Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Fahamu ushindani uliopo kati ya Marekani, Urusi na China katika uundaji wa silaha za Hypersonic
Ni silaha zenye kasi kubwa na zinauwezo wa kuvunja mfumo wowote wa ulinzi ulipo sasa. Zinaitwa silaha za hypersonic weapons, silaha za zamani za vita baridi ambazo zilikuwa vinywaji vya watu wakati huo, lakini siku hizi, zinaonekana kurejeana kuwa jambo la ukweli badala ya matamanio.
Serikali ya China imetangaza wiki hii kwamba ilijaribu silaha yake aina ya Starry Sky-2 kwa mara ya kwanza, kifaa ambacho kinaruka, kwa mujibu wa wa mamlakaza Beijing authorities, zinauwezo wa kazi ya kilometa 7,344 kwa saa. Hiyo maana yake ni mara sita ya kasi ya sauti.
Ata hivyo sio silaha za kwanza. Urusi nayo ilitangaza mwezi uliopita kwamba silaha zake ya MiG-31 zimekuwa zikirandaranda kwenye eneo la bahari Caspian tangu mwezi Aprilizikiwa na kombora jipya la hypersonic, 'Kinjal. Wizara ya Uinzi ya Urusi iliuhakikishia uma kwamba punde tu silaha yake ya Avangard itakuwa tayari, mfumo wa kombora kwamba linauwezo wa kuvuka bara moja kwenda linguine kwa kasi ya hypersonic ya kilometa 24,140 kwa saa.
Mwaka 2015, Marekani ilitangaza kwamba lengo lake ni kutengeneza silaha ya hypersonic ifikapo mwaka 2023. Kitengo maalumu cha makombora cha Marekani kiliomba bajeti ya dola $ 120 million mwaka 2019 kwa ajili ya kutengeza kombora la hypersonic kwa ajili ya ulinzi.
Mwaka 2016, Ofisi hiyo iliomba dola $ 75 million kwa lengo hilo hilo kwa ajili yam waka huu. Marekani ilianza kusaka silaha za hypersonic miongo kadhaa iliyopit, kabala ya kufatiwa na Urusi na baadae China.
Hypersonic ni silaha za namna gani?
James Acton, Mkurugenzi mwenza wa mpango wa sera za nyuklia huko Washington ameiambia BBC kwamba silaha hizo zeye kasi ya kilometa 1,235 kwa saa:
"Kinadharia, zinaweza kwenda mara 5,10 au hata 20 ya kasi ya sati," anasema mtaalam huyo.
George Nacouzi, mtaalamu wa silaha za hypersonic kutoka Rand Corporation, anasema kuna aina mbili za silaha za hypersonic
1: Hypersonic Displacement Vehicles (HGVs), ambazo hutumwa angani, kufikia miinuko ya juu na kisha kuingia tena eneo lengwa kwa njia zisizo za kawaida.
2: Makombora ya Hypersonic cruise (HCM), ambayo kimsingi ni aina ya makombora ambayo yana mfumo wa kusongesha ambao huvunja vizuizi vya sauti mara kwa mara.
Yote yanaweza kusafiri kwa kasi ya zaidi ya kilomita 6,115 kwa saa. Kwa mujibu wa Acton, utengenezaji wake umekuwa ukitarajiwa tangu Vita Baridi, lakini maendeleo yake yamekabiliwa na changamoto kadhaa za kiteknolojia.
Kazi na majukumu mapya
Acton anakubaliana kwamba nchi tatu za Marekani, Urusi na China ziko kwenye mbio ndefu za kumtafuta ni nani atakayekuwa wa kwanza kuja na silaha hizi kwa ufanisi.
"Wanakuja na teknolojia, na kuwekeza mamilioni ya fedha, kwa hivyo maendeleo yake ni kama mbio mpya za kijeshi," anasema.
Ameongeza kuwa China imekuwa ikivutiwa sana na roketi, Urusi yenyewe imejielekeza kwenye silaha aina ya 'gliders', ngawa kwa mujibu wa Moscow itatambulisha silaha yake mpya nyingine ya masafa marefu mwakani inayoitwa ICM.
Nacouzi anagusia kwamba, kwa upande wa Marekani wataaalam wamekuwa wakishughulikia kwa miaka zaidi ya 30, lakini hawajafanikiwa hasa kuja na teknolojia, kutokana na gharama kubwa na sababu zingine. Hata hivyo Waziri wa Uinzi wa Marekani James Mattis, alisema mwezi Aprili kwamba silaha za hypersonic na mifumo ya ulinzi ilikuwa " kipaumbele namba moja" kwa ajili ya uchunguzi na maendeleo ya kijeshi ya taifa hilo.
"Ushahidi uliopo ni kwamba Marekani inaendelea kuwa kinara kwa aija hiyo ya teknolojia," anasema Acton.
Tishio jipya la kinyukila
Wadadisi wanasema chagamoto iliyopo sasa sio kwenye kutengeneza aina hii ya silaha, lakini "Silaha hizi hazijawa kwa kiwango kikubwa bado. Kwa upande wangu , hatua kuwa itakua kama, kwa upande mwingine, Urusi au China wataweza kuja na silaha ya nyuklia ya masafa marefu zaidi," anasema.
Kulingana na mtaalamu huyo, Urusi na Uchina zinaonekana kuzingatia kuweka silaha zao za hypersonic kuzihusianisha na vichwa vya mabomu ya atomiki, wakati Merekani yenyewe inataka kuhusisha zaidi na silaha za kawai
"Ama uzipe uwezo wa kinyuklia ama la, ukweli ni kwamba, kwa mtazamo wa kiusalama, madhara ama hatari yake itakuwa kubwa, "liongeza.
Yote yakiwa mezani, watalaam wanasema hawana shaka kwamba silaha za hypersonic zitakuwa chanzo cha vitosho ama vita katika siku za usoni.da.