Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 03.07.2018

Chanzo cha picha, Getty Images
Juventus wameanza mazungumzo na Real Madrid kumchukua mchezaji wa kiungo cha mbele wa Ureno Cristiano Ronaldo, kuelekea Italia. (Marca)
Chelsea ipo tayari kujadiliana kubadilishana mshambuliaji wa Uhispania Alvaro Morata, mwenye miaka 25, arudi katika klabu yake ya zamani Juventus ili kwa upande wao wampate mchezaji wa kiungo cha mbele wa Argentina Gonzalo Higuain, mwenye miaka 30. (La Gazzetta dello Sport )
Itambidi mlinzi wa Uholanzi Daley Blind, mwenye miaka 28, apate kato la kipato ili kuweza kujiunga tena na Ajax kutoka Manchester United msimu huu wa joto. (Telegraph)
Huddersfield na Wolves wana hamu ya kumsajili winga wa Middlesbrough Adama Traore mwenye miaka 22. Mhispania huyo amefungwa kwa mkataba wenye thamani ya £ milioni 18m zinazohitajika ili aruhusiwe kuondoka. (Sun)
Kipa wa Leicester City na Denmark Kasper Schmeichel, atalengwa na Chelsea iwapo klabu hiyo itamuuza M'belgiji Thibaut Courtois, mwenye miaka 26, na Roma iwapo watamuuza mchezaji wa Brazil Alisson, 25. (Sky Sports)

Napoli wameacha kumuwania mchezaji wa kiungo cha kati wa Italia na Manchester City Jorginho, mwenye miaka 26, kutoka orodha yake ya waliomo kwenye kambi yake ya mafunzo kabla kuanza kwa msimu. (Manchester Evening News)
Aliyekuwa kipa wa Juventus na Italia Gianluigi Buffon, mwenye miaka 40, anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili na mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain mwishoni mwa Juma. (L'Equipe)
Uhispania imemratibu aliyekuwa meneja wa Watford Quique Sanchez Flores kuwa meneja wake mpya baada ya kufutwa kwa Julen Lopetegui mkesha wa kuanza Kombe la Dunia kwa hatua ya kujiunga na Real Madrid. (AS)
Huddersfield inamlenga mshambuliaji wa Leicester na Nigeria Ahmed Musa, mwenye miaka 25, na beki wa kushoto wa Hertha Berlin na timu ya taifa ya Ujerumani Marvin Plattenhardt, mwenye miaka 26. (Mirror)
Kipa wa West Brom Ben Foster, mwenye miaka 35, anakaribia kukamilisha uhamisho wenye thamani ya £ milioni 2.5 kwenda Watford. (Telegraph)

Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea inataka Euro milioni 80 ili kumuachia mchezaji wa kiungo cha mbele wa Brazil, Willian huku Barcelona na Manchester United zikionyesha hamu ya kumsajili mchezaji huyo wa miaka 29. (Mundo Deportivo)
RB Leipzig inatarajia kuishinda Manchester United katika kumsajili beki wa kushoto wa Nottingham Forest wa miaka 16 Matthew Bondswell. (Mail)
Bosi wa Celtic Brendan Rodgers na mwenziwe wa Rangers, Steven Gerrard wote wana hamu ya kumsajili winga wa Wales Harry Wilson, wa miaka 21, kutoka klabu yao ya zamani Liverpool. (Sun)
Mmiliki wa Aston Villa Tony Xia amewashangaza maafisa wa klabu hiyo kwa kudai kwamba hataki kuwauza wachezaji kwa timu za Marekani. (Mirror)













