Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 10.08.2019: Dybala, Sanchez, Aubameyang, Lacazette, Mustafi, Lovren, Neymar

Alexis Sanchez

Chanzo cha picha, Alex Morton

Roma wamefanya mazungumzo na Manchester United kuhusu uwezekano wa kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez, 30. (Telegraph)

Wachezaji wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang na Alexandre Lacazette, ambao wanadaiwa kusaini mkataba mpya na klabu hiyo wanajadiliana kuhusu kurefushwa kwa mikataba yao. (Sun)

Paris St-Germain wanataka kumsaini mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala baada ya uhamisho wa nyota huyo wa miaka 25 kwenda kutibuka. (Mail)

Paulo Dybala

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Paulo Dybala

Juventus itaendelea kupokea ofa ya kumuuza Dybala na wako tayari kumkabidhi kiungo huyo kwa klabu yoyote isipokuwa Inter Milan. (Calciomercato)

Kipa wa Manchester United David de Gea bado hajatia saini mkataba mpya baada ya kukubali mkataba mpya wa miaka sita na United mwezi uliopita.(Sun)

Arsenal wako tayari kupokea ofa ya kumuuza beki wa Ujerumani Shkodran Mustafi, 27, na kiungo wa kati wa Misri Mohamed Elneny, 27, kutoka kwa vilabu vya Ulaya. (Evening Standard)

David de Gea

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, David de Gea, Kipa wa Manchester United

Roma wanashauriana na Liverpool kuhusu mkataba wa thamani ya euro milioni 20 (£18.6m) kumhusi beki wa Croatia Dejan Lovren, 30. (Football Italia)

Real Madrid na Barcelona huenda wakamng'ang'ania mshambuliaji wa PSG na nyota wa Brazil Neymar, 27. (AS)

Chelsea wanajiandaa kutumia £200m kuwasajiklili wachezaji wapya mwaka huu wanaposubiri kukamilika kwa marufuku ya uhamisho wa wachezaji waliowekewa na shirikisho la soka Duniani FIFA. (Goal)

Neymar

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Neymar

Chelsea watampatia mkataba mpya mlinzi wa chini wa chini ya miaka 21 Fikayo Tomori, 21, baada ya kupinga uhamisho wake kwenda Everton. (Goal)

Bekiwa Argentina Marcos Rojo, 29, alikuwa tayari kujiunga na Everton kwa mkopo kutoka Manchester United, lakini United wanataka kumuuza. (Liverpool Echo)

Manchester United walikuwa wanatafajkari uwezrkano wa kumsajili mshambuliaji wa Athletic Bilbao wa miaka 25 Mhispania Inaki Williams kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa. (El Chiringuito, via Manchester Evening News)

Marcos Rojo

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Marcos Rojo (kulia)

Winga wa kimataifa wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, atasalia Crystal Palace hadi Januari dirisha la uhamisho wa wachezaji litakapofunguliwa baada ya mwenyekiti wa klabu hiyo Steve Parrish kusema hatapinga uhamisho wake katika klabu ya Ulaya . (Express)

Kiungo wa kati wa West Ham na England Declan Rice, 20, amesema mwaka huu anayetazamia kukabiliana na mchezaji mpya wa Tottenham Mfaransa Tanguy Ndombele, 22 . (Talksport)

Declan Rice

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kiungo wa kati wa West Ham, Declan Rice

Mshambuluaji wa Ubelgiji Eden Hazard, 28, amekabidhiwa jezi nambari saba ya Real Madrid- iliyovaliwa na Cristiano Ronaldo alipokuwa akichezea klabu hiyo. (Mail)

Mshambuliaji wa LA Galaxy Zlatan Ibrahimovic alitumia maneno makali kuukosoa mfumo mpya wa michuano ya soka ya ligi ya Major . (ESPN)

Mshambuliaji wa zamani wa Stoke City Saido Berahino, 26, amejiunga na klabu ya Ubelgiji ya Zulte Waregem kwa uhamisho wa bila malipo. (Mail)

Eden Hazard

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mshambuluaji wa Ubelgiji, Eden Hazard

Nahodha wa Crystal Palace, Luka Milivojevic ametia saini mkataba mpya wa miaka minne. (Talksport)

line

Tetesi Bora Ijumaa

Kiungo wa kati wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, amepata pigo baada ya uhamisho wake kwenda Everton kutibuka lakini amesisitiza anataka kuondoka Selhurst Park. (Telegraph)

Zaha anahofia amepoteza nafasi ya kuhama kwa kitita kikubwa imepotea baada ya dirisha la uhamisho wa wachezaji kufungwa siku ya Alhamisi. (Mail)

Wilfried Zaha

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wilfried Zaha

Meneja wa Palace Roy Hodgson alimzuia Zaha kufanya mazoezi siku ya Alhamisi kwa sababu mchezaji huyo ''hakuwa na utulivu wa kiakili'' baada ya kuwasilisha barua ya kuomba uhamisho. (Mirror)

Real Madrid wanaamini wamemkosa kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 26, baada ya United kutoimarisha safu yake ya kati siku ya mwisho wa uhamisho wa wachezaji.

Klabu hiyo inayoshiriki ligi ya Uhispania maarufu La Liga, badala yake imeelekeza darubini yake kwa mshambuliaji wa Paris St-Germain na nyota wa kimataifa wa Brazil Neymar, 27. (Marca)

Hofu ya kikosi cha kwanza kitakacho cheza chini ya meneja mpya wa Chelsea Frank Lampard imemfanya beki wa Brazil David Luiz, 32, kushinikiza uhamisho kwenda Arsenal. (Standard)

Neymar Jr. alipojiunga na Paris Saint-Germain

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Neymar

Tottenham walipata pigo baada ya Sporting Lisbon kukataa kupunguza bei ya kiungo wao wa kati Mreno Bruno Fernandes, 24. (Mirror)

United ilipuuza nafasi ya kumsajili mshambuliaji Moise Kean kutoka Juventus, kabla ya kiungo huyo wa miaka 19 kujiunga na mahasimu wao Everton. (90min)