Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Dirisha la uhamisho la mwezi Januari 2020: Je ni mchezaji gani huenda akahamia klabu mpya Januari?
Kwa mara nyengine ni wakati wa dirisha la uhamisho la mwezi Januari.
Klabu zitakuwa katika majadiliano ya kupunguza bei ama hata kumsaini mchezaji maarufu, iwapo zinapigania kushinda taji la ligi, kushiriki katika michuano ya Ulaya ama hata kujaribu kutoshushwa daraja.
Hatahivyo kuna kitu muhimu kuangazia. Wachezaji waliochezea timu moja Ulaya hawashirikishwi sana na ushindaji wa mataji.
Je hatua hiyo inamaanisha kwamba klabuziko tayari kutoa fedha nyingi?
Jinsi thamani ya wachezaji inavyopatikana
Kampuni ya uwekezaji kutoka London Carteret Analytica inashauri timu tatu za ligi ya Uingereza na timu nyengine 12 kuu kutoka Ulaya na duniani kuhusu wachezaji wazuri.
Pia unaweza kusoma:
Data yake inaangazia thamani ya wachezaji - inayopatikana kwa kuhesabu kiwango chao cha mchezo, na mchango atakaopeleka katika klabu yake mpya mbali na umri wake kati 26-30.
Kampuni hiyo imetoa data kwa baadhi ya majina katika orodha ya michezo ya BBCSport ambao wanaweza kuhama mwezi Januari.
LIGI YA PREMIA
PAUL POGBA (26, kiungo wa kati , Manchester United)
Thamani Carteret: £85
Amehusishwa na uhamisho wa Real Madrid, Barcelona, Juventus
Wale wanaofuatilia watagundua kwamba Pogba alikuwepo katika orodha ya BBC Sport kuhusu wachezaji ambao huenda wakahamia timu nyengine mwezi Januari.
Kiungo huyo anaongoza orodha ya wachezaji wanaotaka kuhamia klabu nyengine kwa kuwa mazungumzo kuhusu uhamisho hayawezi kuisha.
Kiungo huyo wa Ufaransa aliyeshinda kombe la dunia hajashiriki mechi nyingi msimu huu kutokana na jeraha la kifundo cha mguu lakini mkufunzi wa Man United Ole Gunnar Solskjaer amesema kwamba mchezaji huyo hatauzwa.
Hatahivyo maswali mengi yamesalia kuhusu hatma yake ya Old Trafford.
CHRISTIAN ERIKSEN (27, kiungo wa kati , Tottenham)
Thamani: £51.4m
Anahusishwa na uhamisho wa Real Madrid, Manchester United
"Eriksen hapendwi tena katika klabu hiyo."
Hayo ndio yaliokuwa matamshi ya mchanganuzi wa kipindi cha BBC Radio 5 Live Darren Fletcher alipokuwa akimtazama raia huyo wa Denmark mapema msimu huu.
Eriksen alishindwa kuhamia klabu nyengine kutoka Spurs msimu huu na Carteret inasema kwamba kiwango chake cha mchezo kimeshuka kwa asilimia 38.5 msimu huu, na hivyobasi kuathiri thamani yake ilioshuka kwa £32.22m.
Mkufunzi wa Tottenham Jose Mourinho, aliyemuulizia Eriksen, alisema: Najua hatma yake .
Kandarasi yake katika klabu ya Tottenham inakamilika msimu huu na ameonyesha kwamba hayuko tayari kutia saini kandarasi mpya , ikimaanisha kwamba mwenyekiti wa klabu hiyo Daniel Levy huenda akamuuza iwapo kutakuwa na ofa nzuri katika dirisha dogo la uhamisho la mwezi Januari.
OLIVIER GIROUD (33, mshambuliaji, Chelse
Amehusishwa na uhamisho wa: Inter Milan, Atletico Madrid
Ni mchezaji mwengine aliyeorodheshwa ambaye ni mshindi wa kombe la dunia akiichezea Ufaransa.
Giroud amekuwa hashirikishwi katika mechi nyingi katika klabu ya Chelsea chini ya ukufunzi wa Frank Lampard, kutokana na mchezo mzuri wa mshambuliaji wa England Tammy Abraham, huku Michy Batshuayi akiwa mbele yake katika itifaki.
Kandarasi ya mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal inakamilika mwisho wa msimu huu.
Akiwa na magoli 80 katika ligi ya Premia atakuwa na mchango mzuri katika klabu ambayo imekosa mfungaji mabao wa mara kwa mara.
LUCAS TORREIRA (23, kiungo wa kati, Arsenal)
Thamani: £37.85m Napoli
Mchezaji huyu wa Uruguay alionyesha mchezo mzuri alipozinduliwa katika msimu wake wa kwanza Arsenal lakini amekuwa akikosa kuchezeshwa mara kwa mara msimu huu hatua iliozua mjadala wa iwapo anataka kuondoka.
Kiungo huyo kutoka Sampdoroa huenda akarudi katika ligi ya Serie A, huku ajenti wake akisema mapema msimu huu ''Tutaona kitakachotokea
CENK TOSUN (28, Mshambuliaji, Everton
Anahusishwa na uhamisho wa: Leeds United, Crystal Palace, Besiktas
Tosun msimu huu ameifungia goli moja Everton na Uturuki magoli 3.
Hicho kitakwambia kila kitu unachohitaji kujua kuhusu hali ya Tosun katika klabu ya Goodison Park. Mchezaji huyo wa zamani wa
Besiktas alishindwa kupata nafasi ya kushiriki mechi mara kwa mara chini ya ukufunzi wa Marco Silva na kwamba hali yake haijaimarika.
Baada ya kusajiliwa kwa dau la £27m mwezi Januari 2018, Tosun alitajwa na mkufunzi wa Everton wakati huo Sam Allardyce kuwa mchezaji bora wa Ulaya akiwa na thamani hiyo.
NATHAN AKE (24, beki, Bournemouth)
Thamani: £52m
Anahusishwa na uhamisho wa: Manchester City, Chelsea, Tottenham
Iwapo uhamisho huu utafanyika basi utafanyika katika siku za mwisho za dirisha la uhamisho.
Ake amekuwa mmoja wapo wa mabeki wanaotegemewa sana tangu alipojiunga na klabu ya Bournemouth 2017 na amekuwa akiichezea Uholanzi mara kwa mara.
Beki huyo wa zamani wa Chelsea kwa sasa anauguza jeraha la mguu na Chelsea wamedaiwa kuwa na kifungu cha kumnunua chenye thamani ya £40m ikiwa ni £12m chini ya thamani yake iliotolewa na kampuni ya Carteret.
WILFRIED ZAHA (27, winger, Crystal Palace)
Thamani: £41.1m
Chelsea inamnyatia winga huyo hodari.
Zaha karibia aondoke Selhurst Park mwisho wa msimu uliopita lakini klabu zilishindwa kutoa dau la £80m ambazo Crystal Palace ziliitisha.
Lakini bei hiyo huenda ikawa kikwazo kikuu kwa baadhi ya timu kwa mara nyengine kwa kuwa Palace inasema kwamba haina mpango wa kupunguza bei hiyo.
Mchezaji huyo wa Ivory Coast ni mchezaji bora wa Palace lakini huenda akajaribu kuondoka tena iwapo klabu inayocheza katika ligi ya mabingwa itapiga hodi kutaka kumnunua- na huku ikiwa marufuku ya Chelsea imeondolewa huenda wakawasilisha ombi..
DWIGHT MCNEIL (20, kiungo wa kati , Burnley)
Thamani: £24.75m
Anahusishwa na uhamisho wa : Tottenham, Newcastle, Crystal Palace
Mchezaji huyo wa timu ya England ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 McNeil, ambaye aliachiliwa na Man United wakati akiwa katika mafunzo katika klabu hiyo ameimarisha mchezo wake katika klabu ya Burnley huku akicheza karibia kila mechi msimu huu.
Mchezaji huyo anayetumia guu lake la kushoto amemfurahisha mkufunzi Sean Dyche akifunga magoli mane kufikia sasa
KUTOKA ULAYA...
JADON SANCHO (19, winga, Borussia Dortmund)
Thamani: £44m.
Amehusishwa na Uhamisho wa: Manchester City, Manchester United, Chelsea, Real Madrid, Barcelona
Sancho amekuwa na matatizo yake katika klabu ya Borrusia Dortmund msimu huu, baada ya kuwachwa nje na kupigwa faini kwa kuchelewa alipotoka kuichezea England.
Lakini ameonyesha uhodari wake uwanjani , akiwa mchezaji wa kwanza wa Ulaya kufunga magoli na kutoa usaidizi wa magoli 10 katika mashindano yote.
Wakati huohuo klabu hiyo ya Ujerumani imewasilisha ombi la kutaka kumnunua mshambuliaji wa Red Bull Salzburg.
Je Sancho angependelea kurudi katika ligi ya Premia, ambapo hakupata nafasi ya kushiriki katika kikosi cha kwanza akiichezea City?
Hatahivyo hatakuwa bei rahisi..
GARETH BALE (30, winga, Real Madrid)
Thamani: £44m
Amehusishwa na uhamisho wa: Tottenham, Manchester United"Wales. Golf. Madrid.
Bale alikuwa na presha kutoka kwa mashabiki wa Real.
Uhamisho wake wa kuelekea klabu nyengine uligonga mwamba na mchezaji huyo wa zamani wa Tottenham na Southampton amekuwa akiwekwa nje na mara nyengine kuchezeshwa chini ya ukufunzi wa kocha Zinedine Zidane.
Kulingana na ajenti wake Bale hafurahii kusalia katika klabu hiyo.
TIMO WERNER (23, mshambuliaji, RB Leipzig)
Thamani: £60.6m
Amehusishwa na uhamisho wa: Real Madrid, Manchester United, Chelsea, Liverpool
Huku mabingwa Bayern Munich na Borussia Dortmund wakiteteleka , RB Leipzig wanaendelea kuonyesha umahiri wao katika ligi hiyo.
Mshambuliaji Werner amekuwa kiungo muhimu , huku magoli yake 18 yakipatikana kila baada ya dakika 79 na huenda mchezaji huyo wa Ujerumani akaondoka iwapo atapata ombi zuri
EDINSON CAVANI (32, mshambuliaji, Paris St-Germain)
Amehusishwa na uhamisho wa Atletico Madrid, LA Galaxy
Mchezaji huyo wa Uruguay Cavani ameshukishwa katika itifaki katika uwanja wa PSG nyuma ya Mauro Icardi, Kylian Mbappe na anapokuwa imara - Neymar.
Cavani amefunga magoli matatu msimu huu , kandarasi yake inakamilika mwezi Juni na huenda akapatikana kwa bei nzuri Januari.
THOMAS LEMAR (24, winga, Atletico Madrid)
Amehusishwa na uhamisho wa: Lyon
Mchezaji wa Ufaransa Lemar alikuwa akilengwa na Liverpool kwa dau la £60m 2017 , lakini alisalia Monaco na Arsenal wakashindwa kumsajili katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari 2018.
Baadaye alielekea Atletico Madrid kwa dau la £52.7m lakini ameshindwa kushirikishwa katika kikosi cha kwanza .
Mwezi Disemba alizomewa na mashabiki wake licha ya timu hiyo kuishinda Osasuna.