Sababu saba zinazoiweka Sri - lanka katika mzozo

Mgogoro wa Siri- lanka

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Maandamano ya Sri- lanka yaliomlazimu rais kujiuzulu

Sri Lanka ni nchi yenye misukosuko; Rais Gotabaya Rajapaksa hatimaye alijiuzulu siku ya Alhamisi baada ya kukimbilia Singapore. Kaimu rais wa nchi hiyo, Waziri Mkuu Ranil Wickremesinghe, anajaribu kuendesha nchi kutoka "eneo salama" baada ya ofisi yake kuvamiwa na makazi yake ya kibinafsi kuchomwa moto.

Waziri Mkuu Wickremesinghe ameweka marufuku ya kutotoka nje na kuwataka wanajeshi kufanya 'chochote kinachohitajika kurejesha utulivu.'

Taifa hilo linakumbwa na ukosefu wa mafuta, chakula, madawa na vitu vingine muhimu, na waandamanaji wanalaumu wanasiasa kwa tatizo hilo .

Hizi hapa sababu kuu za mzozo wa kiuchumi na kisiasa unaokumba Sri Lanka:

Gharama ya maisha

Uchumi wa taifa hilo la kisiwa cha bahari hindi kilicho na takriban watu milioni 22 umedhoofika kwa muda sasa.

Kulingana na banki kuu ya taifa hilo , kwa jumla mfumuko wa kila mwaka wa taifa hilo umepita kiwango cha asilimia 50 na mfumuko wa chakula ndio mbaya zaidi ukiwa katika asilimia 80.

Sarafu ya Sri- lanka , rupee inaendelea kudidimia dhidi ya dola: W akati rais Gotabhaya Rajapakse alipochukua uongozi mnamo mwezi Novemba 2019, kiwango cha ubadilishanaji wa fedha kwa dola moja kilikuwa rupee 179. Lakini sasa kimefikia zaidi ya Rupee 360.

Gharama ya uchukuzi pia imeongezeka maradufu . Hata wale walio na fedha hawawezi kununua chakula na mafuta kutokana na uhaba mkubwa wa bidhaa hizo mbilki.

Shirika la chakula duniani WFP linasema kwamba zaidi ya watu milioni sita hawajua kule watakapopata mlo wao wa baadaye.

Sababu za kimataifa

Vita vya Ukraine vimesababisha kupanda kwa bei za chakula na bidhaa za mafuta ya petroli. Sri Lanka inategemea uagizaji kwa mahitaji yake yote ya mafuta ya petroli , lakini tangu mwanzo wa mwaka huu , taifa hilo limeshindwa kulipia gharama ya uagizaji mafuta na gezi. Hali hiyo imepunguza kasi ya ukuaji wa uchumi wa eneo hilo kila sehemu.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Watu wengi sasa wanatumia kuni badala ya gesi kupika chakula.

Uhaba wa gesi umedumu sana hali ya kwamba baadhi ya sehemu za kuchomea maiti zimelazimika kufungwa, na wafu sasa wanazikwa badala yake, jambo ambalo sio desturi ya watu wengi wa Sri Lanka.

Mdororo wa kimataifa umesababisha raia wa Sri Lanka wanaoishi ng'ambo kuwa na pesa kidogo za ziada za kusaidia familia zinazotatizika nyumbani.

Pesa zinazotumwa kutoka nje zilishuka kutoka $515m mnamo Novemba 2019 hadi $248.9m mwezi Aprili, kulingana na Benki Kuu ya nchi.

Kuanguka kwa utalii

Jarida la kitalii la Lonely Planet lilitaja Sri Lanka kuwa kivutio kikuu cha watalii kwa 2019.

Ufukwe wa bahari wa lanka

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Ufukwe wa bahari wa lanka
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Matumaini ya mapato makubwa ya Utalii yalididimia hatahivyo wakati msururu wa mashambulizi ya kigaidi yalipofanyika Jumapili ya pasaka mnamo mwezi Aprili 2019.

Mashambulizi hayo yaliolenga hoteli tatu na makanisa matatu yaliwaua watu 267 na kuwajeruhi watu 500.

Baada ya Utalii katika kiswa hicho kuimarika na hivyobasi kuchangia pato la dola $450m wakati wa mwezi Disemba wa mwaka huo, kulingana na benki kuu – ikiwa ni pato la chini la mwezi kama huo mwaka uliopita.

Sekta hiyo baadaye ilizoroteshwa na mlipuko wa viruis vya corona.

Data kutoka Benki kuu ya taifa hilo kutoka Mwezi Aprili hadi mwezi Novemba 2020 inaonesha kwamba sekta hiyo ya kitalii iliathiriwa vibaya ikikosa mapato yoyote.

Kazi nyingi katika sekta hiyo zilipotea , hususan zile katika mikahawa iliop[o katika fukwe za bahari inayosifika sana na watalii wanaopenda kuota jua.

Mnamo mwezi Aprili 2021, rai swa Sri lanka alipiga marufuku uagizaji wa mbolea zote , na hivyobasi kuwalazimu wakulima kutumia mbolea ya nyumbani.

Hatua hiyo ilisukumwa na rai awa Sri lank ana wale walio ughaibuini kama hatua ya kuhifadhi mazingira , lakini ukweli ni kwamba ilitokana na kupungua kwa hifadhi ya fedha za kigeni.

Hatua hiyo iligonga mwamba vibaya . Katika maeneo mengi -mazo ya mchele – chakula kinachotumika sana nchini humo lilishuka , na kulifanya taifa hilo kutegemea chakula kutoka nje.

Mapema mwaka huu , serikali ilizindua mipango ya kuagiza tani 400,000 za mchele kutoka india na Myanmar , lakini haijulikani ni kiwango kilichowafikia raia.

Usawa wa kibiashara

Sri Lanka sasa inaagiza bidhaa zenye thamani ya $3bn zaidi kuliko inazouza nje kila mwaka, na hiyo inaelezea kwa nini imekosa fedha za kigeni.

Mauzo ya nje huenda yakaathirika zaidi kutokana na kudorora kwa uchumi kunakosababishwa na uhaba wa nishati na dizeli.

Lakini nchi haiwezi kununua bidhaa nyingi zaidi za petroli kufanya nishati inayohitajika na tasnia yake kwa sababu imekosa pesa.

Mwishoni mwa 2019, Sri Lanka ilikuwa na akiba ya fedha za kigeni $7.6bn, lakini hizi sasa zimeshuka hadi karibu $250m. (All figures from the Central Bank)

Madeni

Miongo mitatu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sri Lanka ilimalizika mwaka 2009. Katika kipindi cha baada ya vita, serikali iliendelea na ujenzi na kuwekeza pakubwa kwenye miundombinu kama vile barabara na bandari.

Uhaba wa dawa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Uhaba wa dawa Sri - lanka

Pesa zilitoka kwa kukopa na nchi inakabiliwa na mzigo wa deni la $51bn - ikiwa ni pamoja na $ 6.5bn inayodaiwa na China.

Kulipa deni kumemaliza akiba ya pesa, na kuacha kidogo kununua chakula.

Kundi la G7 la nchi zinazoongoza kwa viwanda - Kanada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan, Uingereza na Marekani - limesema linaunga mkono majaribio ya Sri Lanka ya kupunguza ulipaji wa madeni yake.

Benki ya Dunia imekubali kuikopesha Sri Lanka $600m, na India imetoa angalau $1.9bn.

Serikali ya Sri Lanka pia imekuwa katika mazungumzo na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kuhusu uwezekano wa mkopo wa $3bn.

Siasa za kitabaka

Katika mitaa ya Colombo, hisia za hasira dhidi ya Rais aliyeondolewa madarakani Gotabaya Rajapaksa - na familia yake ambayo imetawala siasa kwa miongo miwili iliyopita, Waandamanaji wanamlaumu rais - na wanafamilia ambao wamekalia nyadhifa za juu serikalini - kwa muda.

Kakake mkubwa Gotabaya, Mahinda Rajapaksa, alikuwa rais kwa muongo mmoja kuanzia 2005. Familia hiyo inashutumiwa kwa kujilimbikizia mali kupitia ufisadi, jambo ambalo wanalikanusha.

Gotabaya alipokuwa rais alimteua Mahinda kuwa waziri mkuu. Baada ya maandamano hayo kuanza kushika kasi, Mahinda alijiuzulu Mei mwaka huu.

Gotabaya, kanali wa zamani wa jeshi, pia alijaza utawala wake na wanajeshi wa zamani.

Ndugu wa Rajapaksa wana deni kubwa la kupanda kwao kisiasa kwa jukumu lao katika kuwashinda waasi wa Kitamil, lakini wakosoaji wanasema hawajafanya chochote kukuza maridhiano na Watamil walio wachache na pia wanawashutumu kwa kuwapendelea Wasinhala wanaowalenga Waislamu.