Kombe la Dunia Qatar 2022: Kwa nini kuna muda mwingi wa ziada unaoongezwa?

Tuna siku mbili pekee katika Kombe hili la Dunia na tayari tunaona mtindo fulani unaondelezwa:

Muda wa ziada

Mechi hizo nne hadi sasa zimeongezwa takriban dakika 65 kati yao, na mechi ya England dhidi ya Iran ikidumu kwa dakika 117 na sekunde 16.

Hilo lilisababishwa na majeraha - mlinda mlango wa Iran Alireza Beiranvand alizirai baada ya kugongana kichwa na mhezaji mwengine mapema. Lakini pia ni sehemu ya juhudi za pamoja za Fifa kudhibiti muda unaopotezwa kwa kufuatilia kwa usahihi muda ambao mchezo umesimamishwa.

Sababu za kusimamisha mchezo huo ni pamoja na majeruhi, maamuzi ya wasaidizi wa video, ubadilishaji wa wachezaji, adhabu na kadi nyekundu, huku baadhi ya wachezaji mara nyingi wakiahirisha mchezo kuanza kwa makusudi baada ya matukio hayo ili kupoteza muda zaidi.

Mwenyekiti wa kamati ya waamuzi wa Fifa Pierluigi Collina alithibitisha wiki iliyopita kwamba maafisa wasaidizi nje ya uwanja wa mpira walipewa maagizo ya kufuatilia muda uliopotea wakati wa mchezo katika michuano hiyo nchini Qatar, jambo ambalo walijaribu pia kufanya kwenye michuano ya awali ya Kombe la Dunia nchini Urusi mwaka 2018.

"Nchini Urusi, tulijaribu kuwa sahihi zaidi katika kufidia muda uliopotea wakati wa michezo na ndiyo maana uliona dakika sita, saba au hata nane zikiongezwa," aliwaambia waandishi wa habari kwenye mkutano wa kabla ya mashindano kuanza.

"Fikiria juu yake: ikiwa una mabao matatu katika kipindi cha kwanza, labda utapoteza dakika nne au tano kwa jumla kwa sherehe na kuanza tena kwa mchezo."

Matokeo ya mbinu hii mpya ilisababisha idadi ya rekodi kuvunjwa.

Kulingana na Opta, Nusu nne za mechi zilizo na muda mwingi zaidi wa ziada katika mechi moja ya Kombe la Dunia tangu rekodi zilipoanza mwaka 1966 zote zilikuwa Jumatatu:

  • England v Iran kipindi cha kwanza (14:08 dakika)
  • England v Iran kipindi cha pili (13:08)
  • USA v Wales kipindi cha pili (10:34)
  • Senegal v Uholanzi second half (10:03)

Cha kushangaza ni kwamba muda wote huo ulioongezwa ulisababisha magoli ya dakika za mwisho.

Penalti ya Mehdi Taremi ya Iran dhidi ya Uingereza ilijiri baada ya saa 102:30 mchana, likiwa ni bao la mapema zaidi katika rekodi ya Kombe la Dunia ukiondoa muda wa ziada.

Hilo lilifuatiwa kwa haraka na la pili la mapema zaidi, huku bao la Davy Klaassen la Uholanzi likitokea baada ya dakika 98 na sekunde 17.

Mbinu hiyo kwa hakika imezua taharuki kwenye mitandao ya kijamii, huku baadhi ya mashabiki wakipongeza jitihada za Fifa za kubana upotevu wa muda lakini wengine wakihisi inasababisha michezo mirefu isio na lazima.

Vyovyote vile, inapaswa kukufanya ufikirie mara mbili ikiwa utafikiria kuacha mechi ikiendelea hujui ni muda gani utakosa.