Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 14.06.2024

Chanzo cha picha, Getty Images
Newcastle na Bayern Munich zilikuwa klabu za kwanza kuwasiliana na Crystal Palace zikitaka kumsajili winga Mfaransa Michael Olise, 22. (Athletic - usajili unahitajika)
Chelsea nao walifuata mkondo kuwasiliana na Palace kuhusu Olise, na kuwafikia siku ya Alhamisi. (Mirror)
Mchezaji wa kimataifa wa Uingereza aliye na umri wa chini ya miaka 21 anayeichezea Chelsea Noni Madueke, 22, pia yuko kwenye orodha ya walioteuliwa na Newcastle huku klabu hiyo ikiwa na mpango wa kumnunua winga mpya wakati dirisha la uhamisho wa wachezaji litakapofunguliwa. (i Sport)

Chanzo cha picha, Getty Images
Klabu ya Al Nassr inayoshiriki ligi ya Saudi Pro, inataka kumfanya beki wa Liverpool na timu ya taifa ya Uholanzi Virgil van Dijk kuwa beki anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani. (Marca)
Manchester United inamfuatilia kwa karibu beki wa Bayern Munich na Uholanzi Matthijs de Ligt, 24. (Sky Sports Germany)
Manchester United pia ina Mfaransa Jean-Clair Todibo mwenye umri wa miaka 24 wa Nice, klabu nyingine inayomiliki Ineos, kama chaguo wanapotaka kuajiri beki. (Mail)
Mshambuliaji wa Bologna Mholanzi Joshua Zirkzee, 23, pia yuko kwenye rada za Manchester United msimu huu wa joto, lakini wanaweza kukabiliwa na ushindani kutoka kwa AC Milan na Juventus. (Telegraph - usajili unahitajika)

Chanzo cha picha, Getty Images
Liverpool na Manchester United zote zinamsaka beki wa kati wa Lille Mfaransa Leny Yoro, 18, lakini Real Madrid pia wanamtaka. (Athletic - michango inahitajika)
Klabu za Tottenham, Aston Villa na West Ham zinavutiwa na mshambuliaji wa Roma na England Tammy Abraham, 26. (Telegraph - usajili unahitajika)
Aston Villa wanahitaji pauni milioni 40 kumnunua mshambuliaji Jhon Duran, huku Chelsea wakiwa kwenye mazungumzo ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. Raia huyo wa Colombia amecheza mechi tatu pekee za Ligi ya Primea tangu ajiunge nao Januari 2023. (Times - usajili unahitajika)
Mkufunzi mpya wa Fenerbahce Jose Mourinho anataka kumsajili kiungo wa kati wa Denmark Pierre-Emile Hojbjerg, 28, kutoka Tottenham. (Takvim - kwa Kituruki, usajili unahitajika)

Chanzo cha picha, Getty Images
West Ham na Leicester City wamekutana na wawakilishi wa mshambuliaji wa Juventus Muargentina Matias Soule, 21, mjini London. (Tuttosport - kwa Kiitaliano)
Arsenal wanakabiliwa na kipingamizi katika harakati zao za kumnunua mshambuliaji wa Sporting Lisbon na Uswidi Viktor Gyokeres, 26, huku hesabu ya timu hiyo ya Ureno ikiwa juu kuliko ile ambayo The Gunners wako tayari kulipa. (Sun)
Brentford haitamuuza mshambuliaji wa Uingereza Ivan Toney, 28, kwa chini ya pauni milioni 60, ingawa hapo awali walikadiria thamani yake kuwa pauni milioni 80. (Sportsport)
Mkufunzi wa zamani wa Brighton Roberto de Zerbi anatazamiwa kukubali kandarasi ya miaka mitatu kuwa kocha wa Marseille. Brighton angepokea ada ya euro milioni sita
Klabu za Ligi Kuu ya England zinamtaka beki wa Lens na Austria Kevin Danso, 25, ambaye ameungwa mkono na mchezaji wa zamani Rio Ferdinand kuhamia Manchester United. (i Sport)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi












