Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Sababu tano zinazoufanya uchumi wa China kuwa taabani
Uchumi wa Uchina unaporomoka chini taratibu huku ikiondoa mikakato yote ya kukabiliana na na Covid na kudhoofika kwa kudhoofika kwa uchumi wa dunia. Takwimu rasmi za ukuaji wa wa uchumi za robo ya mwaka za kati ya mwezi Julai na Septemba zinatarajiwa kutolewa hivi karibuni - na kama uchumi wa nchi hii ya pili kwa ukubwa kiuchumi duniani utashuka hiyo inaongeza fursa ya taifa hilo kuingia katika mdororo wa uchumi.
Lengo la Beijing - la ukuaji wa uchumi wa kiwango cha 5.5% - kwa sasa haliwezi kufikiwa ingawa maafisa wanaonyesha kupunguza haja ya kufikia lengo hilo. China nurura iporomoke kiuchumi katika robo ya mwaka ya kati ya mwezi Aprili hadi Juni.
Mwaka huu, baadhi ya wachumi hawatarajii ukuaji wowote wa uchumi katika nchi hiyo. Huenda Uchina isikabiliane na mfumuko mkubwa wa bei kama Marekani na uingereza, lakini ina matatizo mengine - viwanda vya nchi hiyo vya dunia vimepata wateja wachache ghafla kwa ajili ya bidhaa zake za ndani na za kimataifa.
Wasiwasi wa kibiadhara baina ya Uchina na chumi kuu kama vile Marekani pia vimeathiri ukuaji wa uchumi.
Na sarafu ya taifa hilo - yuan iko katika mwaka mwaka mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika miongo kwani imeporomoka dhidi ya sarafu ya Marekani -dola. Sarafu dhaifu inawafukuza wawekezaji, na kuchochea wasi wasi katika masoko ya kifedha.
Pia inasababisha ugumu kwa benki kuu kuongeza pesa katika shuhuli za uchumi.
Yote haya yanatokea katika wakati ambapo Rais Xi Jinping akikabiliwa na wakato mgumu - anatarajiwa kuwania muhula wa tatu katika kwa kuidhinishwa na mkutano mkuu wa chama cha kikomunisti (CPC) kinachotarajiwa kuanza tarehe 16 Oktoba.
je ni kosa gani hasa lililofanyika?
1. Mkakati wa kuzuia Covid unasababisha hali kuwa mbaya zaidi
Milipuko ya Covid katika miji kadhaa ikiwemo miji ambayo ni vitovu vya uzalishaji wa viwanda kama Shenzhen na Tianjin, imekuwa ikiathiri vibaya shughuli za kiuchumi kote viwandani.
Watu pia wanatumia pesa katika matumizi kama vile chakula na vinywaji na hivyo kuziweka huduma nyingine chini ya shinikizo kubwa.
Upande wa uzalishaji, shughuli za viwanda zinaonekana kuongezeka tena kufikia mwezi Septemba, kulingana na shirika la taifa la takwimu. Kurejea kwa shughuli za viwanda kunaweza kuwa ni kwasababu serikali inagharimia zaidi miundo mbinu.
Lakini inakuja baada ya miezi miwili ya kudorora kwa uzalishaji, hususan tangu utafiti wa kibinafsi ulipoonyesha kuwa shughuli za viwanda zilipungua katika mwezi Sepemba , huku mahitaji ya bidhaa za viwanda yakipita uzalishaji, bidhaa zinazoagizwa na ajira.
Uagiza wa bidhaa kutoka Uchina katika nchi kama vile Marekani ulipungua pia kwasbabu ya viwango vya juu vya riba, mfumuko wa bei na vita nchini Ukraine.
Wataalmu wanaafiki kuwa Beijinginaweza kuongeza uchocheaji zaidi wa uchumi, lakini kuna sababu ndogo katika kufanya hilo hadi itapoachana na sheria ya kudhibiti covid.
"Hakuna sababu kubwa ya kuongeza pesa katika uchumi wetu kama biashara haiwezi kupanuka au watu hawawezi kutumia pesa," alisema Louis Kuijs, mkuu wa Asia economist katika taasisi ya S&P Global Ratings.
2. Beijing haifanyi juhusi za kutosha
Beijing imeingilia kati -Mwezi Agosti ilitangaza mpango wa yuan trilioni 1 ($203bn; £180bn) wa kuinua biashara ndogo ndogo, miundo mbinu na ujenzi wa makazi. Lakini maafisa wanaweza kufanya juhudi zaidi kuchochea matumizi ili kufikia viwango vya ukuaji na kubuni ajira.
ii ni pamoja na kuwekeza zaidi katika miundo mbinu, kulegeza masharti ya kukopa kwa wanunuzi wa nyumba na serikali za mitaa, na kuondoa kodi za nyumba kwa muda.
3. Soko la mali la China liko katika mzozo
Shughuli dhaifu za ujenzi wa makazi na mawazo hasi katika sekta ya nyumba bila shaka vimezorotesha ukuaji wa uchumi.
Hii imeathiri uchumi vibaya kwasababu makazi na sekta nyingine ambazo zinachangia ukuaji huchukua nafasi ya tatu ya pato la ndani ya nchi (GDP).
"Wakati imani ni dhaifu katika soko la nyumba, inawafanya watu wahisi kutokakuwa na uhakika kuhusu hali ya uchumi kwa ujumla W ," Bw Kuijs alisema.
Wanunuzi wa nyumba wamekuwa wakikataa kufanya malipo ya mkopo wa nyumba wa nyumba ambazo majengo hayajakamilika hazijakamika.
Utashi wa kununua nyumba ni wa kiwango cha chini kwa ajili ya nyumba mpya na hilo limepunguza haja ya kuagiza bidhaa za ujenzi.
Huku wajenzi wa makazi wakikabiliwa na shinikizo, wachambuzi wanasema maafisa huenda wakalazimika kufaya juhudi zaidi kurejesha imani katika soko la makazi.
4. mabadiliko ya tabia nchi yanafanya tatizo hata kuwa baya zaidi
Hali mbaya za hewa inaanza kuwa na athari za kudumu kwa viwanda vya China.
Mawimbi makali ya joto, yaliyofuatiwa na ukame, vilipiga jimbo la kusini- magharibi la Sichuan na mji wa Chongqing mwezi Agosti. Huku idadi ya watu wanaohitaji viyoyozi (feni) ikiongezeka, huduma ya umeme imelielezea shirika la umeme katika eneo hilo ambalo kwa kawaida umeme utokanao na nguvu ya maji.
Viwanda, ikiwa ni pamoja na wazalishaji wakuu kama vile wakengenezaji wa iPhone Foxconn na Tesla,walilazimika kukatiza shughuli zao kwa saa au kufunga shughuli zao kabisa. hatimaye beijing iliingilia kati kunusuru mabilioni ya dola kwa kusaidia makampuni ya nishati na wakulima.
5. Makampuni ya teknolojia ya India yanapoteza wawekezaji
Ufuatiliaji na shinikizo la viwango kwa makampuni ya teknolojia ya China - ambao ulidumu kwa miaka miwili - hausaidii.
Makampuni ya Tencent na Alibaba yaliripoti kushuka kwa mapato kwa kiwango katika kipindi cha robo ya mwaka - faida za Tencent zilizshuka kwa 50%, huku mapato ya jumla ya Alibaba ya kishuka karbu kwa kiwango cha nusu ya mapato yake.
Vijana maelfu kwa maelfu wamepoteza ajira - na kuongeza mzozo wa kazi ambapo mtu mmoja kati ya watu watano wenye umri kati ya 16 na 24 hawana ajita. Hii inaweza kuathiri uzalishaji wa uchina na ukuaji kwa muda mrefu. Wawekezaji pia wanahisi mabadiliko katika Beijing - baadhi ya makampuni yaliyofanikiwa zaidi ya kibinafsi nchini China yamekuwa chini ya uchunguzi mkubwa huku mamlaka ya Bw Xi yakiongezeka.
Makampuni inayomilikiwa na taifa Ayanaonekana kupendelewa zaaidi, wawekezaji wa kigeni wanaondoa pesa zao katka makampuni hayo.
Benki ya Japan Softbank piliondoa kiasi kikubwa cha pesa zake katika Alibaba, huku Berkshire Hathaway ya Warren Buffet ikiuza hisa zake katika kiwanda cha magari cha BYD. Tencent iliondoa uwekezaji wa thamani ya zaidi ya uwekezaji wa dola bilioni 7 katika kipindi cha pili cha mwaka huu pekee.
Na marekani inayaondoa kwenye soko la hisa makampuni ya kichina yaliyoorodheshwa katika soko la hisa la Marekani.
"Baadhi ya maamuzi ya uwekezaji yanaahirishwa, na baadhi ya makampuni ya kigeni yanataka kupanua uzalishaji wake katika mataifa mengine ," taasisi ya viwango - S&P Global Ratings ilismea katika taarifa yake ya hivi karibuni.
Dunia inazoea ukweli kwamba Beijing inaweza kuwa wazi kwa biashara kama ilivyokuwa - lakini Bw Xi anahatarisha mafanikio ya kiuchumi ambayo yaliipatia nguvu China katika miongo ya hivi karibuni.