Kifahamu Chuo Kikuu cha kwanza na kikongwe zaidi duniani kilichotokana na msikiti

Chanzo cha picha, BC/THOMAS BUTTERY
Chuo kikuu ninachozungumzia hapa sio Oxford au Harvard, wala sio Chuo Kikuu maarufu cha Cambridge. Nitakutambulisha huko Morocco katika jiji la Fes, ambalo ni mahali palipozaliwa maarifa ya kisasa. Ni jiji ambalo limethibitishwa kuwa lilifungua chuo kikuu cha kwanza ulimwenguni katika karne ya tisa.
Wakati huo ambapo Ulaya na kwingineko duniani wakitatizika na giza la ujinga, nuru ya maarifa ilikuwa ikimulika Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, iliyokuwa ikitoka katika safari ndefu nje ya bara la Afrika, ili kukata kiu yao kufanikiwa kutokomeza janga la ujinga lililoonekana kuchelewa kuondolewa.
Kwa hivyo, katika mji wa Fez huko Morocco, msikiti uitwao AL QARAWYIN ulifunguliwa mnamo 859 AD, ambao ulibadilika kuwa shule ya elimu na kutambuliwa kama chuo Kikuu cha kwanza ulimwenguni.

Chanzo cha picha, BBC/CHRIS GRIFFITHS
Fatuma Binti Mohamed Al Fihriy, ambaye alikuwa msichana mdogo, alipata sehemu kubwa zaidi ya urithi wa babake na akautumia kufungua chuo kikuu hiki ambacho kinanufaisha ulimwengu wa Kiislamu na jamii nzima.
Chuo Kikuu cha Al Qarayiwiin, ambacho kinachukuliwa kama Chuo kinachosimamiwa vyema, kimekuwa kinara katika elimu ya kisasa ambayo haijaonekana hapo awali, na imekuwa na nafasi kubwa katika ukuaji wa uislamu.
Al Qarawiyin inajulikana kuwa jukwaa la kwanza kutoa vyeti kulingana na kiwango cha elimu ya mtu. Hapa ndipo utamaduni wa vyuo vikuu kote ulimwenguni ulipoanzia, ambavyo ni vyeti ambavyo hutolewa mwishoni mwa elimu. Vyuo vikuu maarufu zaidi ulimwenguni leo, kama vile Oxford, Bologna na Cambridge, vilijengeka kati ya karne mbili hadi nane baada ya kuundwa kwa Al Qarawiyin.
Miongoni mwa masomo yaliyotolewa na chuo hicho ni masomo ya Kiislamu, lugha ya Kiarabu, hisabati na utabibu, na yaliwavutia wanafunzi wengi na macho ya wanasayansi maarufu.

Chanzo cha picha, BBC/CHRIS GRIFFITHS
Chuo kikuu kinachojulikana kwa jina la Chuo Kikuu cha AL QARAWIYIN kilijumuishwa rasmi katika mfumo wa elimu wa Morocco mnamo mwaka 1963, na tawi lingine la Chuo Kikuu lilifunguliwa katika mji huo huo wa Fes huko Morocco.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu hicho walikuwa katika mitaala ya Chuo hicho wakisomea sheria za Kiislamu, sarufi, lugha, sayansi, hisabati na mengineyo.
Mijadala ya kiutendaji ilifanyika, mawazo ya kielimu yanayoweza kuleta mabadiliko yalijadiliwa, changamoto za sasa zilichambuliwa na jinsi ya kuzitatua na mtu yeyote ambaye alionekana kuwa na maoni alialikwa.

Chanzo cha picha, BBC/CHRIS GRIFFITHS
Kwa upande mwingine, chuo kikuu kina maktaba ambayo inatajwa kuwa moja ya maktaba kubwa zaidi kuwahi kuanzishwa na bado iko hai, kama ilivyotangazwa na Umoja wa Mataifa au kunukuliwa kutoka Idara ya Elimu, Sayansi na Utamaduni ya UNESCO. Ilirekodiwa katika Kitabu cha rekodi za dunia cha Guinness na kutambuliwa kama chuo Kikuu kikongwe zaidi ulimwenguni ambacho bado kinafanya kazi.
Maktaba ya chuo kikuu, ambayo inaweza kusemwa kuwa nyumba ya ujuzi, imepambwa na stashahada ya Faduma Al Fihri iliyobandikwa kwenye ubao wa mbao, miswada iliyohifadhiwa tangu karne zilizopita, kitabu cha Muqaddima cha Ibn Khaldun, nyenzo muhimu na kazi za sanaa mbalimbali.
Msikiti wake una paa za kuvutia, dari nzuri, rangi angavu na sehemu za kuvutia za kutembelea, na viwanja vyake viko wazi hata kwa wasio Waislamu, ambao wanaweza kutafakari wakiwa ndani na nje ya msikiti huo, pamoja na majengo yake na njia za maji.

Chanzo cha picha, BC/THOMAS BUTTERY
Maboresho zaidi yalifanywa kwa ujenzi wa msikiti na uwanja wa chuo kikuu kwa ujumla na miundo ya maua iliongezwa katika karne ya 12.
Kwa bahati mbaya, katika karne hizo hakuna maandishi yenye ufanisi isipokuwa kwa watu adimu kama mwanafalsafa na mwanahistoria Ibn Khaldun, inaweza kusemwa kwamba kuna ukuta unaotuzunguka kutoka sehemu ya historia ya chuo kikuu ambayo bado haijatufikia.
Miongoni mwa wahitimu mashuhuri waliohitimu chuo kikuu hicho ni nabii wa Kiislamu wa karne ya 12 Ibn Rushdi, Papa Sylvester ambaye inasemekana alijifunza lugha ya Kiarabu, hasa namba, na baadaye kwenda Ulaya, Moses ben Maimon, Ibn Al Haj Al Badri. , mwanafalsafa Ibn Arabi, mwandishi mwandamizi, mwanasayansi na mwanasiasa Ibn Khaldun, mwandishi Leo Africanus, Mufti Ahmed Mohamed Al-Maqaari na wengine wengi.












