Watford 0-1 Arsenal: Pierre-Emerick Aubameyang airudisha Arsenal nafasi ya nne

Chanzo cha picha, Reuters
Arsenal yafanikiwa kurejea tena nafasi ya nne katika jedwali la ligi ya premia baada ya ushindi wake dhidi ya Watford
Kosa la Ben Foster na kadi nyekundu iliopewa Troy Deeney iliisaidia Arsenal kurejea tena nafasi ya nne bora baada ya kuishinda Watford bao 1-0.
Kipa Foster aliwatunuku Gunners bao la ufunguzi katika dakika ya 10 alipozembea kuchukua mpira baada ya kupewa pasi ya nyuma, Pierre-Emerick Aubameyang alitumia nafasi hiyo kumfikia na kutia mpira kimyani.
Dakika moja baadae, nahodha wa Watford Deeney alilishwa kadi nyekundu kwa kumshambulia usoni kiungo wa kati wa Arsenal Lucas Torreira.
Licha ya kusalia na kikosi cha wachezaji 10 kwa dakika 80, Watford ilitishia lango la Arsenal kupitia mkwaju mzito wa Adam Masina kutoka mbali katika kipindi cha pili, na kumlazimu kipa wa Arsenal Bernd Leno kuwa muokoaji hodari wa mabao.
Mjerumani huyo alimkosesha bao Craig Cathcart kwa kutumia mguu wake muda mfupi baada ya Deeney kulishwa kadi nyekundu- na hata free-kick ya Etienne Capoue haikuzaa matunda.

Chanzo cha picha, Rex Features
Gunners hatahivyo hawakucheza vizuri licha ya kupata bao la ugenini ambalo ni muhimu kwao katika kinyang'anyiro cha kuwania kufuzu kwa ligi ya mabingwa msimu ujao.
Wamepanda hadi nafasi ya nne katika jedwali la ligi ya premia, alama mbili mbele ya Manchester United alama moja bele ya Chelsea kutokana na tofauti ya bao moja.
Nyakati mbili zilizoiponza Watford
Iwapo mashambulizi ya Watford yangeliishia kufunga bao wangelijinyakulia alama tatu za wazi katika mchezo huu; ushindi ambao ungewawezesha kuchupa kutoka nafasi ya 10 hadi ya 7 katika ligi ya Premia.
Badala yake walipoteza nafasi mbili katika sekunde ya 95.

Baada ya mmoja wao kulishwa kadi nyekundu, Watford walifanya mashambulizi makali katika dakika 20 za mwisho ili kusawazish bao walilofungwa, badala ya kutafakari uwezekano wa Arsenal kuwafunga bao la pili.
Laiti Watford, na hasusan Gray, angelitulia katika eneo la cha penati, pengine huenda wangelijizolea angalau alama moja.
Gunners pia hawakua makini walipopata nafasi ya kupenya safu ya mashambulizi huku mcheze wao ukionekana kuwa wa kasi ya chini japo tayari walikua katika nafasi ya ushindi.Arsenal ilikua imeshinda mechi mbili za ugenini mwaka 2019 kabla ya mechi hii.
Utendakazi wao wakiwa uwanja wa nyumbani imewafanya wapewe heshima ya nafasi ya tatu bora katika ligi hii - hali ambayo imewafanya kupambana kufikia nafasi ya nne bora.
Ushindi wao wa ugenini usiotabirika imewapatia matumaini ya kufikia ndoto zao.
Meneja wa Watford Javi Gracia, akizungumza na BBC michezo: "Najivunia sana wachezaji wangu. Sna haja na matokeo, tulipata nafasi lakini hazikuzaa matunda na pia wachezaji wangu 10 waliwatoa kijasho wapinzani wao
"Naheshimu uamuzi wa refa. Kwa mtazamo wangu ilikua wazi amekosea, pengine angelipeana kadi ya njano na wala sio kadi nyekundu. Sikubaliani na uamuzi huo.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Troy amesikitika sana. Hii ilikua mechi muhimu sana kwetu, na alifahamu hilo. Kukosa huduma yake ilikua kibarua kigumu kwetu."
Meneja wa ArsenalUnai Emery akizungumza na BBC michezo: "Tulikua nia mchezo mzuri lakini tungelifanya vizuri zaidi. Hatuweza kufunga bao la pili na ukweli ni kwamba hatukuweza kudhibiti mpira . hasa katika safu ya mashambulizi.
"Matokeo haya ni muhimu, na mechi hii kulingana na tathmini yetu imetupatia ukamavu zaidi.













