Vladimir Putin: Rais wa Urusi 'chupuchupu' kuuawa

Chanzo cha picha, Reuters
Rais wa Urusi Vladimir Putin alinusurika katika jaribio la mauaji muda mfupi baada ya kuanza kwa vita nchini Ukraine, afisa mkuu wa jeshi la Ukraine amesema. Baadhi ya vyombo vya habari vya kimataifa, vikiwemo NDTV na New York Post, vimeripoti habari hiyo leo, vikilinukuu gazeti la Ukraine la Ukrainska Pravda.
Jenerali Kyrylo Budanov, mkuu wa upelelezi wa ulinzi wa Ukraine, amefichua habari kuhusu jaribio la kumuua Putin ambalo halikufaulu. Alisema tukio hilo lilitokea katika eneo la Caucasus.
Habari hizo zinakuja huku kukiwa na mvutano unaoongezeka kati ya Urusi na Ukraine, pamoja na kuongezeka kwa uvumi kuhusu afya ya Putin. Eneo la Caucasus, ambako lilifanyika jaribio la kumuua Putin muda mfupi baada ya kuzuka kwa uhasama nchini Ukraine mnamo Februari 24, liko kati ya Bahari Nyeusi na Bahari ya Caspian.
Taarifa gani hasa zilitolewa na afisa huyu wa upelelezi?
Jenerali Kyrylo Budanov alizungumzia suala hilo katika mahojiano na gazeti la mtandaoni la Ukrainska Pravda.
"Kulikuwa na jaribio la kumuua Putin ... kulingana na maajenti wa Caucasus, si muda mrefu sana uliopita," Bw Budanov alinukuliwa akisema na gazeti la Ukraine.
"Habari hizi hazikuwekwa wazi. Ilikuwa ni kitendo kilichoshindwa kabisa, lakini jaribio hilo lilifanyika kweli ... Ilikuwa takriban miezi miwili iliyopita," aliongeza.

Chanzo cha picha, Reuters
Madai hayo bado hayajathibitishwa na vyanzo huru, lakini habari hizo zinakuja wiki chache baada ya ripoti kuibuka kuwa Bw Putin alifanyiwa upasuaji wa kutoa mafuta kwenye tumbo lake.
Operesheni hiyo "ilifanikiwa sana na hakukuwa na athari", kulingana na ripoti hiyo. Taarifa kuhusu upasuaji wa Putin zilichapishwa kwenye kituo cha Telegram cha SVR, ambacho kinashirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi.
Kulikuwa na taarifa nyingine kutoka kwa mfanyabiashara tajiri ambaye ni rafiki wa karibu wa Putin, ambaye alisema kuwa "Putin anaumwa sana na saratani ya damu".

Chanzo cha picha, Reuters
Mapema mwezi huu, Bw Budanov, katika mahojiano na Sky News, alisema vita vya Ukraine vitakuwa na awamu mpya katikati ya Agosti na vitamalizika mwishoni mwa mwaka, na kusababisha mabadiliko ya utawala nchini Urusi.
Pia alisema kuwa "mapinduzi ya kijeshi" yalikuwa yanaendelea na kwamba hii haiwezi kusitishwa.
"Putin hawezi tena kushikilia wadhifa huo"
Rais wa Marekani tayari ametoa kauli baada ya kusema "Putin hastahili kusalia madarakani".
Mwezi Machi, Rais wa Marekani Joe Biden alitoa kauli kadhaa ambazo hazikuandikwa ambazo ziliongeza mkazo katika uhusiano kati ya Marekani na Urusi, ambao tayari ulikuwa na matatizo.
Hata hivyo, nukuu ambayo haikutajwa jina kutoka kwa "hotuba yake kubwa" huko Poland - katika kile kilichoonekana kuwa wito wa kuangushwa kwa Rais Vladimir Putin - inaweza kuwa ya nguvu zaidi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika hotuba yake kwa kundi la maafisa waliochaguliwa wa serikali ya Poland na wageni wa heshima katika Ikulu ya Kifalme huko Warsaw, rais wa Marekani alikaririwa kwamba kuna vita vinavyoendelea kati ya demokrasia na wanaopinga demokrasia, ambayo alionya vikali dhidi yake.
Aliapa kwamba muungano wa Nato utatetea "kila inchi" ya eneo la nchi wanachama wake. Pia aliahidi kuendelea kuiunga mkono Ukraine, ingawa alisisitiza kuwa jeshi la Marekani halitaingia vitani na Urusi.
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Ilikuwa ni hotuba kali - na inalingana sana na kile ambacho kimesemwa kwa miezi kadhaa na maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani wakiongozwa na Antony Blinken.
Lakini, muda mfupi kabla ya kuhitimisha hotuba yake na kusema "asante" na "amani", Bw Biden baadaye alinukuu matamshi ambayo hayakutajwa jina akiyaelekeza kwa mwenzake wa Urusi: "Kwa ajili ya Mungu, mtu huyu hatasalia mamlakani."
Serikali ya Urusi na yenyewe ikajibu mara moja.
"Hotuba hii ni kejeli kuhusu Urusi ilipaswa kutolewa kwa kufuata maadili," msemaji wa Urusi Dmitry Peskov alisema. "Sielewi kwamba ulimwengu haujaunganishwa na Marekani na nchi nyingi za Ulaya."












