Lishe: Je, vyakula vinavyohitaji kutafuna zaidi vinasaidia kupunguza uzani wa mwili wako?

Une femme en sourire tenant une assiette

Utafiti umebaini kuwa vyakula visivyo vilaini kama vile kufikiria kula tufaha badala ya kunywa juisi yake kunaweza kupunguza njaa kwa kiasi kikubwa na kujihisi kuwa umeshiba, ukilinganisha na vyakula vya majimaji .

Tulizungumza na waandishi wa utafiti na wataalamu wengine ili kujua namna ya kuchagua chakula kunavyoweza kusaidia kupunguza uzito.

Nini kinachotufanya kuhisi kuwa tumeshiba?

Akifafanua jinsi muonekano wa kitu ulivyo na ushawishi katika hisia zetu ya kujihisi kuwa tumeshiba, Helena Gibson-Moore kutoka taasisi ya Lishe ya Uingereza -British Nutrition Foundation amesema:

"Hisia za kujihisi kushiba au kusikia njaa huwa inatokea baada ya mlo ... hutokea kwa ishara zinazoonekana na mwilini ambazo uanza wakati wa kula chakula au kunywa na kuendelea wakati wa kutafunwa, muonekano wake na hata harufu yake. "

Utafiti unasema nini juu ya hili ?

Profesa Anwesha Sarkar wa chuo kikuu cha Leeds amefanya utafiti awali kwa kufafanua kuhusu vigezo vinavyoangazia uhusiano wa muonekano wa chakula na hisia ya kujihisi kushiba.

Une table bien garnie de nourritures

Katika utafiti wa watu 23, washiriki walihojiwa kuhusu namna ambavyo wanakula na utofauti wa muonekano wake mfano kuku akiwa amepikwa katika upishi tofauti tofauti au aina tofauti ya vipande vya kuku .

Wanahisi kuwa matokeo yataonesha namna ambavyo "muonekano wa chakula ndio utakaompa mtu hamu ya kula kuongezeka au kupungua , na kuridhika." Na haya ndio waliyoyabaini katika utafiti wao?

Une femme préparant un jus de fruits ou de légumes

Jinsi itakavyoweza kusaidia watu wanaohitaji kupunguza uzito ?

Matokeo ya utafiti wao yalitabiri kuwa vyakula vyenye muonekano wa ugumu huwa vinawapa watu hamu ya kula na kupunguza njaa kwa kasi kwa kumfanya mtu ashibe haraka ukilinganisha na vyakula vya vimiminika." Na je hicho ndicho walichokipata?

Dkt Keri McCrickerd, mtafiti mkuu wa taasisi ya tiba na sayansi wa Singapore Institute of Clinical Sciences (SICS) na shirika la sayansi na teknolojia la A * STAR, ambaye alifanya utafiti wake mwenyewe na kuelezea namna ambavyo utafiti huu unaweza kutumika kupanga mlo kamili wa mtu kujihisi kuwa ameshiba kwa muda mrefu.

"Tumebaini kuwa watu wako makini sana katika kubadili muonekano wa chakula na kinywaji.Hata mabadiliko ya uzuri wa chakula, kama vile ujazo wa chakula, uwezo wa kutafuna ,utamu wa chakula kunaweza kubadili kiwango cha mtu kula chakula fulani au kunywa kulingana na mtu, alisema.

Une variété de boissons présentées dans des verres

"Suala la muhimu zaidi ni kuwa tumebaini matarajio mengi yanatokana na mabadiliko ya muonekano wa chakula au muundo wa chakula kuwa na athari kubwa, kwa mambo kama ya kipimo cha chakula wakati wa kumuhudumia mtu.

Kuna watu ambao wanachagua chakula kulingana na ujazo, wengine wanapenda kula chakula kidogo na wengine kingi, wengine kigumu, wengine kilani ndio anaridhika. "

Hivyo aina ya chakula ndio inamfanya mtu kujisikia kushiba kwa muda mrefu au la ? "Inawez kuwa vigumu kuangazia aina ya viungo vilivyotumika kupika chakula fulani," anasema Sarkar na Stribitcaia.

"Tunaweza kusema vyakula vigumu kama vile vilivyochemshwa ndio vinaweza kumfanya mtu kujisikia kushiba kwa muda mrefu zaidi, kutokana na mtazamo wa muundo, lakini utafiti zaidi unahitajika na ndio ambao tunafanyia kazi sasa"

Je kuna baadhi ya virutubishi ambavyo hutufanya kuhisi tumeshiba kwa muda mrefu?

Kula chakula ili ushibe sio tu suala la ni chakula cha aina gani . Protini ndio inayofanya kazi ya kutufanya tushibe na Gibson More anaelezea kwamba chakula chenye nyuzi nyuzi nyingi pia kinaweza kumfanya mtu kuhisi kushiba.

Kwa mfano, kushirikisha vyakula vyenye protini kama vile , maharage, mayai, samaki, na kuku {bila ngozi yake} na vyakula vyenye nyuzi nyuzi kama vile mkate, maharage matunda na mboga , hutusaidia kuondoa hisia ya njaa hadi chakula kinachofuatia.

Je ni kitu tulichoweka akilini mwetu?

''Inategemea zaidi na athari za kimetaboliki za virutubisho kwenye utumbo, na saikolojia ina jukumu," anasema Gibson-Moore.

Ni vigumu kubaini hisia kamili ya chanzo cha kuhisi shibe , kwasababu ya athari za kifiziolokia na Saikolojia ya kula chakula cha aina fulani.

Pamoja na muundo wa aina ya chakula, kitu muhimu ni muda anaochukua mtu kukitafuna. Kwa jumla chakula kigumu huchukua muda mrefu kutafuna mdomoni kabla ya kuchanganywa na mate na kumezwa.

Chakula chepesi nacho huchukuwa muda mfupi kutafuna na kumeza.

Chakula kinapochukua muda mrefu kutafunwa mdomono ndiposa kinazidi kutuma ujumbe na kuchochea hisia ya kushiba.

Utambuzi huo ni muhimu sana. Mtafiti huyo hatahivyo angependelea kusema kwamba hawajafanyia utafiti suala hili.

''Ufungaji wa chakula pia unaweza kutushawishi kuhisi shibe,'' anasema McCrckerd.

"Uwekaji lebo ya bidhaa, ladha, umbile, na ukubwa vyote vinaweza kuathiri matarajio yetu ya jinsi chakula au kinywaji kinavyoridhisha, na tunapoamini kuwa ni kingi zaidi, tuna uwezekano mkubwa wa kuchagua sehemu ndogo au kuhisi kushiba zaidi baada ya kula, "anasema.

Je, unapaswa kununua vyakula muhimu zaidi?

Kabla ya kubadilisha orodha yako ya ununuzi wa chakula ili kujumuisha vyakula vilivyo na protini, tahadhari kidogo: Utafiti zaidi bado unahitajika.

"Bado haijulikani ikiwa kubadilisha muundo wa vyakula tunavyokula kutakuwa na athari kubwa kwa tabia zetu za ulaji au uzani wetu kwa wakati," anasema McCrickerd.

"Utafiti mwingi hadi sasa umetoka kwa tafiti ndogo, za muda mfupi ambazo zimebadilisha muundo wa chakula na kuangalia kuona jinsi tabia za watu za ulaji huathiriwa wakati wa mlo.

Tafiti za muda mrefu zinahitajika ili kubaini jinsi athari za vyakula vilivyotafunwa kwa muda mrefu zinavyodumu baada ya siku na wiki kadhaa za matumizi.