Gereza la Cooma: Gereza lililowahi kuwa la wafungwa wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia

Cooma jail

Chanzo cha picha, The Greatest Menace

Maelezo ya picha, Gereza la Cooma

Iko katika moja ya miji midogo yenye baridi na yenye upepo zaidi nchini Australia, gereza la Cooma lina siri kubwa nyuma ya pazia. Si tu kwamba ilifunguliwa tena 1957 kwa madhumuni maalum ya kuwafunga wanaume waliokutwa na; "makosa ya vitendo vya mapenzi ya jinsia moja", pia ilisemekana kutumika kama kipimo cha binadamu na lengo kubwa la mwisho la kukomesha mapenzi ya jinsia moja kwenye jamii.

Gereza la Cooma linaaminika kuwa gereza pekee la wapenzi wa jinsia moja duniani, kwa mujibu wa podcast mpya. Hadi sasa, hata baadhi ya wafanyakazi wa gereza hilo wanasema hawakujua sababu halisi ya wafungwa wa jinsia moja kutengwa huko.

Les Strzelecki, mwenye umri wa miaka 66, alianza kazi kama afisa wa huduma za uangalizi katika gereza hilo mwaka 1979, na baadaye kuanzisha Makumbusho ya Huduma za Marekebisho huko Cooma. Anaamini wafungwa walipelekwa huko kwa ajili ya usalama wao wenyewe.

"Cooma ilikuwa taasisi ya ulinzi"; anaiambia BBC. "Walikuwa katika hatari ya kufanyiwa vurugu katika magereza makubwa kama Long Bay [katika Sydney]". Lakini mfanyakazi mwingine wa zamani, Cliff New, anadai kuwa ilikuwa kwa sababu za huruma. Aliiambia podcast ya The Greatest Menace kwamba wanasaikolojia na wataalamu wa magonjwa ya akili walikuwa "wanakuja wakati wote" baada ya jela kufunguliwa tena mnamo 1957.

Alielewa hatua hiyo ilikuwa kama majaribio ya kuwabadilisha: "Walikuwa wakijaribu kuwarejesha kwenye njia sahihi... Walidhani kuwa wanaweza kuwaponya". Pia wafungwa walikuwa wanaweka kila mmoja kwenye selo yake, alisema. "Huwezi kuwaweka wawili kwa pamoja... hiyo ilikuwa moja ya matatizo yetu makubwa - kuwaangalia", anasema Bwana New, ambaye sasa ana umri wa miaka 94.

Les Strzelecki

Chanzo cha picha, Thomas McCoy

Maelezo ya picha, Les Strzelecki (kushoto) awali alifanya kazi magerezakabla ya kuanzisha makumbusho ya huduma za kurekebisha tabia

Nyaraka za kihistoria zinaonyesha Waziri wa Sheria wa New South Wales (NSW) Reg Downing ndiye aliyeanzisha gereza hilo.

Aliripotiwa kuelezea "ufahari"; wa hatua hiyo, akiambia gazeti la Sydney Morning Herald mwaka 1957:

"Hakuna mahali popote Ulaya au Amerika utakuta gereza lolote ambalo wapenzi wa jinsia moja wametenganishwa na wafungwa wengine".

Reg Downing

Chanzo cha picha, State Library of NSW

Maelezo ya picha, Reg Downing alionyesha matamanio yake ya kuwatenganisha wafungwa wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja na wale wa kawaida

Haijulikani ni lini wafungwa wa jinsia moja waliachwa kupelekwa tena huko Cooma. "Nyaraka nyingi ziliondolewa au kuharibiwa", Bwana Wotherspoon anasema. Idara maalumu a huduma za kurekebishatabia na mwenendo na ile ya Jamii na Haki walikataa kutoa maoni juu ya madai haya, wakigusia "asili yao ya kihistoria".

Bwana Abboud anaamini kuwa wafungwa wa jinsia moja huenda walipelekwa huko hadi mwanzoni mwa miaka ya 1980, akinukuu taarifa ya mwaka 1982 kutoka kwa waziri wa huduma za kurekebisha tabia akidai kuwa sera hiyo bado ipo mpaka sasa.

Cooma

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Cooma ni mji wenye watu wapatao 7,000

Wahalifu wa ngono pia walipelekwa Cooma na kuongeza wafungwa hawa wa jinsia moja walionyanyapaliwa zaidi, anasema Bw. Abboud. Bwana Wotherspoon anasema, huku mjadala wa hivi karibuni wa bunge kuhusu muswada wa ubaguzi wa kidini ukitishia kuruhusu ubaguzi kwa misingi ya mwelekeo wa kijinsia, historia ya hivi karibuni inabeba onyo kali. "Suluhu ya kudumu ni muhimu ili kuhakikisha haturudi nyuma", Bwana Wotherspoon.