Coronavirus: China yasitisha usafiri wa umma katika mkoa wa Wahun

Maafisa wa usalama wanampima joto msafiri katika eneo la mto Yangtze Januari 22, 2020 mjini Wuhan

Chanzo cha picha, Getty Images

Hali ya wasiwasi inaendelea kuongezeka katika mji wa Wuhan nchini China baada ya huduma za usafiri kusitishwa katika juhudi za kukabiliana na kusambaa kwa kirusi hatari cha Corona ambacho kinasababisha maradhi ya mapafu kuua watu 17.

Mamlaka katika mkoa wa Wahun imesitisha kwa muda usafiri wa ndege kutoka na kuenda latika mji huo, ikiw ani pamoja na treni, feri na mabasi.

Wakazi wamearifiwa wasiondoke katika mji huo ulio na watu milioni 11.

Baadhi yao wameelezea wasiwasi kuhusu upungufu wa chakula, mmoja alisema "huu ni mwisho wa dunia".

Visa vipya vya maambukizi zaidi ya 500 vimethibitishwa huku kirusi hicho kikisambaa hadi mataifa ya kigeni.

Virusi vipya pia vimeenea kutoka Wuhan hadi majimbo kadhaa ya China, Marekani, Thailand na Korea Kusini.

Virusi, vinavyojulikana kama 2019-nCoV, inaarifiwa kuwa ni aina mpya ambavyo havijatambuliwa awali kuwa vinaathari kwa wanaadamu.

Taarifa hii yenye kuogofya ulimwenguni kutokana na kasi ya ueneaji wa ugonjwa huo, mlipuko huo umewauwa watu 17, na kuna kesi 440 zilizothibitishwa.

Wachnguzi wa afya wanaarifu kuwa Virusi hiyo ilitoka katika soko la vyakula vya baharini ambalo "lilichanganya vyakula hivyo na shughuli haramu za wanyama wa porini".

Kama hiyo haitoshi Viongozi huko Hong Kong pia waliripoti kesi mbili za kwanza za eneo hilo.

Kama utakumbuka vizuri kulikuwa na virusi vya Sars ambavyo viliwauwa karibu watu 800 ulimwenguni mwanzoni mwa miaka ya 2000 na madaktari wanaarifu kuwa navyo ni jamii ya virusi vya Corona.

Mkutano wa kutathmini hatari za kiafya zinazokabili ulimwenguni ulisitishwa ili kuamua ikiwa inapaswa kutangazwa dharura ya afya kimataifa kama ilivyotokea wakati wa homa ya nguruwe na ugonjwa wa Ebola pia.

China virus

Chanzo cha picha, Google

Maelezo ya picha, usafiri wa umma wasitishwa nchini China kutokana na kitisho cha virusi vya Corona

Jioni ya Jumatano, viongozi wa China walithibitisha idadi ya waliokufa ilikuwa karibu mara mbili kutoka tisa kwa siku moja . Wote waliofariki hadi sasa ni kutoka Hubei, mkoa unaozunguka Wuhan.

Maafisa wa China waliarifu kuwa nchi hiyo kwa sasa iko katika "hatua muhimu zaidi" ya kuzuia na kudhibiti virusi hivyo.

Maafisa wanaarifu kuwa "Kimsingi, usiende Wuhan. Na wale wa Wuhan tafadhali usiondoke mjini," alisema makamu wa Tume ya Kitaifa ya Afya Li Bin katika mojawapo ya mkutano wa kwanza wa umma tangu kuzuka vya virusi hivyo.Mapema wiki hii, China ilithibitisha kwamba maambukizi baina ya binadamu na binadamu yametokea.

Dalili za maambukizi ya virusi hivi vipya vya Corona ni pamoja na dalili ya kushindwa kupumua vyema, homa, na kikohozi.

Maelezo ya video, Uchina yathibitisha virusi vya corona vinaweza kusambazwa

Kesi ya kwanza nchini Marekani ilithibitishwa mwanzoni mwa wiki hii . Rais Donald Trump alisema hali hiyo imedhibitiwa na kwamba anaamini taarifa iliyotolewa na viongozi wa China.

Ni jaribio kubwa la kuzuia kuenea kwa virusi hivi vya Corona , ambavyo tunajua sasa vinaweza kuenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.

Kuzuia usafiri wa aina yoyote kutoka sehemu moja kwenye ingine ulimwenguni Kunaweza kupunguza nafasi ya virusi vya Corona kufikia miji mingine nchini China na nchi zingine ulimwenguni.

Zuio hilo limetekelezwa kutokana na mamilioni ya watu wanaojiandaa kusafiri kwenda nchini China kwa likizo ya wiki nzima ambayo ni Mwaka Mpya wa Lunar.

Swali kubwa lililosalia ni ikiwa ni je wakaazi wa milioni 8.9 wa Wuhan wanaweza kutumia njia za barabara kuondoka eneo hilo