Msafara wa Raila Odinga wazuiwa kuingia katikati ya mji wa Nairobi

Msafara wa kiongozi wa Muungano wa Azimio Azimio La Umoja One Kenya Raila Odinga siku ya Jumatatu ulizuiwa kufululiza moja kwa moja hadi katikati ya mji wa Nairobi ili kuongoza maandamano aliyoyataja kuwa ya amani dhidi ya serikali.
Odinga aliyeambatana na naibu wake katika Muungano huo Martha Karua , kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka na kiongozi wa chama cha Roots Party George Wajackoyah, miongoni mwa viongozi wengine wa upinzani alishindwa kukabili vizuizi vilivyowekwa na maafisa wa polisi katika barabara tofauti ili kuingia katikati ya jiji hilo.
Badala yake Raila Odinga alilazimika kupenyeza hadi katika eneo bunge lake la la zamani la Kibra kutoka eneo la kawangware ili kuhutubia umati mkubwa wa watu ulioandamana naye.
Akiwahutbia wakazi hao Raila Odinga alitoa wito kwa serikali kupunguza hali ya juu ya maisha.
Vilevile ametaja kuwa waoga wale waliopanga njama ya kuvamia kampuni yake ya Spectra na shamba la aliyekuwa rais Uhuru Kenyatta.
Aidha naibu wake Martha Karua alionya kuhusu mpango wa serikali wa kutaka kumkamata kiongozi huyo.
Mapema akianzisha maandamano hayo kupitia eneo la Kawangware, maafisa wa polisi waliwarushia vitoa machozi waandamanaji waliokuwa wakibeba matawi ya miti , mabango , sufuria ,na baadhi ya vyakula ili kupinga hali ya juu ya Maisha.
Hatua hiyo ilisababisha hali ya mshikemshike kati ya maafisa wa polisi waliokuwa wakitumia vitoa machozi na maji ya pilipili kuwatawanya waandamanaji hao waliopenyeza na kuingia katika barabara ya kuelekea Ngong kabla ya kukatiza na kuingia katika eneo la Kibera, eneo bunge ambalo kiongozi huyo aliwahi kuwa mbunge wake
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Mamia ya watu wasiojulikana wavamia shamba la Kenyatta
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Awali kabla ya Raila Odinga kuanzisha maandamano yake mamia ya watu wasiojulikana walivamia shamba la familia ya rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta lililopo katika eneo la Kamakis Jiji Nairobi.
Kulingana na walioshuhudia tukio hilo, wavamizi hao walikata miti Kwa kutumia misumeno ya umeme na kuiba mamia ya mifugo kutoka kwa shamba hilo kubwa lililopo nje kidogo ya jiji kuu la Nairobi.
Sehemu kubwa ya ardhi hiyo imetengwa kwa ajili ya mradi wa makazi ya hali ya juu. Hakukuwa na polisi au vikosi vya usalama kwenye eneo hilo . Waandishi wa habari wa eneo hilo wanaoripoti uvamizi huo pia walishambuliwa na umati huo.
Biashara karibu na shamba lote zimefungwa. Kiwanda cha gesi kinachomilikiwa na familia ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga pia kimeharibiwa katika eneo la viwanda la Nairobi.
Maandamano pia yamefanyika katika miji na majiji kote Magharibi mwa Kenya, ngome ya Bw Odinga. Waandamanaji walichoma matairi na kuziba barabara kuu katika jiji la Kisumu.
Muandamanaji mmoja ameuawa katika ghasia hizo.
Wanahabari Wanaoripoti maandamano Kibra washambuliwa na genge lenye visu
Vilevile wandishi wa vyombo vya habari vya humu nchini na kimataifa walishambuliwa na genge la watu wenye visu huko Kibra siku ya Jumatatu walipokuwa wakiangazia maandamano ya kupinga serikali ya kila wiki mara mbili.
Wengine kadhaa walijeruhiwa baada ya genge la watu wenye ghasia kurushia magari yao mawe ndani ya eneo la DO la Kibra.
Kulingana na Citizen Digital, Jase Ndungu, mwandishi wa habari anayeangazia maandamano ya Kibra, genge lililojihami liliwavamia wanahabari waliokuwa wakifuatilia maandamano hayo, na kuwalazimisha kukimbia kuokoa maisha yao.
"Genge hilo lilijifanya kuwa sehemu ya waandamanaji lakini ikawa kweli walikuwa na silaha," Ndung'u aliambia Citizen Digital.
Baadhi ya waandishi wamepoteza simu zao, pochi na vitu vingine vya thamani.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 3
Polisi wazingira mitaa ya Nairobi kudhibiti maandamano Kenya

Mapema leo askari walipiga kambi katika maeneo mbalimbali ya miji ili kutuliza ghasia za maandamano mjini Nairobi, katika jitihada za kuzuia maandamano yaliyoitishwa na upinzani kuhusu gharama ya juu ya maisha na madai ya ukiukwaji wa maadili katika uchaguzi.
Kuna idadi kubwa ya polisi katika Kibera na Mathare - makazi ya mabanda yasiyo rasmi na makubwa zaidi katika jiji - ambapo waandamanaji wanazuiwa kuinga katikati mwa jiji.
Bw Odinga, aliitisha maandamano nchi nzima kuhusu madai kuwa uchaguzi wa mwaka jana uliibiwa.
Pia anasema rais William Ruto ameshindwa kushughulikia gharama ya juu ya maisha nchini.
Raila, aliyekuwa Waziri Mkuu alishindwa na Bw Ruto katika uchaguzi wa Agosti mwaka jana.
Aliungwa mkono na aliyekuwa rais Uhuru Kenyatta.
Tayari maafisa wa polisi wameyataja maandamano hayo kuwa ya haramu licha ya viongozi wa upinzani kudai kwamba haki yao ya kikatiba inawaruhusu kutekeleza wajibu huo.












