Barua kutoka Afrika: Jumbe za WhatsApp kwa akinamama wa Nigeria zimekuwa kero

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika mfulululizo wa barua kutoka Afrika, mwandishi wa vitabu vya simulizi nchini Nigeria, Adaobi Tricia Nwaubani anasema watoto siku hizi wanalazimika kuondoa sauti wa ujumbe wa WhatsApp kutoka kwa mama zao.
Ni miaka michache tu iliyopita, mchekeshaji mmoja nchini humo aliwasema kwa utani akinamama wa makamu wa Nigeria na tabia zao kutuma simu kwa muda mrefu.
Inawezekana wanahitaji watoto wao wawasaidie kuandika ujumbe na kuutuma, au kufungua akaunti na kusoma barua pepe zao.
Na sababu zao za kila mara wanapokuta mtu alipiga simu na kumkosa wanasema "simu yangu ilikuwa kwenye mkoba."
Siku hizi, utani huo umekuwa kwa wamama wa Nigeria na namna wanavyowasiliana kwenye WhatsApp, mtandao ambao ni maarufu zaidi barani Afrika.
Mchekeshaji wa Nigeria kama Maraji amekuwa akitumia tabia yao hiyo kama utani .

"Mama yangu huwa anakaa muda wote wa asubuhi kwenye WhatsApp," alisema Udo mwenye miaka 39- ambaye nyumbani kwake ni Lagos.
"Muda wote anapokunywa kifungua kinywa au chai huwa anaangalia picha za watu zilizowekwa kwenye whatsapp ."
Tofauti na kwenye mtandao wa Twitter na Instagram, WhatsApp inaweza kufanya kazi hata kama intaneti ni ya chini katika maeneo mengi ya Nigeria.
Whatsapp haiitaji mtu kuwa na maelezo ya mtu au neno la siri kufungua, hivyo inawafanya waweze kutumia mtandao huo kiurahisi na kiukweli kwao , WhatsApp ndio mtandao wao.

Malalamiko yaliopo kwa vijana wa Nigeria kuhusu idadi ya meseji ambazo wanapokea kutoka kwa mama zao ambao wanatumia mtandao wa WhatsApp ni nyingi.
"Ukiamka tu unakutana na video 10 kutoka kwa mama yako ," Ihuoma, 41 mkazi wa Abuja Nigeria.
"Kila ujumbe unaanza kwa kusema : 'Lazima uangalie hii!' 'Hii inaweza kumsaidia mtu!' Hayo ndio maneno ya mwanzo."
'Kushirikishana ujuzi'
Lakini mama yangu mwenye umri wa miaka 76-, Patty, aliniambia kuwa jumbe zote huwa ametumiwa na huwa anatuma kwangu zile ambazo anaona zinanifaa".
"Huwa situmi jumbe za aina moja kwa kila mtu, ninaangalia maudhui yake," alisema.
"Huwa natuma jumbe hizo kwa watoto wangu, ni kama elimu na kuchangamsha akili zao na nnataka wapate ujuzi na kujua wengine wanafanyaje mambo.
Ni kama semina ninayotaka wanangu waipate."

Chanzo cha picha, AFP
Tangu Ihuoma atoe sauti kwa meseji za WhatsApp ambazo anatumiwa na mama yake na mara chache huwa anafungua meseji hizo.
Kwa akinamama wengi Nigeria suala la kutuma katika matangazo ujumbe alioandika mwenyewe kwa WhatsApp ni kubwa sana.
Inawafanya kupeleka maombi, ushauri na maoni yao.
Mwanamke mmoja alilalamika kwenye Twitter kuhusu tabia ya mama yake kuweka vitunguu katika kila pembezoni mwa nyumba ili kuondoa sumu, na mama yake alidai kupata ujuzi huo kwenye WhatsApp.

"Katika kundi la whatsapp la familia , mama yangu huwa anatuma meseji nyingi kwangu na ndugu zangu kuhusu masuala ya afya na ushauri wa mambo mbalimbali ," alisema Udo. "Na ukimuuliza baadhi ya maswali anakwambia jaribu kutumia na utaona matokeao yake.'"
Jumbe za tahadhari za watoto kuibiwa au matukio mbalimbali ya uhalifu na kusisitiza kuwa tunapaswa kuwa makini.
"Meseji hizo nyingi zilinifanya kutoka katika kundi la familia," Udo alisema. "Kaka yangu alimfungia mama asimtumie meseji tena jambo ambalo lilimuuma sana mama yangu. Lakini shida hata ukimwambia usitume hasikilizi anatuma tena."
Watu wengi wameniambia wamewafungia WhatsApp za mama zao bila kuwajulisha.


"Niliwahi kuhusika na mjadala mtandaoni kuhusu suala hili," Ihuoma alisema.
"Baadhi ya watu walitoa maoni kuwa wanataka kuwafungia mama zao wasiwatumie ujumbe wa whatsapp tena lakini hawawezi kufanya hivyo kwa mtu ambaye amewabeba miezi tisa tumboni.."
Walikuwa wamechoka kupata meseji za tahadhari, mifano ya kidini, wataalamu wa afya kuzungumzia jambo fulani kwa kutoa hatari zakemfano ugonjwa wa kansana namna gani nguo ya kubana inavyoweza kusababisha shambulio la moyo.
Simulizi nyigi zisizo za kweli au uelekeo sahihi.

Taarifa zote zilikuwa na picha na video.
Upatikanaji wa intaneti nchini Nigeria umefanya wanaigeria kuwa na maajabu mengi mtandaoni na picha nyingine huwa za kutengeneza.
Na kuwaaminisha watu kuwa mambo hayo yametokea au taarifa hizo za kweli kwa sababu wanaona picha.

"Mama yangu aliwatumia ndugu zangu picha ya video ya mnyama wa kutisha jamii ya mjusi(dragon)- akielea angani " alisema Grace, 41 anayeishi Lagos.
"Aliwaambia kuwa hicho ni kirusi cha corona kinaondoka duniani."
Grace alihamaki kuona mama yake ambaye ana elimu nzuri tu kuamini mambo kama hayo, mama yake mwenye miaka 76-alikuwa ameamini kabisa kuwa kirusi cha corona kimepigwa picha kikiondoka angani huko katika mji wa China wa Wuhan.
"Alinihoji nimejuaje kuwa video ile sio ya kweli, 'Mama, virusi vya corona haviwezi kupaa!' tulimcheka tu ."
Ni ngumu mara nyingine kuwaelimisha kuhusu ukweli wa video hizo na hata isiwezekane kumweleza kitu chochote tofauti na mara nyingine huwa ananiona kuwa nimekuwa mkali kwake au nmemdharau".
."















