Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa: Arsenal yamtaka Coman, Madrid wamgeukia Haaland
Arsenal wanaangalia uwezekano wa kumsajili winga wa Ufaransa wa Bayern Munich mwenye umri wa miaka 28, Kingsley Coman. (Star)
Rais wa Real Madrid, Florentino Perez, anataka kumsajili mshambuliaji wa Norway wa Manchester City mwenye umri wa miaka 24, Erling Haaland. (Fichajes)
Manchester United na Liverpool ni miongoni mwa klabu zinazopenda kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa wa Lyon mwenye umri wa miaka 21, Rayan Cherki, msimu huu wa joto. (Mail)
Manchester United na Tottenham wamefanya mazungumzo na Eintracht Frankfurt kuhusu usajili wa kipa wa Brazil mwenye umri wa miaka 22, Kaua Santos. (Bild)
Chelsea walijaribu kumsajili beki wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 33, Virgil van Dijk, msimu huu wa joto, kabla ya kusaini mkataba mpya na Liverpool. (Mail)
Mshambuliaji wa Ureno wa Chelsea mwenye umri wa miaka 25, Joao Felix, ambaye yuko kwa mkopo AC Milan, anataka kuhamia Saudi Arabia au klabu yake ya zamani ya Benfica msimu huu wa joto. (Sport )
Liverpool wanataka kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa wa Eintracht Frankfurt mwenye umri wa miaka 22, Hugo Ekitike, msimu huu wa joto. (Caught Offside)
Everton wanatarajiwa kushindana na Inter Milan kwa ajili ya kumsajili kiungo wa Iceland wa Genoa mwenye umri wa miaka 27, Albert Gudmundsson, ambaye yuko kwa mkopo Fiorentina. (Teamtalk)
Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti, anatarajiwa kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa mwezi baada ya fainali ya Copa del Rey dhidi ya Barcelona, huku Brazil wakitarajia kumteua raia huyo wa Italia mwenye umri wa miaka 65 kuwa kocha wao wa timu ya taifa. (Sky Sports)
Nottingham Forest wanapanga kuanza mazungumzo mapya ya mkataba na winga wa Uingereza mwenye umri wa miaka 24, Callum Hudson-Odoi. (Football Insider)
Barcelona wamejiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili winga wa Hispania anayekipiga Athletic Bilbao mwenye umri wa miaka 22, Nico Williams. (Marca)
Arsenal, Liverpool na Chelsea wanaongoza kinyang'anyiro cha kumsajili winga wa Hispania chini ya miaka 21 wa Real Betis mwenye umri wa miaka 19, Jesus Rodriguez. (Caught Offside)
Atletico Madrid wanaataka kumsajili winga wa Argentina wa Manchester United mwenye thamani ya pauni milioni 70, Alejandro Garnacho, mwenye umri wa miaka 20, lakini watakumbana na ushindani kutoka kwa Bayer Leverkusen. (Teamtalk)
Tottenham ni miongoni mwa vilabu kadhaa vinavyomfuatilia mshambuliaji wa Gambia wa Dutch Lions mwenye umri wa miaka 17, Gibril Sima. (Football Insider), external