Unazijua athari za sumu kuvu katika ugali wako?

ugali

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 3

Uchunguzi uliofanywa na kituo cha televisheni nchini Kenya umefichua ni jinsi gani sera dhaifu zilivyoruhusu viwango vya hali ya juu vya unga wa ugali wenye sumu kuvu - aflatoxin kuuzwa nchini humo jambo lililosababisha watu wengi kuhoji juu ya viwango vya usalama wa chakula nchini humo.

Uchunguzi uliofanywa na televisheni ya kibinafsi NTV ulifanya vipimo vya unga wa Ugali wa mahindi na mtama za nenmbo aina 12 za bidhaa hizo za nafaka.

Unaweza pia kusoma:

Nembo tatu zilibainika kuwa na viwango vya hali ya juu vya sumukuvu kuliko kiwango kinachopendekezwa cha sehemu 10 kwa bilioni, huku saba zikiwa bado zikiwa na viwango vya hali ya juu vya sumukuvu (aflatoxin).

Aflatoxin, ambayo hutengenezwa na fangasi katika mazao ya kilimo na inaweza kusababisha saratani.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Wiki moja tu iliyopita Mamlaka ya Kenya ya viwango (kebs) ilinyang'anya makampuni ya utengezaji wa Siagi ya karanga inayotumiwa zaidi kupakwa kwenye mikate kutokana na hofu kuwa ilikuwa na sumu kuvu. Pia ilionya Umma dhidi ya kutumia kama chakula cha unga wa ugali kutoka makampuni matano ya unga wa mahindi.

Madaktari na wataalamu wa chakula waliohojiwa katika taarifa ya uchunguzi ya runinga walisema kuwa baadhi ya watu walikufa kutokana na ulaji wa unga huo unaodaiwa kuwa na sumukuvu.

Madaktari pia walihusisha visa vya saratani za ini na mfuko wa uzazi na ulaji wa ugali wenye sumu kavu.

Unaweza pia kusoma:

Waziri wa Kilimo Mwangi Kiunjuri, ambaye pia alihojiwa na uchunguzi wa runinga, alithibitisha kuwepo kwa sumu ya sumukuvu katika vyakula nchini humo .

Alisema kuwa wana wasiwasi kuwa wanyama wanaofugwa nyumbani , kama vile ng'ombe, pia wanakula vyakula vyenye sumu jambo na kuisambaza kwa walaji.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Bwana Kiunjuri alilaumu biashara ya kikanda kuwa sababu ya kuwepo kwa chakula chenye sumu.

"Huwezi kusema kuwa utapambana nayo ndani ya mipaka ya Kenya. Tunabadilisha ," alisema.

Mahitaji ya hali ya juu ya chakula kikuu unga wa mahindi yamekuwa yakiilazimisha serikali kubuni sababu ya kuagiza mahindi kutoka nje ya nchi.

Mwaka 2009, Mkurugenzi Mkuu wa Kebs Kioko Mangeli alifichua kuwa Wakenya wamekuwa wakila ugali wenye sumu tangu mwaka 2008, huku serikali ikiwa na uelewa fika wa hilo.

"Nina uhakika wa zaidi ya 100% kwamba inawaathiri watu na kwamba katika kipindi cha miaka 10 hadi 15 tutakuwa pia na visa vingi vya saratani kokana na mahindi ," Bwana Mangeli aliiambia kamati ya bunge la Kenya.

ugali

Chanzo cha picha, Getty Images

Kutokana na hayo Wakenya wameingia katika mtandao wa habari wa kijamjii wa Twitter kupitia hashtag #WhiteAlert huku wakiitaka serikali iwakamate maafisa wanaohusika na kuhakikisha viwango vya usalama wa chakula nchini humo.

Hali ikoje kwa Tanzani juu ya Sumukuvu katika nafaka?

nafaka

Chanzo cha picha, Getty Images

Tanzania ikiwa ina maatumizi ya nafaka kwa kiwango kikubwa Afrika mashariki, vyakula ambavyo vinaweza kuambukizwa sumu kuvu ni kama vile mahindi na unga wake, karanga na mazao yanayotokana na karanga, muhogo.

Sumu kuvu inatokana na fangasi ambayo inayoota kwenye mbegu za nafaka, hutokea pale ambapo nafaka ikiwa imetunzwa vibaya.

Sumu hiyo mara nyingi husababisha kansa ya ini na inaweza kusababisha vifo vya watu kwa pamoja na kama watu wakila chakula hicho kwa pamoja basi wote wanaweza kuathirika.

Unaweza pia kusoma:

Sumu kuvu (fangasi) unaoota kwenye mbegu za nafaka na jamii ya kunde, mazao ya mizizi na karanga.

Mtaalamu wa masuala ya Afya na mwandishi kutoka nchini Tanzania Syriacus Buguzi anasema kuwa Sumu kuvu ni tatizo kubwa nchini Tanzania, utafiti uliofanyika mwaka 2012 uliangazia taifa zima na kuonyesha jinsi sumu hiyo inaweza kuathiri chakula kwa kiwango kikubwa.

Mwaka 2016, kesi 65 ziliripotiwa katika maeneo ya Chemba and Kondoa mkoani Manyara na watu 19 walifariki dunia kutokana na ugonjwa unaojulikana kitaalamu kama 'Aflatoxicosis' unaosababishwa na sumu kuvu kwenye nafaka iliyoharibika.

Ruka X ujumbe, 3
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 3

Buguzi anasema mara nyingi athari hii inapowatokea watu, ni ngumu kugundua chanzo cha tatizo lililowapata kutokana na uelewa kuwa mdogo bado.