Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ufyatuaji wa silaha ya hypersonic ya China walitia wasiwasi jeshi la Marekani
Mwenyekiti wa majeshi ya Marekani Mark Milley alisema katika mahojiano na kitengo cha habari cha Bloomberg kwamba jeshi la China linapanuka kwa kasi.
Gazeti la Financial Times lilirippti mwezi huu kwamba jaribio hilo lilishangaza jeshi la Marekani. Hatahivyo Bejing imekana kufanya jaribio lolote la silaha na badala yake kusema kwamba kilikuwa chombo cha angani.
'Kile tulichokiona ulikuwa ni mfumo wa silaha ya Hypersonic . na inatia wasiwasi sana' , Jenerali Milley aliambia Bloomberg siku ya Jumatano.
'Sijui iwapo ni wakati wa Sputnik , lakini nadhani inakaribia wakati huo . Tunasikiliza'.
Matamshi yake ndio utambuzi wa kwanza rasmi wa Marekani kwamba China ilifanya majaribio mawili ya silaha wakati wa majira ya joto.
Ripoti zinasema kwamba ilikuwa silaha ya kinyuklia inayoweza kukwepa mifumo ya ulinzi ilio angani ya Marekani.
Urushaji angani wa setlaiti ya Usovieti ya Sputnik mwaka 1957 uliishangaza Marekani , ambayo ilihofia kwamba Usovieti ilikuwa imepiga hatua ya kuwa na uwezo mkubwa wa kiteknolojia.
Hatua hiyo ilimshinikiza rais John F Kennedy kutangaza kwamba Marekani itawapeleka watu mwezini , lengo lililoafikiwa chini ya muongo mmoja.
Msemaji wa Pentagon John Kirby alikataa kuzungumzia kuhusu matamshi ya jenerali huyo katika hotuba yake siku ya Jumatano akisema: hii sio teknolojia ambayo ni geni kwetu , ambayo hatujaifikiria kwa muda.
Aliongezea kwamba Marekani inafanya kazi kuimarisha mifumo ya ulinzi na kutafuta uwezo wake wa silaha za Hypersonic.
Silaha za hypersonic zina uwezo wa kusafiri mara tano zaidi ya kasi ya sauti. Zinatajwa kuwa na uwezo mkubwa wa kwenda mbali pamoja na kukwepa mifumo ya ulinzi angani.Jenerali mkuu nchini Marekani amesema kwamba China inatuhumu kwamba jaribio la silaha yake ya aina ya hypersonic linakaribia wakati wa silaha ya Sputnik , akielezea uzinduzi wa setlaiti uliosababisha vita baridi kuhusu ushindani wa silaha .
Wiki iliopita Marekani ilifanya jaribio la silaha tatu aina ya hypersonic , kutoka katika kituo cha Nasa mjini Virginia
Majaribio hayo yatatumika kuelezea hatua zitakazopigwa katika uundaji wa silaha mpya aina ya hypersonic , maafisa wa Marekani walisema katika taarifa.
Jenerali Milley pia alionya kwamba jeshi la China limeimarika kutoka kikosi kidogo hadi jeshi kubwa lenye uwezo katika kila kitengo na lina hamu ya kujiimarisha ulimwenguni.
Kulingana na CNN, mkurugenzi wa CIA Bill Burns alielezea China wiki iliopita kama tishio kubwa la kiteknolojia kwa Marekani .
Mapema mwezi huu , alisema kwamba shirika hilo la upepelezi litaimarisha juhudi zake dhidi ya China.
Ikulu ya rais ya Joe Biden imesema kwamba uhusiano kati ya China na Marekani ni ule wa ushindani wa kimkakati.
Jenerali Milley mwezi uliopita alikabiliwa na wito wa kujiuzulu na kushtumiwa kwa tabia za uhaini baada ya kuripotiwa kwamba aliwahakikishia wenzake wa China katika siku za mwisho za utawala wa rais Trump kwamba Marekani haitafanya shambuli lolote la kinyuklia.
Mwenyekiti huyo wa majeshi yote baadaye alisema kwamba wito huo ulitokana na kazi na majukumu yake..