Ligi ya Premia: Man City yawika Newcastle yailaza Tottenham ugenini

Chanzo cha picha, Getty Images
Pep Guardiola amemwagia sifa chungu nzima kiungo wake wa kati David Silva kama mmojawapo wa wachezaji wake wazuri zaidi aliokutana nao baada ya kuchangia katika magoli yote matatu katika ushindi mkubwa dhidi ya klabu ya Bournemouth ugenini
Akiadhamisha mechi yake ya 400 akiichezea City, Silva alionyesha umahiri wake huku mabingwa hao wakipanda hadi nafasi ya pili katika jedwali la ligi wakiwa pointi mbili nyuma ya Liverpool.
Wakati huohuo goli la kwanza la mchezaji aliyevunja rekodi ya usajili katika klabu ya Newcastle Joelinton liliipatia ushindi klabu hiyo huku mkufunzi Steve Bruce akijipatia pointi za kwanza kama meneja tangu ajiunge na timu hiyo.
Mshambuliaji huyo wa Brazil alichukua fursa ya masikhara ya safu ya ulinzi ya Tottenham kudhibiti pasi ya mchezaji wa ziada Christian Atsu kabla ya kumfunga kipa Hugo Lloris.
Atsu, aliyeingia baada ya Allan Saint-Maximin kutolewa kutokana na jeraha la mguu alitoa usaidizi wa goli hilo katika mchango wake muhimu.

Chanzo cha picha, AFP
Spurs ilikosa ujuzi wa kuingia katika lango la Newcastle ambayo wachezaji wake wanne wa safu ya kati walirudi nyuma na kuanza kulinda lango lao.
Son Heung-min, akiichezea Tottenham kwa mara ya kwanza msimu huu baada ya kuhudumia marufuku ya mechi tatu alishindwa kuona lango la wageni hao licha ya kupata fursa za wazi.
Na hayo yakijiri magoli mawili ya Sergio Aguero yaliisaidia ManCity kuilaza Bournemouth ugenini.
Mchezaji huyo baadaye alimpatia pasi nzuri mshambuliaji matata wa timu hiuyo Raheem Sterlingkwa goli la pili kabla ya Aguero kujaza bao la tatu wavuni.
Mkufunzi Pep Guardiola alimmwagia sifa tele Silva kwa kuchangia katika magoli yote.

Chanzo cha picha, Getty Images
''Alicheza vizuri sana. Yeye huwa mzuri sana katika mechi kama hizi ambapo timu zinalinda lango'', alisema Guardiola said.
''Yeye ni miongoni mwa wachezaji bora zaidi kukutana nao''.
Licha ya kuwa na masikhara mengi katika safu yao ya ulinzi , City ilitawalamchezo huo kwa kipindi kirefu.













