Inawezekana vinyesi kudondoka kutoka kwenye ndege? na kuna uwezekano gani wa vinyesi hivyo kutumwagikia?

An aeroplane lands in a beautiful sunset

Chanzo cha picha, Getty Images

Waingereza huwa na wasiwasi wa hali ya hewa, lakini mtu mmoja kutoka Berkshire, magharibi mwa London, amekuwa na sababu maalum ya wasiwasi juu ya mbingu zilizo juu yake. Alikuwa amepumzika katika bustani yake pale "alipondokewa na 'kinyesi', kutoka kwenye ndege.

Ilitokea katikati ya Julai, lakini imejitokeza sasa kufuatia mkutano wa baraza.

Akizungumza kwenye jukwaa la masuala ya anga, Kansela Karen Davies alisema aliwasiliana na mpiga kura mmoja na "kuogopa" kusikia tukio hilo "baya".

Alielezea jinsi "bustani yake yote, na miavuli ya bustani, na yeye wote walikuwa wamefunikwa" na kinyesi.

Kwa hivyo hii ilitokeaje, na je! Sisi sote tunahitaji kutazama angani?

Nini kilitokea?

Windsor

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ndege zinazotrua kwenye uwanja wa ndege wa Heathrow kawaida hupita juu ya eneo la Windsor

Mtu huyo anaishi Windsor, mji maarufu uliopo kasri la Malkia, na pia njia ya kuelekea Heathrow, uwanja mkubwa zaidi kati ya viwanja vya ndege vitano vinavyohudumia London.

"Najua visa kadhaa vinatokea kila mwaka na maji taka yaliyohifadhiwa kutoka kwa ndege," Bi Davies alisema, "lakini maji taka haya hayakuhifadhiwa na bustani yake yote ilikuwa imejaa kinyesi."

"Alikuwa nje kwenye bustani yake wakati huo, kwa hivyo ni jambo la kutisha, la kutisha. Tunatumai kuwa haliwezi kutokea tena kwa mkaz wetu yoyote," aliongeza.

Diwani mwingine wa baraza hilo, John Bowden, aliikiita kitendo hicho "kimoja kati ya bilioni moja".

Alipendekeza hali ya hewa ya joto ilimaanisha kuwa kinyesi kinaweza "kutoka kama kitu safi zaidi".

Hili linatokeaje?

Vyoo vya ndege uhifadhi taka za binadamu katika matanki maalum, ambayo kawaida hutolewa kila baada ya ndege kutua.

Lakini mamlaka ya kimataifa ya anga inakubali kuwa uvujaji mkubwa unaweza kutokea angani.

BBC ilizungumza na mtaalam wa anga Julian Bray juu ya jinsi maji machafu kama hayo yangeweza kutokea.

"Ndege za kisasa zina choo chenye eneo kubwa la wazi, hivyo ziko salama sana na zimefungwa vizuri. Tatizo ni kwenye maungio kati ya choo kinachotumiwa na tanki la kuhifadhi," Bray alisema.

"Lakini kamwe haiwezi kuwa imeunganika kwa asilimia 100% kwani lazima kuwe na upenyo kidogo kwasababu ndege inapitia viwango tofauti vya shinikizo na hali ya hewa."

"Kinachoonekana kutokea hapa ni kwamba inataka kutua ardhini, hali ya hewa inabadilika na kunakuwa na mabadiliko ya msikumo. Maji taka yanavuja na kwa bahati mbaya yanamkuta muungwana bustanini bila kusahau miavuli yake miwili. "

Kwa namna gani jambo hili ni kawaida?

An aeroplane toilet showing blue disinfectant

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Bonge la taka za binadamu ' ambalo hudondoka kutoka kwenye ndege ikiwa angani linaitwa "barafu ya blue" kwa sababu ina mchanganyiko wa taka za binadamu nadawa za bakteria.

"Ni tukio la nadra sana. Ilikuwa ikitokea sana katika siku za zamani na kitu hiki kinachoitwa barafu ya bluu ilikuwa kawaida kutokea, "Bray alisema.

Ilipewa jina la barafu ya bluu kuliko rangi nyingine yoyote kwa sababu ni mchanganyiko wa haja ndogo na kemikali ya kuua wadudu, alifafanua.

"Huwa inatokea - sio mara kwa mara, lakini huwa inatokea kweli. Huwa inadondoka kama donge la barafu. Siyo ya kupendeza sana," aliongeza.

Mtu mmoja ambaye aliwahi kushuhudia barafu ya blue ikidondoka- Paul kutoka Iver - anaelezea uzoefu wake alipozungumza ana BBC.

"Nilikuwa natoka hospitali ya Malkia Margaret , ndege ya shirika la ndege ya Canada ilikua inapita juu karibu kabisa ikiwa inaenda kutua uwanja wa Heathrow," Paul alielezea, "na baadhi ya barafu ya chooni ilidondoka na kudondokea kwenye matawi mawili ya mti, uliokuwa mita kama 3.6 mbele yangu."

Paul anaiona kama mtu mwenye bahati kuendelea kuwa salama na hai, na anadhani mkazi mwenzake wa Berkshire anapaswa pia kujiona ni mtu mwenye bahati.

Mamlaka za ndege nchini Uingereza ziliambia BBC mwaka 2016 kwamba karibu madonge ya barafu ya bluu 25 hudondoka kila mwaka kwenye anga la Uingereza, lakini hilo linatokea kila mahali.

Donge la barafu lililodondoka kwenye kijiji kimoja kaskazini mwa jimbo la Haryana nchini India mwezi Januari, 2018 linadhaniwa ni kinyesi cha binadamu kilichoganda, ambacho kilidondoshwa na ndege

'Kinyesi' hicho kilidondoka kwenye kijiji cha Fazilpur Badli na kilikuwa na uzito wa kati ya kilo 10-12.

The 10-12kg

Chanzo cha picha, GURGAON POLICE

Maelezo ya picha, Kilo kati ya 10-12kg ya barafu 'kinyesi' iliyodondoka katika kijiji cha Fazilpur Badli, Kaskaizni mwa India

Mmoja wa maafisa waandamizi aliambia BBC baadhi ya wanakijii walidhani ni kitu kilichotoka kwenye sayari nyingine ama anga za mbali. "Nilielezwa walichukua sampuli," alisema.

'Kulipwa fidia'

Mmoja wa wakazi wa eneo hilo karibu na uwanja wa ndege, Andrew Hall, ambaye alikuwepo akifuatilia mkutano wa baraza kupitia mtandao , alisema mtu huyo mwenye bahati mbayea aliyedondokewa na kinyesi cha kwenye ndege anapaswa kulipwa fidia.who was present at the virtual council meeting, said the unfortunate man would be right to seek substantial compensation.

"Mkampuni ya maji yanapigwa faini za mamilioni ya fedha yakichepusha maji taka kwenye mito," alisema, na "wakati ndege ikidondosha vinyesi kwenye viwchwa vya watu, kusema ukweli, nadhani hii ni mbaya zaidi,."

One plane flies

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kawaida kwa sasa ndege hufuatana kwa kutua kwa foleni - hapa ndege moja inaruka kupitia msukosuko unaosababishwa na ule wa mbele

lakini kwa upande wake Davies anasema mkazi huyo ameamua kutotaka kulipwa fidia. "Hatafanya hivyo kwa sababu ya kuharibiwa kwa miamvuli kadhaa bustanini," alisema.

BBC iliwasiliana na mamlaka za anga Uingereza kuzungumzia hili, lakini haikupata majibu kwa siku kadhaa