Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Everton 1-1 Aston Villa: Goli la Walcot lavunja matumaini ya Mbwana Samatta na Aston Villa kusalia katika EPL
Aston Villa italazimika kushinda mechi zake zote mbili za mwisho dhidi ya Arsenal na West Ham iwapo inataka kusalia katika ligi ya Premia , kulingana na kocha Dean Smith.
Villa ilinyimwa ushindi mzuri wa ugenini wakati mchezaji wa ziada wa Everton Theo Walcott alipofunga bao la dakika 87 ili kusawazisha bao la Ezri Konsa.
Kikosi cha Smith kina pointi tatu chini ya nafasi bora ya kusalia katika ligi , na mechi moja ya nyumbani dhidi ya Arsenal Jumanne ijayo na baadaye kucheza mechi yao ya mwisho ugenini dhidi ya West ham tarehe 26 mwezi Julai .
'' Inaonekana hivyo'',alisema Smith baada ya kuulizwa iwapo sasa walihitaji ushindi wa mechi hizo mbili.
Villa imeshinda mara moja katika mechi 12 za ligi ya premia lakini Smith anaamini kwamba timu yake ina uwezo wa kusalia katika ligi hiyo.
''Najua hatujatoka kwasababu naona uwezo wa wachezaji wangu, aliongezea. Tulifanya kila kitu kushinda mechi hii lakini bahati mbaya kutomakinika na kushindwa kufunga bao la pili kumetugharimu.
Bao la kwanza la Konsa katika ligi ya England lilionekana kuipatia ushindi mkubwa Villa katika uwanja wa Goodison park, baada ya beki huyo wa zamani wa Brentford kufunga akiwa karibu na goli kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na Hourihane.
Lakini Villa haikuweza kuzuia ushindi huo, wakati Walcott aliposawazisha kwa kichwa licha ya jaribio la konsa kulipangua shambulio hilo katika mstari wa goli.
Muda unayoyoma kwa Aston Villa
Lengo la Smith na wachezaji wake wa Villa ni kufika katika siku ya mwisho ya msimu na fursa ya kusalia katika ligi ya Premia.
Licha ya kuchukua pointi nne katika mechi mbili za mwisho muda unayoyoma kwa klabu hiyo ya eneo la Midlands.
Huku Westaham ikiialika Watford siku ya Ijumaa, Villa itakuwa pointi nne kutoka eneo salama iwapo mechi zitakazochezwa tarehe 16 na 17 zitakwisha kwa sare katika uwanja wa London.
Baada ya kukiona kikosi chake kikichukua uongozi katika dakika ya 72 huku wakifanya shambulio la kwanza , Smith alionekana kama mtu asiyetakiwa baada ya kipenga cha mwisho cha mechi huku timu yake ikishindwa kutumia fursa waliokuwa nayo walipokuwa wakiongoza 1-0.
Villa iliwazuia wapinzani wao na kutowaruhusu kushambulia lango lao kabla ya Konsa kufunga kufuatia mpira wa adhabu kutoka kwa Hourihane.
Hatahivyo Villa ndio timu ya pekee ambayo haijakosa kufungwa ugenini katika ligi ya Premia msimu huu.
Je Villa itaponea kushushwa daraja?
Kwa sasa Villa ipo katika nafasi ya 19 katika ligi ya Premia na iko pointi nne nyuma ya Watford , ambayo ndio inayoshikilia nafasi ya mwisho juu ya eneo la kushushwa daraja.
Arsenal ambayo hivi majuzi iliiwalaza mabingwa wa ligi ya England Liverpool imeimarika na inatumai itashinda mechi mbili zilizosalia ili kufuzu katika makombe ya Ulaya.
West ham ambayo ipo katika nafasi ya 16 na haijacheza mechi moja iko pointi sawa na Watford na inatishiwa kushuka daraja iwapo itapoteza mechi tatu zilizosalia
Mashabiki wa Villa pia watakuwa wakiangalia matokeo ya klabu ya Bounemouth , Watford na West Ham katika wiki zijazo. Akiuzngumza wikendi mkufunzi wa Astona Villa Smith alisema:
''Nimesema mara kadhaa tangu mwanzo kwamba mchezo wetu haujatupatia matokeo tuliokuwa tukitarajia. Mbinu niliotumia na wachezaji ni kwamba leo ndio siku ya nusu fainali ya kwanza ili kuweza kufuzu awamu ya pili''.
''Hatuwezi kudhibiti kitu chengine chochote, bali mchezo wetu tu. Hii ilikuwa nusu fainali yetu ya kwanza ili kuweza kufuzu awamu ya pili''.