa hiyo,kwamba hoteli walipolala walirekodiwa kisiri, na picha hizo kuhaririwa na kuchapishwa mitandaoni ambapo watazamaji walipata fursa ya kuwatazama wakiwa na mahusiano yao kw asaa nzima, alidhani kwamba ni mzaha. Ila alipotazama picha hizo za video kwwneye mtandao wa telegram, alishtuka sana.

Emily alishtuka kabisa kuona video hiyo na kuhofia kwamba huenda ikatzamwa na wafanyakazi wenzake au hata jamaa zake nyumbani. Baada ya hapo, wawili hao hawakuzungumza kw awiki kadhaa.

Kwa hivyo sekta hii ya biashara – ambayo inawadhulumu wapenzi wasiokuw ana habari yoyote kuhusu kurekodiwa kwa siri – inafanya vipi kazi zake na ni nani anayesimamia biashara hiyo?

Nilijifanya kama mteja na kulipia kupata huduma ya tovuti inayotangaza video za ngono mubashara. Kila mwezi nilikuwa nalipa dola 65, sawia na Pauni 47 ama Yuan 450.

Nilipoiingai kwenye mtandao huo, nilikuwa na uwezo wa kuchagua katika chaneli tano ambazo zilikuwa zinatangaza mubashara pica za ngono, kila mmoja ikioneysha picha kutoka kwa kamera za siri zilzizowekwa kwatika vyumba vya kulała kwenye hoteli kadhaa. Picha hizo zilianza kurekodiwa punde tu, mtu anapoingia ndani ya chumba kwa kutumia kadi ya kufungua mlango na kemera zinaanza kufanya kazi .

Two different hotel rooms are visible on the livestream the BBC subscribed to - the view from the spy-cam clearly shows the double beds
Maelezo ya picha, PICHA: Kamera za siri ya SPYCAM zinazotangaza mubashara zinaonyesha vyema palipo vitanda katika vyumba vya hoteli.

Katika mtandao wa Telegram – ambao umepigwa marufuku China, ila bado unatumika sana kwa shughuli ambazo si halali – AKA ilitangaza matangazo ya mubashara ya video za ngono. Chaneli moja ya Telegram ilikuwa na wateja zaidi ya 10,000 katika muda ambao tulifanya uchunguzi wetu.

Vile vile kuan hifadhi ya vodeo za ngono kwenye mtandao huo huo wa Telegramkwa wale wanaotaka kutazama baadaye kwa malipo. Nilikuw anaweza kuona kwamba kuna vido zaidi ya 6,000 ambazo zimehofadhiw apale ambazo huenda zilirekdoiwa 2017.

Wateja wa AKA wanaweza kutoa maoni yao kwenye chalei hiyo ya Telegram, wanapoendelea kutazama video hizo zawageni wanaoigia katika vyumba vya hoteli – wakikagua jinsi miili yao ilivyo, wakiwasema kuhusu mazungumzo yao na hata kufanya Tathmini ya mbinu zao za kujamiaana.

Wanashereheka wakati ambapo wapenzi ama wanadoa wanapoanza kushirki ngono – na hulalamika ikiwa wapenzi hao watazima taa, wakikasirika ni kwa nini wanafanya mambo yao kwenye giza. Wanawake hupewa jina la 'hawara' na mengine mengi ya kuwadhalilisha.

Tumefanikiwa kupata moja ya kamera hizo za siri katiak chumba hiki kilichowekwa katika hoteli ya Zhengzhou iliyopo katikati mwa hina, hili iliifanikishwa kwa kuweka pamoja mambo muhimu , tiloyoyapata kutoka kwa watejwa wa mitandao hiyo, mtandao w akijamii na utafiti wetu.

Watafiti waliokuwa katika Eneo hilo, waliweza kuingia katika chumba hicho cha hoteli, na kuipata kemra – lensi yake ilikuwa imeangalizwa kwa kitanda na ilikuwa imefichwa kwenye mfumo wakuleta hewa safi chumbani na waya zake zilikuwa zimeunganshwa na mfumo wa stima wa ndani ya chumba.

Maelezo ya video, Tazama: Wakati BBC ilipobaini kamera ya siri iliyofichwa kwenye moja ya chumba cha hoteli

Kifaa maluum cha kutambua kamera iliyofichwa, ambacho kinauzwa mitandaoni halikuwaarifu wateja kwamba wanarekodiwa kisiri.

Timu yetu iliiondoa kemra hiyo ya siri na taatrifa hizo zikasambaa haraka kwa mtandao wa Telegram.

'Zhonghua {jina la kemera} limeondolewa!' Mteja mmoja waliandika kwenye mtandao wa telegram.

'Ni masikitiko kwamba chumba hicho kina sauti na picha nzuri kabisa!' AKA aliandika kwenye CHATI iliyokuwa inaendelea.

Ila malalmiko yaliyosheheni yaligeuka kuwa sherehe na furaha katiak saa chache tu. AKA aliandika kwenye chati hiyo kwamba kamera nyingine ilikuwa imeanza kufanya kazi katika hoteli nyingine.

''Hii ndio kasi …ya {mtandao wetu wa matangazo mubashara}…' AKA aliwaambia wateja wake. ' Ni mambo mazuri, ya kuridhisha, sio?'

Katiak muda wa miezi 18 ambapo tulitekeekza uchunguzi wetu tulikgunduwa makumi ya mawakala /mawakala wengine kama AKA.

Mawasiliano kati yao na na wateja wao yalionyesha wazi kwamba wanafanyia kazi wengine walio juu yao kifedha ambao wanafahamika kama 'wamiliki wa kamera.''

Watu hawa, mawakala wao kwa mawasiliano yao, inaahsiria kwamba wanafanya Mpango wa kamera za siri kuwekwa kwenye vyumba vya hoteli, na wanasimamia matangazo ya mubashara kwenye mitandao na tovuti zinazotoa huduma hiyo.

Wakati ambapo tulifanya mawasiliano ya moja kwa moja na AKAK, alitutumia kimakosa ujumbe kutoka kwa mtu ambaye alitaja kama 'mmiliki wa kamera' , ambaye ana jina la anwani la BROTHER CHUN.

AKA alifuta ujumbe huo mara moja na kukataa kuendelea kuzungumzia suala hilo, lakini tulifanikiwa kumtumia ujumbe BROTHER CHUN wa moja kwa moja.

Na japo tulikuwa na ushahidi kuwa alikuwa ana miliki tovuti ya kutangaza ngono mubashara ambayo alimpa AKA kusimamia, BROTHER CHUM alidai kwamba yeye ni wakala tu, ila alionekana kuw ana ufahamu wa jisni mtandao huo wa biashara unavypanuka kupita kiwango chake.

Kilicho wazi ni kwamba kuna idadi kubwa za pesa ambazo zinatengenezwa kutokana na biashara hiyo. Kulinganna ada za kuwa mteja kwenye mtandao huo, na ada ya kutazama ila mwezi, BBC inakadiria kwamba AKA peke yake alipata kipato cha 163,200 Yuan ($22,000, £16,300) tangu mwezi Aprili mwaka jana. Kipato cha wastani nchini China mwaka jana kilikuwa 43,377 Yuan ($6,200, £4,600) kulingana na takwimu za Idara ya takwimu ya China Bureau of Statistics.

Eric and Emily shot from behind - both wearing light coloured bucket-style hats and white t-shirts. They are looking over the water at a city skyline.
Maelezo ya picha, Eric na emily hawatembei hadharani bila ya kuvalia kofia sasa, kwa kuwa wanahofia huenda mtu akawatambua.

Kuna sheria kali kuhusu biashara ya kuuza kamera za siri na matumizi yake nchini China, lakini tuligunduwa kwamba ni rahisi sana kwa mja kuzinunuwa katika soko kubwa la bidhaa za elektoniki nchini humo – Huaqiangbei.

Takwimu kamili kuhusu ni watu wnagapi ambao wamefikishw amahakamani kwa kosa la kusambaza picha za ngono zilizorekodiwa kisiri ni ngumu kupata.

Mamlaka nchini China zimeweka wazi taarifa kidogo sana zinazohusianana aina hizi za kesi ambazo zinasikizw amahakamani. Na kesi ambazo zipo wazi zilikuwa kutoka maeneo mbali mbali kati ya Mikoa ya Jilin kaskazini mwa nchi hiyo na ule wa Guangdong ulipo kusini mwa China.

Mhudumu wa shiirika la kijamii Blue Li, kutoka Hong Kong linalofahamika kama RainLily – ambalo linawasaidia waathiriwa waliorekodiwa kisiri kuondoa video zao kwenye mitandao – anasema kwamba kuna haja kubwa kutoka kwa wateja kwa huduma zao kuondowa video hizo mitandaoni , lakini kazi hiyo inaonekana kuwa ngumu.

Kampuni ya Telegram haijawahi kujibu wanapotumiwa ujumbe na RainLily kuwataka kuondoa video hizo mitandaoni. Hali ambayo anasema inawalazimu kuwasiliana na mawakala ambao wanasimamia chaneli hizo zenye wateja na kuwaomba kuondoa video hizo kwa kuwapa 'kitu kidogo'

'Tunaamini kwamba kwamba makampuni ya Teknolojia yana paswa kuwajibishwa kuchukuwa jukumu la kuliangazia suala hili na changamoto zinazojitokeza.

Kwa sababu makapuni haya hayawezi kuondolewa makosa wala kutojumuishwa kwenye wakulaumiwa. Ni lazima waangazie tatizo hili kwa kuwa sera zao zinabuni mfumo wa jisni utayarishai wa matangazo ya video za ngono yanavyosambazwa,' Li amesema.

BBC imeiambia Telegram kupitia huduma yake ya REPORT FUNCTION , kwamba AKA na BROTHER CHUN – na makundi ambayo wanayasimamia – walikuwa wanasambaza picha za ngono kwenye chaneli za telegram, ila kampuni hiyo haikujibu masawli yetu wala kuchukuwa hatua yeyeote.

Tazama hapa
Maelezo ya video, Kamera za siri zilivyotumika kurekodi ngono

Tulipojaribu tena kuwasiliana nao baada ya siku kumi, na kuwapa matkeo ya uchunguzi wetu, telegram ilitueleza kuwa: 'Kusambaza picha za ngono ambazo wahusika hawajaridhia na kuidhinisha ni kinyume na sheria na kanuni za Telegram, na wafanyakazi wetu hudhibiti jinsi picha na video zinavyosambazwa kwenye mtandao wetu…Aidha sisi hupokea taarifa za kuripoti maudhui ya kuogfya, kuudhi ama yasiyonsahihi kwa ajili ya kuondoa mamilioni ya picha na video ambazo ni chafu na zenye kuwa na athari mbaya katika jamii, kila siku.'

Tuliwasilisha matokeo ya uchunguzi wetu kwa BROTHER CHUN na AKA na kuonyesha jinsi walivyokuwa wanafaidika na biashara haramu inayokiuka haki za kimsingi za watu wanaorekidiwa katika hoteli wanazolala.

Hawakujibu, ila saa chache baada ya hapo akaunti za Telegrama ambazo walikuwa wanaziendesha na kusimamia zilionekana kufutwa. Hata hivyo, tovuti ambayo AKA alinipa fursa ya kuingia na kutazama kw amalipo, bado iliendelea kutoa matangazo mubashara ya picha za wageni wakiwa hotelini.

Eric na emily wameathirika pakubw ana kilichowakuta. Wao huvalia kofia hadharani kila wanapotoka nje ili kuzuia kutambuliwa na hawakai te akatika hoteli wanaposafiri.

Eric aliwacha kutumia huduma ya mtandao wa kuonyesha picha za ngono alizokuwa mteja wake katika mtandao wa Telegram. Ila anakiri kwmaba mara kwa mara hutazama picha hizo za ngono {PONORGAPHY} mara kwa mara akihofia huenda akizipata picha za video ambapio wahusika wakuu ni yeye na mpenzi wake emily.

Imetafsiriwa na kuhaririwa na Laillah Mohammed , taarifa zaidi na Cate Brown, Bridget Wing and Mengyu Dong