Europa League: Kocha wa Chelsea apandwa na hasira akijiandaa kuvaana na Arsenal

Chanzo cha picha, Getty Images
Kocha wa Chelsea Maurizio Sarri alionekana mwenye hasira alipoondoka katika ukumbi wa mazoezi saa chache kabla ya fainali ya ligi ya Europa dhidi ya Arsenal nchini Azerbaijan.
Mtaliano huyo ambaye amehusishwa na tetesi za kuhama Chelsea, alirusha na kisha kupiga teke kofia yake katika uga wa Baku Olympic Stadium.
Awali mshambuliaji Gonzalo Higuain na mlinzi David Luiz walirushiana cheche za maneno baada ya kutofautiana.
Chelsea imesema hatua ya Sarri haikuwa na uhusiano "wowote na mmoja wa wachezaji wake".
Klabu huyo inasema Sarri alikasirika kwa kuwa"hakuweza kufanya mazoezi na wachezaji wake kama alivyopanga" kwasababu uwanja huo ulikuwa wazi kwa wanahabari.
Kumeibuka tetesi pia kuhusu hatma ya Sarri katika uwanja wa Stamford Bridge, lakini amesema ataungumza na klabu hiyo baada ya fainali hii.

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, PA

Chanzo cha picha, Getty Images









