Mzozo wa Tigray: 'Raia wauawa’,yasema Amnesty International

"Mamia ya watu" huenda wameuawa katika mzozo unaoendelea kufukuta katika jimbo la Tigray ikaskazini mwa Ethiopia, Shirika la kutetea haki la Amnesty International linasema.

Waliyoshuhudia mapigano ya siku ya Jumatatu wanalaumu wapiganaji wanaounga mkono chama cha Tigray People Liberation Front (TPLF) kwa kutekeleza mauaji hayo lakini maafisa wa jimbo la Tigray wamekanusha kuhusika kwa vikosi vya TPLF.

Mapigano kati ya vikosi vya serikali na TPLF yalizuka wiki iliyopita.

Kupata mawasiliano imekuwa vigumu baada ya huduma za simu na intaneti kukatizwa.

Hii itakuwa mauaji makubwa ya raia tangu mzozo ulipoanza.

Kumekuwa na hali ya taharuki ya muda mrefu kati ya serikali ya Ethiopia na TPLF, ambayo inaongoza jimbo la Tigray, ambalo lipo kaskazini mwa nchi, na matokeo ya mzozo huo umekuwa makabiliano ya kijeshi ikiwa ni mashambulio ya angani yanayofanywa na vikosi vya serikali.

Kutokana na makabiliano hayo maelfu ya raia wamevuka mpaka na kuingia nchini Sudan, ambako wamepewa hifadhi katika kambi ya wakimbizi.

Shirika la Amnesty limesema nini?

Katika taarifa, Shirika hilo lilisema linaweza kuthibitisha kwamba "Waathiriwa kadhaa ambao idadi yao huenda ikafikia mamia ya watu walichomwa kisu au kakatwa mapanga hadi kufa katika mji wa Tigray nchini Ethiopia haiku wa Novemba tarehe 9".

Maafisa wake "waliona picha na video za kutisha za miili ya watu iliyotapakaa maoneo tofauti au zingine zikibebwa kwa machela ambazo zilizothibitishwa kidijitali ".

Shirika la kutetea haji la Amnesty linasema wahasiriwa walionekana kuwa wafanyakazi na kwamba hawakuhusika kwenye mzozo.

Deprose Muchena, Mkurugenzi wa Amnesty International katika eneo la mashariki na kusini mwa Afrika, alitaja hali hiyo kuwa "janga la kutisha " na kutoa wito kwa serikali kurejesha huduma za mawasiliano ili waweze kufuatilia hali inayoendelea katika eneo hilo.

Amnesty limesema mashahidi walizungumzia majeraha waliyopata baada ya kushambuliwa kwa "vifaa vyenye makali kama visu na mapanga". Baadhi ya walioshuhudia matukio hayo wanasema mashambulio yaletekelezwa na vikosi tiifu kwa TPLF baada ya kushindwa na vikisi vay serikali katika eneo Lugdi.

Umoja wa Mataifa umesema kuwa vifaa muhimu vya misaada kwa maelfu ya watu kaskazini mwa Ethiopia uno hatarini kutokana na Thalia zinazoendelea katika eneo hilo

Katika ujumbe uliyotolewa kupitia kanda ya video siki ya Alhamisi, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alisema vikosi vyake "vimekomboa" sehemu ya magharibi ya Tigray kutoka mikononi mwaf TPLF.

Pia aliawalaumu wapiganaji waliyo na ufungamano na TPLF kwa ''ukatili", na kusema kuwa wakati wanajeshi walipochukua udhibiti wa mji wa Sheraro "walipata miili ya wafanyakaziwa jeshi la ulinzi ambao waliuawa, kisha mikono na miguu yao kufungwa''

Je ni nini kilitokea awali?

Waziri Mkuu aliamuru vikosi vya serikali kukabiliana na vikosi tiifu kwa TPLF Novemba 4 baada ya kusema kambi ya kijeshi imeshambuliwa.

Kutokea wakati huo kumeripotiwa mashambulio kadhaa ya agani. Bwana Abiy amesema vikosi vya serikali vimepiga hatua kubwa.

TPLF ilikuwa mwanachama mkuu katika serikali ya muungano ya Ethiopia kwa miaka kadhaa lakini Bwana Abiy amethibiti ushawishi wake baada ya kuingia madarakani mwaka 2018 TPLF ilikataa kujiunga na chama cha muungano.

Viongozi wa Tigray wanasema wamelengwa kimakosa kwa madai ya ufisadi.

Bwana Abiy anawalaumu baadhi ya viongozi wa TPLF kwa kuwa " watoro wa haki" na kupinga hatua yake ya kufanya marekebisho ya jinsi Ethiopia inavyoendeshwa.