Masaibu ya wakimbizi wa Darfur

Wakimbizi wanaoishi katika kambi moja huko Darfur wanaelezea masaibu yao miaka 5 tangu watimuliwe makwao.

Hamisa akiwa katika kambi ya Hassa Hissa Darfur 2007
Maelezo ya picha, Zaidi ya miaka 10 tangu kuzuke mapigano Darfur zaidi ya wenyeji milioni mbili wamelazimika kutoroka makwao
Hamisa akiwa bado katika kambi hiyo Hassa Hissa Darfur 2014
Maelezo ya picha, Hamisa alitoroka nyumbani kwake mwaka wa 2003 baada ya wavamizi kuwashambulia na bunduki.Alitorokea milimani akiwa amembeba mmoja wa wajukuu wake
Wanachama wa muungano wa wakulima
Maelezo ya picha, Ukulima ndio uti wa mgongo wa Wasudan Kusini.Kukuibuka vita mifugo mimea na mali ya watu huporwa na kuharibiwa.
Kambi ya Zinglei
Maelezo ya picha, Kuna zaidi ya kambi 27 katika eneo la kati la Darfur
Mkimbizi akijenga nyumba ya kudumu ya matofali katika kambi ya Hamadia Kusini mwa Darfur
Maelezo ya picha, Kufuatia mapigano yaliyodumu kwa muda mrefu sasa wakimbizi wameanza kujenga nyumba za kudumu katika kambi hizo za wakimbizi wa ndani kwa ndani
Wenyeji wakiangalia kisima kipya kikichimbwa Khamsa.
Maelezo ya picha, Amina (aliyevalia nguo ya kijani kibichi)anaonekana hapa miaka 7 iliyopita katika kisima cha Khamsa.
Amina akichungulia dirishani
Maelezo ya picha, ''Bado tunakabiliwa na changamoto tele baada ya kuishi hapa kwa zaidi ya miaka 10''anasema Amina ambaye mwenyewe anamtoto mwenye umri wa miak 9
Yusuf akiwa katika kambi ya Aslam 2014
Maelezo ya picha, Kupata mapato kambini ilikuwa ngumu sana wakati huo kwa Yusuf ambaye alikuwa amejifunza kuoka mikate . Kwa sasa ameoa na anafamilia ya watoto watatu.
Haja akiwa amembeba mjukuu wake
Maelezo ya picha, Haja akiwa na kifunga mimba wake Horan mwaka wa 2007 katika kambi ya Hassa Hissa
Haja akiwa ameketi kitandani akimtizama mjukuu wake
Maelezo ya picha, Licha ya kuhama kutoka mako moja hadi mengine maisha bado ni yaleyale tu kwa Haja sasa yeye pamoja na wajukuu wake ni vijakazi wa nyumbani.
Sasa mtizame Rawia akiwa karibu na kisima cha maji
Maelezo ya picha, Rawia alitoka kwakwe mikono mitupu pamoja na mumewe na wanawe .Alikuwa ni mabaki ya chakula na pipa la kutekea maji.
Wanawake wakiwa nje ya vyumba vyao
Maelezo ya picha, Mapigano haya huko Darfur yanapembe tofauti kwa hivyo ni vigumu kusuluhisha. Kuna wale wanaopigana na serikali,kunawale wanaopigana kwa misingi ya Dini. Kwa mujibu wa UN zaidi ya watu 390,000 walitoroka makwao mwaka huu.
Kinyozi katika kambi ya Khamsa Dagiag iliyoko Darfur
Maelezo ya picha, Mkataba wa kusitisha mapigano ya mwaka wa 2011 haukudumu kwani waarabu hawaamini wakristu weusi ambao wengi ni wakulima.
Mwanamke akichorwa na henna miguuni
Maelezo ya picha, Wanawake wa Darfur wakijipaka Hinna tayari kwa hserehe kambini.
Viongozi wa jamii wakizungumza kwa simu ya mkononi
Maelezo ya picha, Viongozi wa jamii wanapewa heshma lakini wanasema ukosefu wa ajira umepelekea vijana kuwapuuza na wakati mwengine hata kuwakaidi.