Mourinho asema 'adharauliwa'

Chanzo cha picha, Getty Images
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema ''anadharauliwa'' na vyombo vya habari licha ya rekodi yake kama meneja.
Raia huyo wa Ureno amekashifiwa kwa njisi anavyowachukulia beki Chris Smalling na Luke Shaw msimu huu.
United wameshidwa kufunga bao lolote katika mechi nne zilizopita.
Mourinho ameongoza timu ya Chelsea kushinda mara tatu katika ligi ya Premia ,na ameogoza mara mbili katika ligi ya mabigwa barani ulaya.
Manchester United watakuwa wenyeji wa Arsenal siku ya Jumapili katika uwanja wa Old Trafford.
Mourinho anadai vyombo vya habari vinastahili kumuheshimu meneja wa Arsenal,Arsene Wenger.








