Kimbunga cha mwisho kilitua mkoa wa Lindi miaka 67 iliyopita

Wakati upwa wa kusini mwa Tanzania ukijiandaa na makali ya Kimbunga Kenneth kinachotarajiwa muda wowote kuanzia leo usiku mpaka Ijumaa alfajiri, mamlaka nchini humu zimebainisha kuwa mara ya mwisho kwa wnwo hilo kupigwa na tufani ilikuwa takribani miongo saba iliyopita.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imebainisha kuwa kimbunga cha mwisho kuikumba nchi hiyo kilikuwa mwaka 1952 mkoani Lindi.
Kipindi hicho nchi ilikuwa chini ya ukoloni wa Mwingereza na ilikuwa bado ikiitwa Tanganyika.
"Wakati ule Lindi haikuwa na watu wengi, na wala hakukuwa na miundombinu mingi ya kuharibiwa kama ilivyo kwa sasa," amesema Agness Kijazi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa TMA.
"Wakati huu maendeleo ni makubwa katika pwani yetu na watu ni wengi, hivyo athari (za Kimbunga Kenneth) zitakuwa kubwa," amesema Kijazi.
Kijazi amesema kufikia sa tisa mchana wa leo kimbunga kitakuwa umbali wa kilomita 177 kutoka pwani ya Mtwara kikiwa na kasi ya kilometa 140 kwa saa.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa YouTube ujumbe
Kutokana na kasi hiyo kimbunga kinatarajiwa kutua nchini Msumbiji kuanzia alfajiri ya Ijumaa kikiwa na kasi kilomita 100 kwa saa.
Hata hivyo, kitakapotua kimbunga hicho ni karibu na mpaka wa Tanzania kwa kilomita 230, na athari zake zinatarajiwa kukumba maeneo yaliyo ndani ya kilomita 600.

Chanzo cha picha, AccuWeather
"Nchini mwetu, maeneo ya mpaka Lindi na Ruvuma yataathirika sana," amesema Kijazi na kuongeza, "wakazi hususani wa Mtwara kwa sasa wanaweza wakaona tu kuna mvua zinanyesha lakini waendelee kuchukua tahadhari. Kadri muda unavyosidi kusonga ndiyo kimbunga kinazidi kukaribia nchi kavu."
Maelezo ya Kijazi yanarandana na ya Shirika la Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani WMO linaendelea kuonya kuwa Kimbunga Kenneth ni hatari sana na kinaelekea kupiga eneo ambalo halijawahi kukumbwa na tufani toka picha za satelaiti zianze kuchukuliwa.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Picha za satelaiti kwa mara ya kwanza zilianza kuchukuliwa toka angani kuanzia miaka ya 1940, na picha ya kwanza kwa utabiri wa hali ya hewa ilipigwa mwaka 1960 na chombo cha TIROS-1 cha shirika la anga la Marekani NASA.

Wakati huo huo, mamlaka visiwani Zanzibar, Tanzania zimesitisha usafiri wa baharini kama sehemu ya tahadhari dhidi ya Kimbunga Kenneth.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Visiwa vya Zanzibar vinategemea usafiri wa majini kama njia kuu ya mawasiliano na biashara baina ya visiwa vikuu viwili vya Pemba na Unguja pamoja na miji ya Tanzania bara hususani Dar es Salaam, Tanga na Bagamoyo.
Wakazi wa Mtwara asubuhi waliitikia wito wa kuhama maeneo wanayoishi na kukimbilia kwenye shule na uwanja wa ndege.

Hata hivyo, ilipotimu tisa unusu mchana baadhi ya wakazi hao walianza kurudi kwenye makazi yao.
Mwandishi wa BBC Eagan Salla aliyepo katika eneo hilo anasema 'giza limeanza kuingia na watu wanahisi njaa'