Pep Guardiola: Ni bingwa wa rekodi katika soka la England

Pep

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakati Etihad iliripuka katika sherehe za ubingwa katika siku ya mwisho ya ligi, uso wa Pep Guardiola ulibubujikwa na machozi aliyotiririka mashavuni mwake.

Magoli matatu ya dakika 15 za mwisho yalitosha kuipa ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Aston Villa na kuipa Manchester City ubingwa wa Ligi Kuu, EPL.

Katika wiki chache zijazo, hata hivyo, kabla ya msimu mwingine kuanza, Guardiola anaweza kujipa muda kutafakari juu ya mafanikio yote ambayo ameyapata wakati wake katika Ligi Kuu ya England. Pep ni gwiji wa kuvunja rekodi.

Utawala wa kuvunja rekodi

City ina pointi 93 ikiwa ni alama kubwa katika nafasi ya nne katika historia ya Ligi Kuu ya England. Hata hivyo, ni mara ya tatu kwa City kupata alama nyingi wakati wa utawala wa Guardiola.

BBC

Guardiola amekuwa mashine ya kuvunja rekodi wakati akiwa England:

Msimu wa 2017-18

Alama alama nyingi zaidi (100), magoli (106) na tofauti kubwa ya lmabao katika msimu (+79)

Tofauti kubwa ya alama kati ya mshindi na aliyeshika nafasi a pili (alama 19 mbele ya Manchester United iliyoshika nafasi ya pili)

Kushinda mechi nyingi zaidi (mechi 32) na ushindi mfululizo (michezo 18) - akiwa sawa na Liverpool (2019-20).

Kushinda mechi nyingi ugenini zaidi ya mechi (16)

Msimu wa 2018-19

  • Kushinda mechi nyingi nyumbani (18) - kama walivyofanya katika msimu wa 2011-12 side, Chelsea (2005-06), Man Utd (2010-11) na Liverpool (2019-20)

Msimu wa 2020-21

  • Ushindi mfululizo (21) na kushinda mechi nyingi za ugenini (12)
  • Kucheza mechi nyingi bila ya kutanguliwa kufungwa (19)
Pep
Maelezo ya picha, Guardiola (kushoto) na kocha wa Liverpool Jurgen Klopp (kulia) ambaye amekuwa mpinzani wake katika misimu ya hivi karibuni

Mwaka 2021 kikosi cha Guardiola kilishinda michezo 36 ya ligi katika kalenda ya mwaka, kikiipiku rekodi ya kushinda michezo 33 iliyowekwa na kikosi cha Bob Paisley cha Liverpool mwaka 1982. City pia iliweka rekodi ya kushinda michezo ya ugenini 19 katika kipindi hicho cha miezi 12.

Katika msimu huu, Guardiola amekuwa meneja wa kwanza kufikisha alama 500 katika michezo 213 games, ambayo ni 18 pungufu ya rekodi iliyowekwa awali na Jose Mourinho.

Guardiola ni meneja wa nne katika historia ya ligi kuu England kushinda mataji manne katika misimu mitano, wengine ni George Ramsey (Aston Villa), Bob Paisley (Liverpool) na Alex Ferguson (Man Utd).

Magoli, Mashuti na pasi ni Pep na City yake

BBC
Maelezo ya picha, Manchester City ina uwiano mzuri wa magoli kwa mchezo

Haishangazwi kuona kwamba City imekuwa timu yenye kupiga mashuti mengi zaidi kuliko timu yoyote katika kipindi cha Guardiola kwenye ligi kuu England (4,038), huku Liverpool ikiwa nafasi ya pili kwa mashuti 3,781. City pia mefunga mabao mengi zaidi.

City pia imegongesha mwamba mara nyingi zaidi , mara 135 katika misimu 6 iliyopita, ikifuatiwa na Chelsea, ambayo mashuti yake 97 yaligonga mwamba.

Kwenye kumiliki mpira City ya Guardiola ni habari nyingine, katika misimu 6 imemiliki mpira 67% katika kipindi hicho ikipiga pasi 155,639 ikiwa ni pasi 15,000 zaidi ya timu nyingine inayofuata.

Sterling ndiye kinara wa mabao kwenye ligi chini ya Guardiola akipachika mabao 85, matau zaidi ya Aguero, huku Gabriel Jesus akifuatia kwa mabao 58.

Kevin De Bruyne tanaongoza kwa kupiga pasi za mabao akipiga pasi 77, ambazo ni 23 zaidi ya anayemfuatia, Sterling.

Inaelezwa pia kocha huyu ametumia pesa nyingi zaidi karibu £900m tangu mwaka 2016- kiasi ambacho kitafikia karibu £1bn kwa ujio mshambuliaji mpya Erling Haaland kutoka Dortmund.