AFCON 2023: Nini tunapaswa kujua kuhusu nusu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika

.

Chanzo cha picha, BBC Sport

Hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) imewadia huku michezo ya robo fainali ikiambatana na mabao ya dakika za lala salama, mikwaju ya penalti na uchezaji bora wa makipa.

Katika michuano hiyo ambapo mashabiki walishuhudia kushindwa na kuondolewa kwa timu maarufu, timu nne zilizosalia kwenye michuano hiyo zote zina historia ya kushinda barani Afrika.

Ivory Coast, wenyeji wa mechi hizo, waliweka matumaini ya kunyanyua kombe hilo kwa ushindi mnono dhidi ya Mali.

Nahodha wa Afrika Kusini Ronwen Hayden Williams aliokoa penalti nne katika pambano la kusisimua dhidi ya Cape Verde na kusaidia katika ushindi wa Bafana Bafana.

Nigeria ilikuwa timu iliyoimarika hatua kwa hatua wakati wa michuano hiyo na kuweza kutinga nusu fainali kwa ushindi dhidi ya Angola, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo licha ya kuwa nyuma ya Guinea, iliweza kurejea mchezoni na kutinga fainali ya timu nne za mashindano hayo.

Kwa njia hii, katika nusu fainali, Nigeria itacheza na Afrika Kusini Jumatano, na kisha Ivory Coast itacheza dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Je, tunajua nini kuhusu michezo ya nusu fainali?

Afrika Kusini itamenyana na Nigeria mjini Boake, huku kocha Hoopoe Bruce akisema timu yake "haina cha kupoteza".

Nigeria, ambayo inapewa nafasi kubwa ya kufika fainali, ilishinda Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara ya mwisho mwaka wa 2013 na inatafuta taji lao la nne kwenye michuano hiyo.

Katika nusu fainali ya pili, wenyeji wanamenyana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika Uwanja wa Alassane Ouattara mjini Abidjan.

Mchezo bora zaidi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ulikuwa dhidi ya Guinea, na timu hii ilipigana kwa moyo wake wote na kufanikiwa kushinda 1-3.

Timu hiyo italazimika kumenyana na Ivory Coast ambao walikuwa karibu kurejea nyumbani baada ya kufanya vibaya kwenye hatua ya makundi.

Ivory Coast ilimfukuza kocha Jean-Louis Gasse wakati ilionekana kana kwamba hawakuwa na nafasi ya kusonga mbele kutoka kwa kundi lao. Baada ya hapo, Emres Fae akawa kocha mkuu wa muda na aliweza kuzichabanga Senegal (mabingwa watetezi) na Mali.

Mechi ya fainali itafanyika Februari 11 mjini Abidjan, na mechi ya kumjua mshindi wa tatu na nne itafanyika siku moja kabla ya hapo.

Uchambuzi juu ya uchezaji wa timu

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Wataalamu wengi walidhani kwamba Senegal, timu ambayo ilishinda kombe la ubingwa kwa mara ya kwanza katika michezo ya awali nchini Cameroon, ina nafasi nzuri zaidi ya kushinda wakati huu. Hisia ambazo ziliimarishwa baada ya Senegal kutinga hatua ya 16 bora ikiwa na pointi nyingi zaidi.

Hata hivyo, “Taranga Lions” hawakuweza kupita kizuizi cha wenyeji katika hatua ya 16 bora licha ya bao la mapema walilofunga dhidi ya Ivory Coast.

Uchezaji mzuri hatua ya makundi ulikuwa timu mbili zisizojulikana za mashindano hayo. Equatorial Guinea na Cape Verde, licha ya kutovutia sana kabla ya mechi, zote zilifuzu kwa hatua ya mtoano zikiwa vinara wa makundi yao.

Equatorial Guinea, bila shaka, ilishindwa, huku Emilio Vansue, mfungaji bora wa michuano hiyo kufikia sasa, akikosa penalti.

Cape Verde iliongoza Kundi B mbele ya Misri na Ghana, lakini ndoto ya Blue Sharks ilifikia kikomo waliposhindwa na Afrika Kusini katika robo-fainali.

Angola ilikuwa moja ya timu nyingine zilizoshangaza katika mashindano hayo. Timu hiyo iliongoza Kundi D na Ferdi, nahodha wa timu, washambuliaji wake, Mabulolo na Golsen Dala walicheza kwa kiwango ambacho kilizidi matarajio. Utendaji mzuri wa timu hii uliendelea katika hatua ya 16 dhidi ya Namibia, lakini katika robo ya kwanza, nguvu ya washambuliaji wa timu hii haikufikia safu ya ulinzi ya Nigeria

Ingawa Nigeria ilifuzu kwa urahisi katika hatua ya muondoano, timu hii haikufanya vyema kulingana na matarajio ya mashabiki wakati wa mashindano hayo na kupata matokeo bora zaidi mchezo baada ya mchezo. Kipengele muhimu zaidi cha timu hii ni safu yake ya ulinzi imara, ambayo imefanya ushindi dhidi ya Nigeria kuwa kazi ngumu sana.

Morocco, haswa baada ya mchezo wao mzuri kwenye Kombe la Dunia la 2022 huko Qatar, ambayo ilifika nusu fainali, walionekana kama washindani wakuu kabla ya mashindano hayo. Lakini "Atlas Lions" iliondolewa kwenye michuano hiyo baada ya kufungwa 2-0 dhidi ya Afrika Kusini katika hatua ya 16 bora. Kwa njia hii, kusubiri kwa Morocco kushinda ubingwa wa pili wa Afrika imekuwa karibu nusu karne.

Morocco haikuwa jina pekee kubwa kuhangaika katika mashindano haya. Wakiwa wamepoteza mechi zao mbili kati ya tatu za hatua ya makundi, Ivory Coast ilijitahidi kufuzu kama moja ya timu nne bora za michuano hiyo, ikimaliza ya tatu katika kundi lao.

Bila shaka, "Elephants" walipoteza makali yao katika mchezo dhidi ya Senegal na kisha Mali, na sasa wana nafasi ya kushinda Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara ya tatu.

Cameron pia alikuwa mmoja wa majina mengine ambao walishindwa katika mashindano haya. Timu hii ilisonga mbele kwa shida kutoka hatua ya makundi na kisha kwenda nyumbani baada ya kushindwa na Nigeria.

Ghana na Algeria timu mbili ambazo zina historia ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo pamoja na Tunisia ndizo timu dhaifu za kipindi hiki ambazo zilifanikiwa kupata pointi mbili pekee katika hatua ya makundi.

.

Chanzo cha picha, BBC Sport

Maelezo ya picha, Emilio Ensue wa Equatorial Guinea ndiye mfungaji bora wa michuano hiyo hadi nusu fainali

Wafungaji bora wa Kombe la Mataifa ya Afrika kabla ya hatua ya nusu fainali

Mabao matano: Emilio Ensue (Equatorial Guinea)

Mabao manne: Golson Dala (Angola), Mustafa Mohamed (Misri)

Mabao matatu: Ademola Lookman (Nigeria), Mabololo (Angola), Lassin Sinaiko (Mali), Mohamed Bayo (Guinea), Baghdad Boujanah (Algeria), Bertrand Traore (Burkina Faso).

Imetafsiriwa na Asha Juma