Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 16.03.2019: Sterling, Courtois, Rodriguez, Giroud, Suso, Umtiti, Valencia, Dubravka

Raheem Sterling

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Raheem Sterling

Real Madrid ina mpango wa kumnunua mshambuliaji wa Manchester City na England Raheem Sterling, 24, kama sehemu ya kuimarisha kikosi chake. (Mirror)

Meneja wa Real Zinedine Zidane amemuonya kipa wa klabu hiyo Mbelgiji Thibaut Courtois, 26, kuhusiana na utendakazi wake mbaya siku za hivi karibuni. (Sun)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amefutilia mbali uwezekano wa klabu hiyo kuwasajili wachezaji wapya. Badala yake Klopp ameongeza kuwa mpango weka ni kuimarisha timu iliyopo sasa kufikia kiwango cha juu zaidi cha uchezaji kwa 100% . (Mail)

Jurgen Klopp

Chanzo cha picha, Rex Features

Maelezo ya picha, Jurgen Klopp, Meneja wa Liverpool.

Mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo, 34, huenda akachukuliwa hatua na Uefa baada ya kuonekana kana kwamba anawwapia mashabiki wa Atletico Madrid wakati wa mechi ya ligi ya mabingwa. (La Gazzetta dello Sport - in Italian)

Mlinzi wa Ufaransa Samuel Umtiti, 25, amesema kuwa angelipendelea kujiunga na Manchester City ama Manchester United ikiwa ataondoka Barcelona msimu huu. (Calciomercato - in Italian)

Mshambuliaji wa Chelsea, mfaransa Olivier Giroud, 32, amesema haoni uwezekano wake wa kuendelea kuchezea klabu hiyo endapo ataendelea kucheza nafasi yake ya sasa. (Sun)

Olivier Giroud

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Olivier Giroud (Kushoto)

Meneja wa Muda wa Manchester United Ole Gunner Solskjaer ameamua ni wachezaji gani wataondoka Old Trafford msimu huu wa joto, huku beki wa kulia Antonio Valencia,33 akiwa na uhakika wa kuondoka kwake. (Manchester Evening News)

Arsenal inaaminiwa kuwa moja ya vilabu vinavyopania kumsajili Valencia, baada ya baba yake kuthibitisha kuwa mchezaji huyo atahama Manchester. (Metro)

Gunners wako katika hatari ya kumkosa mkurugenzi wa zamani wa kiufundi wa Roma, Monchi, baada ya klabu ya La Liga, Sevilla, kufanya mazungumzo na mhispania huyo wa miaka 50. (Metro)

Monchi (Kushoto) Mkurugenzi wa kiufundi wa zamani wa Roma

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Monchi (Kushoto) Mkurugenzi wa kiufundi wa zamani wa Roma

Arsenal pia inaongoza katika kinyan'ganyiro cha usajili wa mshambuliaji wa AC Milan, raia wa Uhispania Suso, 25. (Mirror)

Meneja wa Newcastle, Rafaeal Benitez amedokeza kuwa ana matumaini ya kumshawishi kiungo wa kati Isaac Hayden asihame klabu hiyo.

Tayari kiungo huyo wa miaka 23 ameomba kupewa uhamisho mara mbili. Benitez ana amini mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal ana nafasi nzuri ya kuchezea timu ya taifa ya England. (Chronicle)

Tetesi Bora Ijumaa

Arsenal na Leicester zote zina hamu ya kumsajili mchezaji wa Celtic na mlinzi wa Scotland Kieran Tierney, mwenye umri wa miaka 21.

Arsenal na Leicester zote zina hamu ya kumsajili mchezaji wa Celtic na mlinzi wa Scotland Kieran Tierney

Chanzo cha picha, SNS

Maelezo ya picha, Arsenal na Leicester zote zina hamu ya kumsajili Kieran Tierney

Leicester inamtaka Tierney aichukue nafasi ya mlinzi Ben Chilwell wakati wakitarajia maombi kuwasilishwa kwa mchezaji huyo. (Mirror)

Gunners imefanya mazungumzo na winga wa zaidi ya miaka 21 wa Rennes Ismaila Sarr. Arsenal imeipiku klabu hiyo ya Ufaransa kufika katika robo fainali ya Ligi ya Uropa Alhamisi. (Goal France)

Juventus itafanya kila iwezalo kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, mwenye miaka 20, kutoka Paris St-Germain msimu huu wa joto. (Tuttosport)

Kylian Mbappe

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kylian Mbappe

PSG itamkabidhi meneja Thomas Tuchel mkataba wa mwaka mmoja zaida. Raia huyo wa Ujerumani alisaini mkataba wa miaka miwili mnamo Mei 2018.(L'Equipe)

Manchester United wamejiunga katika kutaka kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa PSG Adrien Rabiot, wa miaka 23. Raia huyo wa Ufaransa hana mkataba ifikapo msimu wa joto na tayari amezungumza na Barcelona, Arsenal, Chelsea na Tottenham. (Sun)