Floyd Mayweather: Raia huyo wa Marekani anasema kuwa atapigana na Manny Pacquiao baadaye mwaka huu

Floyd Mayweather na Manny Pacquiao

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mayweather na Pacquiao walitarajiwa kugawana takriban $230m (£150m)baada ya pigano lao 2015

Floyd Mayweather atatoka katika kustaafu ili kupigana na Manny Pacquiao katika pigano la marudiano baadaye mwaka huu

Wawili hao kwa mara ya kwanza walikutana mjini Las Vegas mnamo mwezi Mei 2015 , huku Mayweather akishinda kupitia kwa wingi wa pointi.

Mayweather alichapisha kanda ya video katika mtandao wa kijamii ikiwa na maandishi: Narudi kuzipiga dhidi ya Pacquiao mwaka huu. Pigano lenye malipo ya pesa nyingi linakaribia.

Bondia huyo mwenye umri wa miaka 41 hajapigana tangu pigano lake na nyota wa UFC Conor McGregor mwezi Agosti 2017.

Alitanagaza kustaafu baada ya kumpiga knockout Conor katika raundi ya kumi na hivyobasi kuweka rekodi yake kuwa mapigo 50 bila kushindwa.

Maelezo ya video, Hassan Mwakinyo: Bondia Mtanzania asema maisha magumu yamechangia ushindi wake

Mkutano wa kwanza kati ya Maywqesther na Pacqiiayo lilikuwa ushindani mklai katika historia ya ndondi likitajwa kuwa pigano la karne.

raia wa Uinfereza Amir Khan pia amekuwa na hamu ya kuzipiga dhidi ya Pacquiao baada ya kumshinda samule Vergas mapema mwezi huu.