Habari 4 njema kuhusu matibabu ya saratani zinazoleta matumaini kwa wagonjwa

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Hatua zilizofikiwa katika tiba ya saratani kunatoa matumaini kwa wagonjwa

Mkutano wa kila mwaka wa Jumuiya ya Marekani ya Clinical Oncology (Asco) ulileta habari njema kuhusu matibabu ya aina mbalimbali za saratani.

Madaktari wawasilisha hatua zilizofikiwa katika vita dhidi ya uvimbe kwenye mapafu, ubongo, puru na Hodgkin's lymphoma, aina ya saratani inayoathiri chembe za mfumo wa kinga.

Hapo chini, tunatoa tafiti nne kuu zilizotolewa wakati wa hafla hiyo.

Saratani ya mapafu: tiba ya kuongeza muda wa kuishi

Watafiti katika Kituo cha Saratani cha Yale (USA) walionyesha kuwa dawa ya osimertinib - ambayo imekuwa ikitumika kwa miaka mitatu kwa watu walio na aina maalum ya saratani ya mapafu - ina uwezo wa kurefusha maisha ya wagonjwa ambao wamefanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe.

William Nassib William Jr, mtaalam wa magonjwa ya saratani na kiongozi wa utaalam wa uvimbe wa Kikundi cha kliniki za onkolojia, anaelezea kuwa dawa hii ni kwa wagonjwa walio na saratani ya mapafu ya seli isiyo ndogo - aina ya kawaida ya ugonjwa wa mapafu - ambao umekuwa na mabadiliko katika jeni inayoitwa EGFR.

Uvimbe huu unapogunduliwa katika hatua zake za awali, kwa kawaida madaktari hufanya upasuaji ili kuondoa tishu zilizoathiriwa za mapafu. Lakini daima kuna swali: kuna seli za saratani katika eneo hilo?

Hii ni mojawapo ya matatizo makuu baada ya operesheni, kwani uvimbe huo mdogo unaweza kukua kwa muda unavyosonga na kurejesha ugonjwa huo.

Ili kuepuka hali hii, wataalam wanaagiza kinachojulikana kama matibabu ya kusaidia, ambayo hujaribu kuondoa seli za ugonjwa ambazo haziwezi kuondolewa kwa upasuaji.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Tiba inayolengwa hufanya kazi tu kwenye seli zilizo na mabadiliko maalum ya jeni
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Katika siku za nyuma, njia kuu iliyotumiwa kufanya aina hii ya matibabu ilikuwa chemotherapy. Sasa, matibabu yaliyolengwa yameonekana kujitokeza - kama vile osimertinib- ambayo hufanya kazi kama makombora ya kuongozwa na kushambulia molekuli maalum za uvimbe.

Hata hivyo, matumizi ya matibabu haya ya kisasa zaidi yanahitaji majaribio ya kuchambua wasifu wa maumbile ya saratani na mabadiliko yanayotokea ndani yake.

Osimertinib, kwa mfano, inafanya kazi tu kwa watu binafsi wanaobeba jeni iliyobadilishwa ya EGFR, ambayo inawakilisha kati ya 15% na 20% ya watu walio na saratani ya mapafu ya seli isiyo ndogo.

Matokeo ya dawa hii iliyochapishwa katika majarida ya kisayansi yalionyesha kuwa 85% ya wagonjwa waliokidhi vigezo hivi na kuchukua osimertinib walinusurika kifo hadi miaka 5.

Katika kundi la matibabu ya kutuliza akili ilikuwa 73%.

"Hii inaimarisha wazo kwamba dawa hii inazuia seli hizi ndogo za saratani kutoka kwa ukuaji tena, au labda hata kuziondoa kabisa, na hivyo kuongeza muda wa kuishi kwa wagonjwa," anasema William Jr.

Daktari anasema kwamba dawa za kisasa zaidi katika onkolojia - kama vile matibabu yaliyolengwa na matibabu ya kinga, ambayo tutazungumzia baadaye - yanajaribiwa (na kuidhinishwa) taratibu kwa awamu za awali kabisa za ugonjwa huo.

Awali, yalikuwa tu kwa ajili ya saratani ambazo zimesonga kihatua na wakati tayari ugonjwa umeenea.

"Kwa hili, tutazungumza zaidi na zaidi sio tu juu ya kudhibiti uvimbe huu, lakini hata juu ya kuponya," anatabiri.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Uvimbe wa ubongo wenye saratani (Glioma) bila matibabu ya ya kemotherapi

Ubongo haujaundwa tu na chembe za neva. Kiungo kinachohusika na kumbukumbu na kufikiri kina seli za glial, ambazo ni muhimu kwa utendaji na kinga ya mfumo mkuu wa neva.

Tatizo ni kwamba seli hizi zinaweza pia kubadilika na kuwa saratani. Katika kesi hii, ugonjwa unaojulikana kama glioma.

Kuna aina ambayo ina sifa maalum sana. Glioma ya kiwango cha chini kawaida huwa polepole na haina maumivu makali: mgonjwa kawaida huishi miaka au miongo kadhaa baada ya utambuzi.

"Hata hivyo, ina athari kubwa kutokana na ukweli kwamba inaathiri vijana, kwa kuwa inaonekana karibu na umri wa miaka 20," anasema Clarissa Baldotto, daktari katika Kamati ya Tumors ya Mfumo Mkuu wa Neva wa Jumuiya ya Brazili ya Kliniki ya onkolojia - (SBOC).

Eneo hili la dawa halijakuwa na taarifa zozote kwa miaka mingi na ukweli kwamba uvimbe hukua kwenye ubongo, eneo nyeti kama hilo, ilifanya iwe ngumu kukuza matibabu salama na madhubuti.

Lakini hii ilibadilika na uwasilishaji wa utafiti ambao ulitathmini vorasidenib, kutoka kwa maabara ya Servier, ambayo pia ni tiba inayolengwa.

Watafiti kutoka Kituo cha Saratani ya Memorial Sloan Kettering (USA) walionyesha kuwa dawa hii inapunguza hatari ya ugonjwa kuendelea au kifo kwa 61%.

Kwa kuongeza, matibabu mapya yana faida ya pili. Inaahirisha hitaji la kutumia matibabu mengine yenye sumu zaidi (kama vile chemotherapy na radiotherapy) ili kudhibiti kuenea kwa seli za saratani kwenye ubongo.

Kuepuka sumu hii ni muhimu zaidi katika kesi ya gliomas ya kiwango cha chini, kwa kuwa waathirika wakuu wa ugonjwa huo ni vijana, ambao wangeweza kuteseka kwa matatibabu hayo kwa miongo mingi.

Baldotto anaita matokeo ya utafiti huo kuwa "ya kuvutia."

"Majaribio ya kimatibabu pia yalionyesha kuwa dawa hii, inayotumiwa mara moja kwa siku iliyo kwa mfumo wa tembe, inavumilika na ina kiwango cha chini cha madhara," anaongeza.

Kama ilivyo kwa saratani ya mapafu ya seli isiyo ndogo hapo juu, mgonjwa wa glioma anahitaji kufanyiwa uchunguzi ili kutathmini mabadiliko ambayo uvimbe uko nayo.

Vorasidenib hufanya kazi wakati kuna mabadiliko katika jeni za IDH1 na IDH2.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Saratani ya puru: njia moja zaidi ya kuiponya

Ndani ya ulimwengu wa saratani ya utumbo mpana (ambayo huathiri sehemu ya mwisho ya mfumo wa usagaji chakula), uvimbe unaotoka kwenye puru huwakilisha takriban theluthi moja ya wenye ugonjwa huo.

Wanasayansi katika Kituo cha Saratani ya Memorial Sloan Kettering wameonyesha kuwa mbinu mbili tofauti za matibabu zinaweza kufikia matokeo sawa: kiwango cha juu cha kuishi na hata tiba baada ya miaka mitano ya matibabu.

Katika utafiti huo, sehemu ya watu waliojitolea walio na uvimbe huu, walifanyiwa matibabu ya tiba ya mionzi ya chemotherapy na radiotherapy. Sehemu nyingine, yenye sifa sawa, iliamua tu kufanyiwa tiba ya chemotherapy pekee.

Matokeo yao yalilinganishwa na yalionyesha athari nzuri sawa: karibu 80% ya washiriki katika makundi yote mawili walikuwa hai na hawakuwa na ugonjwa ndani ya miaka mitano.

"Katika miaka ya hivi majuzi, tumepiga hatua kubwa katika matibabu ya ugonjwa huu," asisitiza mtaalamu wa saratani Virgílio Souza e Silva, kutoka Kituo cha Saratani cha A.C.Camargo, huko Sao Paulo.

Kwa maoni yake, data iliyotolewa "inabadilisha kilichokuwepo miaka 20 iliyopita", lakini haina maana kwamba matibabu ya radiotherapy yatatelekezwa kabisa.

"Baadhi ya watu wataendelea kunufaika na tiba ya mionzi. Kwa wengine, chemo pekee itatosha," anasema.

Wengine, chemo pekee itatosha", anahakikishia.

Hodgkin lymphoma: Mabadiliko katika njia ya kutibiwa

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Aina hii ya saratani huathiri baadhi ya seli za mfumo wa king na hili linajidhihirisha kwa vijana katika muongo wa pili au wa tatu wa maisha.

Katika hatua za juu zaidi za ugonjwa huo, matibabu ya kawaida yana chemotherapy na dawa inayoitwa brentuximab vedotin, kutoka kwa kampuni ya dawa Takeda.

Wataalamu kutoka Kituo cha Matibabu cha City of Hope, pia nchini Marekani, waliamua kupendekeza mbadala katika mpango huu.

Wamejaribu ikiwa brentuximab vedotin inaweza kubadilishwa na nivolumab (Bristol Myers Squibb), aina ya tiba ya kinga, kitengo kimoja na dawa zinazochochea mfumo wa kinga ya mgonjwa kutambua na kushambulia seli za saratani.

Takwimu za awali kutoka kwa utafiti huu zinaonyesha kuwa 94% ya wagonjwa waliopokea mpango mpya wa matibabu (nivolumab + chemotherapy) walikuwa bado hai katika miezi 12. Miongoni mwa wale ambao waliendelea na mchanganyiko uliopita (brentuximab vedotin + chemo), kiwango kilikuwa 86%.

Guilherme Perini, daktari wa magonjwa ya damu katika Hospitali ya Waisraeli ya Albert Einstein huko Sao Paulo, anahitimisha utafiti huo kama "wa kihistoria" na anaangazia kipengele kingine: kazi ilijumuisha wafanyakazi wa kujitolea wadogo, wenye umri wa miaka 12 na zaidi.

Faida nyingine ya nivolumab ilikuwa uvumilivu mkubwa wa wagonjwa kwa madhara. Waandishi wenyewe wanasema kwamba ni muhimu kuchunguza makundi yote mawili kwa muda mrefu, lakini wanaamini kwamba matokeo yaliyopatikana yanatumika kama msingi wa kubadilisha njia ambayo ugonjwa wa saratani ya Hodgkin lymphoma inavyotibiwa hii leo.