Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 05.01.2020:Lingard, Maddison, Koulibaly, Eriksen, Pogba, Rodriguez

Man United wako tayari kutoa kiasi cha Pauni million 45 ili kumnasa nyota wa Leicester City James Maddson na watamtoa Jesse Lingard ili kuweza kufanikisha usajili huo.

(Sunday Mirror)

West ham watapigana vikumbo na Man City katika kuwania saini ya beki kisiki wa Napoli Kalidou Koulibali. (Sunday Express)

Inter Milan wanataka kumsajili kiungo wa Spurs Christian Eriksen kwa dau la pauni million 20 katika dirisha hili la januari licha ya nyota huyo atakuwa huru kuondoka bure mwishoni mwa msimu. (Sun on Sunday)

Wagonga nyundo wa London, West ham wanatarajia kukutana na viongozi Wa Benfica wikiijayo ili kukamilisha dili ya usajili wa mkopo wa kiungo Gedson Fernande's mwenye miaka 20. (Record, via Daily Star Sunday)

Bosi wa Everton, Carlo Ancelotti anataka kumsajili kwa mkopo James Rodriguez kutoka Real Madrid. (Sun on Sunday)

Tottenham wanamatumaini ya kumsajili moja kwa moja kiungo Giovan lo Celso kutoka Real Betis ambaye anakipiga na Spurs kwa mkopo.(Sun on Sunday)

Crystal palace wanamuwania kimsajili kwa mkopo mshambuliaji Cenk Tosun kutoka Everton.(Sunday Mirror)

Beki wa Arsenal Mjerumani Shkodran Mustafa mwenye miaka 27 anaweza kuachana na washika mitutu wa London mwishoni mwa mwezi huu.(Sunday Mirror)

Bosi wa Leicester City Brendan Rodgers hajathibitisha taarifa za kukubali au kukataa kuwa timu yake itamsajili beki wa Juventus Merih Demirah. (Mail on Sunday)Tottenham wanamatumaini mshambuliaji wale kinda wa Miaka 17 Troy Parrot atasalia kwenye klabuni hapo kwa kwa kusaini mkataba mpya wa muda mrefu mwezi ujao.(Lancashire Telegraph)

Meneja wa Newcastle United Steve Bruce amesema kipaumbele cha timu hiyo ni kusajili mshambuliaji mwezi huu wa januari.(Sky Sports)

Meneja wa Wolves Nuno Santo ametupilia mbali mpango wa kumuuza beki wa kiitaliano Patrick Cutrone mwenye Miaka 22.(Football Insider)

Juventus wamefanya mazungumzo ya awali na Chelsea ili kuangalia uwezokano wa kumsajili beki wa kushoto wa timu hiyo mbrazil Emerson.