Mambo 9 ya kushangaza kuhusu wakati

sa

Chanzo cha picha, Edouard Taufenbach and Bastien Portout

Makala hii inakusudia kujibu maswali magumu kuhusu wakati, ikiwa ni pamoja na sayansi ya kusafiri kurudu nyuma ya muda au kwenda mbele ya muda, jinsi saa zinavyofanya kazi. Mambo 9 ya kushangaza kuhusu fizikia, saikolojia na historia ya wakati:

Lugha huathiri utambulisho wa muda

Namna tunavyousoma wakati huathiriwa na lugha tunayotumia. Kwa mfano, wazungumzaji wa Kiingereza huelezea wakati kama kitu chenye mbele na nyuma, au mstari wa mlalo unaotoka kushoto kwenda kulia.

Wazungumzaji wa Kimandarini wanatazama wakati kama mstari wa wima ambapo chini unawakilisha siku zijazo. Wagiriki muda una sehemu tatu; mkubwa, mwngi au mrefu. Jamii ya wenyeji wa Australia, katika eneo la Pormpuraww, huupanga muda kwa kuzingatia mashariki na magharibi.

Huenda isiwezekana kuwa na utambuzi bila kuwa na muda

Kusonga mbele kwa wakati ni kama mapigo ya moyo yasiyoonekana katika maisha yetu, na huathiri ufahamu wetu. Muda na utambuzi wako vinaenda sambamba. Hata mwanadamu aliye katika pango lenye giza bado anapitiwa na muda.

Holly Andersen, mtaalamu wa falsafa ya sayansi na metafizikia katika Chuo Kikuu cha Simon Fraser huko Burnaby, British Columbia, anaamini haiwezekani kuwa na ufahamu bila kuwa na wakati au kupita katika wakati. Fikiria jinsi utambulisho wako unavyojengwa kwa wakati, na kuhifadhiwa kama kumbukumbu.

Hakuna saa sahihi kwa 100%

ededs

Chanzo cha picha, Edouard Taufenbach and Bastien Portout

Maelezo ya picha, Je, muda unaweza kurudi nyuma katika baadhi ya matukio?

Wataalamu wa vipimo hufanya kazi kuuweka muda katika teknolojia bora na hupima kupita dakika, sekunde na saa. Ingawa saa zao ni sahihi, ila sio kamilifu. Hakuna saa duniani ambayo ni "sahihi" kabisa.

Mchakato wa kufafanua ni saa ngapi sasa - unategemea saa nyingi kote ulimwenguni. Maabara zote za kitaifa hutuma utunzaji wao wa wakati katika Ofisi ya Kimataifa ya Uzani na Vipimo huko Paris, ambayo hutengeneza wastani wa muda. Kwa hivyo wakati ni muundo wa mwanadamu.

Utambuzi wa wakati huundwa katika akili zetu

Mtazamo wetu kuhusu wakati unatokana na namna akili zetu zinavyofanya kazi. Muda sio tu kiini cha jinsi tunavyopanga maisha, lakini jinsi tunavyo yaishi.

Faida yake ni kwamba hii inatupa kiasi fulani cha udhibiti wa jinsi tunavyoutazama muda. Kwa mfano, kufanya shughuli kwa kurudia-rudia zitakupa hisia kuwa muda unakwenda haraka.

Kuna watu wataishi karne ya 22 miongoni mwetu

Karne inayofuata unaweza kuiona iko mbali sana: ambapo vizazi vitakavyo ishi karne hiyo havijazaliwa bado. Ila ukweli ni kwamba, kuna mamilioni ya watu duniani sasa ambao watakuwapo karne ya 22.

Mtoto aliyezaliwa mwaka wa 2023 atakuwa na umri wa miaka 70 mwaka 2099.

Uingereza kubadilisha saa

Kubadilisha saa kwa majira ya kiangazi - ili kutumia vyema saa ndefu za mchana - hakukubaliwi na kila mtu. Lakini ipende au ichukie, kuna mwanaharakati Mwingereza William Willett, alifanikiwa kuwashawishi viongozi wa kisiasa.

Uingereza ilifanya mabadiliko hayo wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia. Hatua hiyo ilikuja kwa sababu ya uhaba wa makaa ya mawe - na muda mrefu wa mchana ulimaanisha uhitaji mdogo wa umeme wa makaa ya mawe ili kuwasha taa.

Lilikuwa wazo zuri, Uingereza ilichukua hatua ya kuongeza saa mbili mbele ya GMT, kuokoa gharama za viwanda.

Muda, mwanga na sauti

Unaposoma maneno haya, ni rahisi kudhani ni "sasa". Hata hivyo, sivyo. Fanya kitendo rahisi cha kumtazama mtu anayezungumza nawe.

Uthibitisho utaona midomo yao inacheza kabla ya sauti kutoka (kwa sababu mwanga husafiri haraka kuliko sauti) lakini ubongo wetu husawazisha ili kuzifanya zilingane.

Na hilo si jambo la ajabu kidogo kuhusu wakati. Sheria za fizikia zinaonyesha katika hali zingine. Mwanafalsafa Katie Robertson anaelezea athari za kizunguzungu na muda.

Siku zetu zinarefuka kutokana na masafa ya mwezi

swe

Chanzo cha picha, Edouard Taufenbach and Bastien Portout

Maelezo ya picha, Je, muda ni njozi tu?

Huenda ikakushangaza kujua kwamba Mwezi - katika mzunguko wa sayari yetu – unasogea mbali na dunia. Kila mwaka umbali kati ya Dunia na Mwezi huongezeka kwa nchi 1.5 (sentimita 3.8). Na kufanya siku zetu kuwa ndefu kidogo.

Mwezi kukimbia dunia kumesababisha urefu wa wastani wa siku ya dunia kuongezeka kwa takriban milisekunde 1.09 kwa karne tangu mwishoni mwa miaka ya 1600. Ingawa hayaonekani kuwa mabadiliko makubwa lakini yatakwua makubwa katika kipindi cha miaka bilioni 4.5 ijayo.

Watu wengi hawaishi 2023

Kwa Wanepali wengi, makala haya hayakuchapishwa mwaka 2023. Katika kalenda ya Kinepali ya Bikram Sambat, ni mwaka 2080. Takribani kalenda nne hutumiwa kati ya makabila tofauti huko.

Myanmar ni mwaka 1384 , nchini Thailand ni 2566, nchini Ethiopia ni 2016, ambapo mwaka huchukua miezi 13. Kalenda ya Kiislamu ni mwaka 1445.