Afcon 2021: Kila unachohitaji kujua kuhusu mashindano nchini Cameroon

Africa Cup of Nations trophy

Chanzo cha picha, Getty Images

Michuano ya kwanza mikubwa ya kandanda 2022 itaanza Jumapili, huku Kombe la Mataifa ya Afrika likichukua nafasi kuu.

Nyota kadhaa wa Ligi Kuu na Ulaya watashuka dimbani Cameroon, huku wenyeji wakimenyana na Burkina Faso katika mchezo wa ufunguzi.

Kwa mara ya kwanza ilipangwa kuanza Juni 2021 lakini ikasogezwa mbele hadi Januari mwaka jana ili kuepusha msimu wa mvua nchini Cameroon, michuano hiyo imecheleweshwa hadi 2022 kwa sababu ya janga la coronavirus.

Shirikisho la Soka barani Afrika (Caf) limekabiliwa na ukosoaji juu ya muda wa kipute hicho na mwezi uliopita ilibidi kushughulikia uvumi kwamba michuano hiyo ingecheleweshwa au kuhamishwa kufuatia kuibuka kwa kirusi cha Omicron cha Covid-19.

Mshambulizi wa zamani wa Arsenal na Uingereza Ian Wright alisema baadhi ya taarifa hasi kwenye vyombo vya habari ni "kutoheshimu" na "kuchomwa na ubaguzi wa rangi".

Ni muundo gani na michezo ni lini?

Kwa michuano ya pili mfululizo, Kombe la Mataifa itakuwa na washiriki 24.

Hiyo inamaanisha makundi sita ya wanne, huku mawili ya juu yakifuzu kwa hatua ya 16 bora sambamba na timu nne zilizo kwenye nafasi ya tatu bora.

Michezo itafanyika saa 13:00, 16:00 na 19:00 (mara zote GMT) wakati wa awamu ya makundi, na nyakati mbili za maondoano zitatumika katika awamu ya maondoano kuanzia Jumapili, 23 Januari.

BBC itatangaza michezo 10 ikijumuisha fainali katika uwanja wa Olembe mjini Yaounde Jumapili, Februari 6. Mchezo wa kwanza kuonyeshwa utakuwa pambano la uzito wa juu kati ya Nigeria na Misri siku ya Jumanne.

Mpira unaotumiwa ni Umbro Toghu, uliopewa jina kutokana na vazi la rangi nyingi na lililopambwa vizuri ambalo hapo awali lilibuniwa kwa ajili ya watu wa kifalme lakini sasa linajulikana kote Kamerun.

Washindani wakuu ni akina nani?

Ni vigumu kuwapuuza mabingwa Algeria, ambao wako kwenye msururu wa mechi 34 bila kushindwa na kuongozwa na winga wa Manchester City Riyad Mahrez.

Senegal ya Sadio Mane, timu iliyoorodheshwa bora zaidi barani Afrika kwa miaka mitatu iliyopita, walikuwa washindi wa pili mwaka wa 2019 na miongoni mwa wapinzani wakuu, huku mabingwa mara saba Misri wakijivunia kuwa na mchezaji bora zaidi duniani hivi sasa ndani ya Mohamed Salah, ambaye ameng'ara akiwa Liverpool msimu huu.

Ghana na Nigeria ni miongoni mwa nchi zilizofanikiwa zaidi barani humo lakini zilikuwa na kampeni zisizoridhisha za kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2022, huku Cameroon - ikiwinda taji lao la sita la Kombe la Mataifa ya Afrika - itapania kupata nafasi katika ardhi ya nyumbani.

Mali inaweza kuwa kikosi cha kushtukiza baada ya kufuzu kwa hatua ya maondoano ya Kombe la Dunia kwa kwenda bila kufungwa licha ya kupokonywa faida ya nyumbani.

Ivory Coast, Morocco na Tunisia ni miongoni mwa mabingwa wengine wa zamani waliopo na, kwa upande mwingine wa wigo, Comoro na Gambia ni wafuzu kwa mara ya kwanza.

Vipi kuhusu muda?

Kumekuwa na manung'uniko kutoka kwa baadhi ya vilabu vya Ulaya kuhusu kuwaachilia wachezaji wao katikati ya msimu kwa ajili ya michuano hiyo.

Klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza Watford, kwa mfano, ilishutumiwa kwa "kutoa meno" na Nigeria katika mzozo wa kupatikana kwa Emmanuel Dennis, pambano ambalo Hornets walishinda.

Hata hivyo, hali ya hewa nchini Cameroon na kulazimishwa kubadili michuano hiyo inayofanyika kila baada ya miaka miwili hadi mwaka wa Kombe la Dunia kumeifanya Caf kuwa na chaguo adimu katika muda wake.

Toleo la 2023 limepangwa kufanyika Juni na Julai mwaka ujao nchini Ivory Coast.

Gianni Infantino, rais wa shirikisho la soka duniani Fifa, amependekeza kuhamishwa kwa kombe la mataifa hadi kati ya Septemba na Novemba katika kalenda ya kimataifa iliyorekebishwa.

Vipi kuhusu masuala ya nje ya uwanja, kama vile coronavirus?

Ugonjwa huo bila shaka umeathiri michuano hiyo, huku Caf ikifikia 60% idadi ya wanaoingia kuona mechi .

Michezo inayohusisha waandaji Cameroon itaruhusiwa kuwa na asilimia 80%, na ni wale tu ambao wamechanjwa kikamilifu na wamepimwa virusi vya Covid-19 ndio wanaweza kuhudhuria mechi.

Huku asilimia 2 pekee ya nchi ikiwa imechanjwa kikamilifu kulingana na takwimu za Our World in Data, itafurahisha kuona jinsi vikwazo hivyo vinavyoathiri mahudhurio ya mechi 52 kuenea katika viwanja sita.

Nchi kadhaa ziliripoti kesi katika maandalizi ya michuano hiyo, huku Cape Verde ilikumbwa na mlipuko wa ugonjwa katika kambi yao ya mazoezi na washiriki wa kwanza Gambia walilazimika kusitisha mechi mbili za kirafiki, huku zaidi ya nusu ya kikosi chao kikikosekana.

Miundombinu nchini Cameroon na utayari wao wa kuwa mwenyeji umetiliwa shaka, ikizingatiwa walipaswa kuandaa mashindano ya 2019 ambayo yalilazimika kuhamishiwa Misri.

Kuna wasiwasi wa kiusalama juu ya Limbe, mji katika eneo la kusini-magharibi ulioathiriwa na vita katika miaka ya hivi karibuni na wanamgambo wa eneo hilo wanaofuata ajenda ya kujitenga.

Tangu mwaka wa 2017, makundi yenye silaha - ambayo yanahoji kuwa maeneo ya Anglophone ya Cameroon yametengwa na serikali inayozungumza Kifaransa - yamejaribu kuunda jimbo lililojitenga linaloitwa Ambazonia.

Katika harakati za kudumisha utulivu, magari ya kivita na vituo vya ukaguzi vimesambazwa wiki hii katika eneo la Limbe, ambapo bomu lililotegwa ndani ya gari lililipuka usiku wa kuamkia Januari 2021 kwa Cameroon kuandaa Michuano ya Mataifa ya Afrika Januari 2021, na milipuko zaidi imetokea katika eneo hilo miezi ya hivi karibuni.

Viongozi wa eneo hilo wamesema hatua za kiusalama zilizochukuliwa zinamaanisha kwamba hakutakuwa na usumbufu wowote kwa Afcon, huku Limbe ikitarajiwa kuandaa mechi nane, zikiwemo mbili za mtoano.

Jinsi ya kufuata mashindano

BBC itatangaza michezo 10, ikijumuisha miwili ya robo fainali, nusu na fainali. Sky Sports itaonyesha kila mechi nchini Cameroon, huku beIN SPORT, Canal+ na SuperSport zikiwa kati ya zile zinazotoa matangazo kote Afrika.

Tovuti ya BBC Sport pia itakujulisha wakati wa mashindano, ikijumuisha habari za kila siku za mechi, pamoja na matangazo ya moja kwa moja kuanzia robo fainali na kuendelea.