Treble ya 1999: Mechi tano zilizoisaidia Man Utd kushinda Ligi Kuu, Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakiwa tayari wametwaa taji la Ligi Kuu na Kombe la FA, Manchester City wamebakiza mechi moja kushinda Ligi ya Mabingwa na kutwaa Treble yani ,mataji matatu kwa mpigo msimu mmoja.
Ni timu moja tu ya Uingereza iliyowahi kukamilisha kazi hiyo hapo awali - wapinzani wao wa jiji la Manchester United katika msimu wa 1998-99.
Huku kocha wa Manchester City City Pep Guardiola akitumai kumwiga meneja wa United Sir Alex Ferguson miaka 24 baadaye, BBC Sport inaangalia mechi tano ambazo ziliisaidia United kupata ushindi wa kwanza wa mataji matatu Uingereza.
Arsenal 1-2 Man Utd (marudiano ya nusu fainali ya Kombe la FA)

Jumatano, 14 Aprili 1999
Winga wa Manchester United Ryan Giggs alionyesha mojawapo ya mchezo wa ajabu katika muda wa nyongeza na kuwaweka Mashetani Wekundu kwenye fainali ya Kombe la FA kwa kuwagharimu wapinzani wao Arsenal.
Baada ya kutoka sare katika nusu fainali ya kwanza ya 0-0, pande zote mbili zilirejea Villa Park kwa mechi ya marudiano ya katikati ya juma iliyojaa mvutano.
United walipata bao la kuongoza kupitia kwa David Beckham kabla ya Dennis Bergkamp kusawazisha kipindi cha pili.
Matumaini yoyote ya kupata Treble yalianza kupotea kwa haraka kwa United huku nahodha Roy Keane akitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 74 na Phil Neville akafunga mkwaju wa penalti baada ya muda wa kawaida kumalizika.
Lakini matumaini ya Arsenal yalizima punde penati ya Bergkamp ikiokolewa na Peter Schmeichel, kabla ya Giggs kupata bao la ushindi dakika ya 109 baada ya kuwachenga mabeki kwa kasi ajabu.
Juventus 2-3 Man Utd (Agg: 3-4, Champions League semi-final second leg)

Chanzo cha picha, Getty Images
Wednesday, 21 April 1999
Wiki moja baadaye United waliandaa fainali yao ya pili kwa mtindo wa kusisimua.
Kikosi cha Ferguson kilifungwa 1-1 na Juventus katika mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Uwanja wa Old Trafford, na haraka wakajikuta wakifungwa 2-0 mjini Turin baada ya mabao mawili ya Filippo Inzaghi katika dakika 11 za kwanza.
Nahodha aliyeongeza nguvu Roy Keane, alionyesha ,mojawapo ya uchezaji bora zaidi katika historia ya United.
Raia huyo wa Ireland alifunga kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na David Beckham dakika ya 24 na kuwasisimua mashabiki
Dwight Yorke alisawazisha dakika 10 baadaye na, huku United wakiwa tayari wameshatangulia kwa bao la ugenini, Andy Cole alifunga la tatu katika hatua za mwisho.
Doa pekee kwenye rekodi ya United lilikuwa kadi za njano kwa Keane na Paul Scholes, kumaanisha kwamba wote wawili wangekosa fainali ya Barcelona mwezi mmoja baadaye. Walisonga mbele.
Man Utd 2-1 Tottenham (Premier League final day)

Chanzo cha picha, Getty Images
Sunday, 16 May 1999
Manchester United ilifanikiwa kupata taji lao la tano la Ligi Kuu ya Uingereza katika kipindi cha miaka saba kwa ushindi dhidi ya Tottenham Uwanjani Old Trafford katika siku ya mwisho ya msimu huu.
United walikuwa pointi moja juu ya Arsenal walio nafasi ya pili, wakijua ushindi wakiwa nyumbani dhidi ya Spurs walio katikati ya jedwali ungetosha kutawazwa mabingwa.
Wageni walichukua uongozi wa kushtukiza kupitia kwa Les Ferdinand dakika ya 24, lakini Mashetani Wekundu walisawazisha muda mfupi kabla ya kipindi cha kwanza cha mapumziko kwa shambulio la kujikunja kutoka kwa Beckham.
Cole alifunga bao la ushindi dakika mbili baada ya mchezo kuanza tena, akimlamba kipa Ian Walker na kumaliza kwa ustadi.
United walishikilia taji lao la kwanza katika ardhi ya nyumbani tangu enzi za Sir Matt Busby. Taji la kwanza kati ya matatu lilikuwa limepatikana.
Man Utd 2-0 Newcastle (FA Cup final)

Saturday, 22 May 1999
Wikiendi iliyofuata Manchester United waliwatawala Newcastle United katika fainali ya Kombe la FA na kujihakikishia fursa ya tatu kumiliki kombe la ligi na lile la FA mara mbili miaka ya 1990.
Siku nne kabla ya fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya vijana wa Ferguson walifanikiwa kutwaa taji lao la 10 la Kombe la FA kutokana na mabao ya Teddy Sheringham na Scholes waliotokea Wembley.
Sheringham alichukua nafasi ya Keane aliyeumia katika kipindi cha kwanza na kuiweka United mbele baada ya dakika 11 kufuatia bao moja-mbili na Scholes.
Kiungo huyo wa kati wa Uingereza alimaliza dakika saba za mwisho za kipindi cha pili kwa umahiri
Newcastle hawakutoa majibu mengi na, baada ya kushinda kombe namba mbili, United walielekeza nguvu zao kwa Barcelona haraka.
Man Utd 2-1 Bayern Munich (Champions League final)

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Wednesday, 26 May 1999
Mwishoni mwa Mei 1999 Manchester United ilifikia ahadi yao.
Huku Ligi ya Premia na Kombe la FA tayari zikiwa zimepatikana, United walikamilisha Treble yao ambayo haijawahi kushuhudiwa kwa ushindi ambao hauaminiki kabisa dhidi ya wababe wa Ujerumani Bayern Munich katika fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya huko Nou Camp.
Wakiwakosa Keane na Scholes waliofungiwa, United walisalia nyuma dakika ya sita kwa mpira wa adhabu uliopigwa na Mario Basler.
Bayern, ambao pia nao walikuwa wanapigania kushinda ,mataji matatu kwa mpigo , walikuwa timu bora zaidi usiku, wakigonga mwamba wa goli na lango katika kipindi cha pili lakini hawakuweza kuwaangamiza United.
Na walikuwa wachezaji wawili wa akiba waliowaadhibu baada ya Sheringham kusaidia mpira uliopigwa na Giggs kusawazisha dakika ya 91.
Dakika mbili baadaye Ole Gunnar Solskjaer alifunga bao la pili na kumpa meneja Ferguson taji lake la kwanza la Ligi ya Mabingwa - ndani ya 'Fergie time'.
Hali ya wasiwasi na ya kutisha hadi dakika ya mwisho kabisa, sasa ni zamu ya City kujaribu kufikia mafanikio makubwa zaidi ya wapinzani wao wakubwa.












