Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
DRC yamkamata kamanda wa waasi wa FDLR
Raia mmoja wa Rwanda ambaye aliwahi kuhudumu kama kamanda wa waasi wa kabila la Hutu anayetafutwa kwa kutekeleza mauaji nchini DRC amekamatwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Habyarimana Mucebo ,mwanachama mwandamizi wa kundi la waasi wa Rwanda ,FDLR alikamatwa katika eneo la Rutshuru,kaskazini mashariki mwa DR Congo.
Wanachama wa kundi hilo walitoroka DR Congo baada ya mauaji ya kimbari ya 1994 nchini Rwanda.
Mauaji hayo ya takriban Watutsi 800,000 pamoja na Wahutu wenye msimamo wa kadri yalizua hiasia kali katika eneo hilo.
Bwana Mucebo ,afisa wa maswala ya kiintelijensia anachunguzwa kulingana na jeshi.
Viongozi wengi wakuu wa kundi hilo la waasi wanatafutwa na Rwanda kwa jukumu lao katika mauaji ya 1994.
Kukamatwa kwa Mucebo hakuhusishwi na mashtaka ya mauaji ya kimbari kama ilivyoripotiwa hapo awali.