Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 03.05.2021: Neymar, Abraham, Kane, Grealish, Keita, Alaba

Chanzo cha picha, Getty Images
Mkurugenzi wa michezo wa Paris St-Germain Leonardo haonekani kushawishika kuwa mshambuliaji wa Brazil Neymar,29, atasaini nyongeza ya mkataba na klabu hiyo ya Ufaransa. (Marca)
Meneja wa West Ham David Moyes amesema timu yake itaingia sokoni kumsaka mshambuliaji katika dirisha lijalo la usajili, lakini hawatamuwania Muingereza Tammy Abraham ,23 kama bei yake itasalia kuwa £45m. (Football London)
Manchester City haitakua ''sehemu sahihi ya wachezaji'' iwapo hawatapata nafasi ya kucheza kila mmoja, hii ni kwa mujibu wa meneja wa City Pep Guardiola. (Manchester Evening News)

Chanzo cha picha, Reuters
Mkurugenzi wa ufundi wa AC Milan Paolp Maldini amesema klabu itasitisha mazungumzo na wachezaji kuhusu ongezeko la mkataba baada ya ripoti kuwa mlinda mlango wa Italia Gianluigi Donnarumma ambaye mkataba wake unamalizika msimu huu wa joto, kukabiliwa na mashabiki. (Ansa, via Mail)
Kiungo wa kati wa zamani wa Manchester United Roy Kean anaamini kuwa klabu hiyo inapaswa kujaribu kumsajili mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, 27 na Jack Grealish anayekipiga Aston Villa ili kuwapa changamoto wanaoongoza ligi ya primia Manchester City next msimu ujao. (Sky Sports)
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema anaona mustakabali mzuri siku za usoni kwa mchezaji wa nafasi ya kiungo wa kati wa Guinea Naby Keita,26, katika klabu hiyo. (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images
Tottenham wanamuwinda winga wa Brazil Rodrigo Varanda na mazungumzo ya awali yameanza ya kumnasa mchezaji huyo mwenye miaka 18 anayekipiga Corothians. (Sun)
Mlinzi wa Austria David Alaba, 28, atapokea mshahara wa Euro milioni 12 sawa na mlinzi wa kati wa Real Madrid Sergio Ramos baada ya kuelekea Bernabeu kwa uhamisho huru mkataba wake na klabu ya Bayern Munich utakapomalizika. (Fabrizio Romano, via AS)

Chanzo cha picha, Getty Images
Fulham imemfuatilia mshambuliaji wa Peterborough United, Siriki Dembele, 24, ambaye pia anazivutia klabu za Rangers, Celtic na Crysta Palace. (Football Insider)












